Kwa jinsi waarabu (DP) wanavyosifiwa na viongozi wetu, ni vyema sasa waarabu wakainunua na CCM pia

Zanzibar-ASP

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2013
Posts
11,550
Reaction score
40,697
Viongozi wetu wametuambia muarabu wa Dubai aliyeuziwa bandari zetu zote za Tanganyika atahakikisha anaongeza mapato ya kutosha, ajira za kudumu maradufu na mapato shazi hivyo tumuunge mkono.

Sasa kwa kuwa CCM imekuwa chama cha kudumu hapa Tanzania na kwa zaidi ya miaka 60 ya umiliki na uendeshaji wa serikali ya Tanzania bado maendeleo yamekuwa ya kusuasua, ni wakati muafaka sasa kwa CCM ikajiuza kwa muarabu wa Dubai ili maendeleo yaje chap chap.

Makada wa CCM tengenezeni mkataba chap chap, mambo yaende haraka ili mkutano mkutano mkuu wa CCM uitishwe kwa dharula ili muarabu wa Dubai achukue chama haraka iwezekanavyo, maendeleo yaje haraka haraka.

CCM Oyeee!
 
Wakaorodheshwe kwenye masoko ya hisa ADX na DFM waarabu wawasaidie taarifa kusomana!
 
🤣
 
Wapewe CCM waimiliki milele.
 
Kweli Kabisa
 
Lkn tuambiane ukweli tu, hapo bandarini hakukuwa na tija yoyote. Ilikuwa ni wizi mwanzo mwisho.

Na kelele nyingi zinapigwa kwa na wanufaika wa wizi kwa kuwa wanajua Sasa mkate wao kushney.
Sasa si ndio maana unaambiwa Serikali ya ccm ibinafsishwe.
Serikali imeshindwaje kudhibiti huo wizi bandarini Kwa kutumia Sheria zetu? au Sheria za Tz zinaruhusu wizi na ufisadi?
Imeshindwa kufunga mifumo imara kudhibiti huo wizi?
Imeshindwa kuajili hata wataalam kutoka mataifa mengine ili kusimamia hizo bandari?
Hiyo hoja ni dhaifu Sana na haihalalishi bandari zetu kugaiwa bure na milele kwa wageni.
Je hao wageni nao wakiwa wezi utafanyaje na ushawakabidhi milele?
 
Lkn tuambiane ukweli tu, hapo bandarini hakukuwa na tija yoyote. Ilikuwa ni wizi mwanzo mwisho.

Na kelele nyingi zinapigwa kwa na wanufaika wa wizi kwa kuwa wanajua Sasa mkate wao kushney.
Sawa kabisa. Kwahiyo ili kukomesha huo wizi na kuongeza tija ndo tunampa mwarabu. Kwa maana hiyo hiyo sasa, tumpe na CCM pia maana nayo imejaa majizi na hakuna ufanisi!
 
Lkn tuambiane ukweli tu, hapo bandarini hakukuwa na tija yoyote. Ilikuwa ni wizi mwanzo mwisho.

Na kelele nyingi zinapigwa kwa na wanufaika wa wizi kwa kuwa wanajua Sasa mkate wao kushney.
Serikali inamiliki Jeshi, uhamiaji, TISS, polisi na magereza inashindwa kusimamia bandari?????

Tuseme tu Saa100 anafanana na mimi kwa kweli!

Leo JPM akafufuka akakuta Tunatoa bandari zote Za bara hadi ziwa Victoria pale kwa wakwe zake Busisi
atapiga yule mama kwa Kweli.
 
Kwani JPM yeye ndo nani!?
Huwa aliyetuibia 1.5t!
MunguMtu wenu huyo alishindwa ht kuajiri tu for 6yrs.
 
Na kwa mlivyo wajinga waabudu mizimu nyie mpk leo bado mnawaza eti atafufuka!!
 
Lkn tuambiane ukweli tu, hapo bandarini hakukuwa na tija yoyote. Ilikuwa ni wizi mwanzo mwisho.

Na kelele nyingi zinapigwa kwa na wanufaika wa wizi kwa kuwa wanajua Sasa mkate wao kushney.
Hatupingi ubinafsishaji, tunapinga mkataba mbovu, baasi!
Mkataba wowote wenye tija ni wazi kabisa utaongeza ufanisi ktk bandari zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…