Kwa kampeni yenu hii, mtawatoa wote lakini hamtaweza kuyafuta waliyoyafanya

Hao uliowataja hawajawahi kushutumiwa na bunge kwamba wawajibishwe.
 
pole sana naona ume join jF mwezi huu
 
Huyu kiturilo ni new member. Atakuwa Makonda mwenyewe amezingua kazini kutapatapa.

Kwa uovu ambao wanazi wa Magufuli wanawafanyia watanzania,wakubambikia watu makesi na kumdharau raisi wa awamu ya sita,bora waondolewe tu.
 
Hapa ndio umechemsha,yuko wapi sasa kama walisalim amri,wameshibda tena kwa KO ,wanakula nchi kilainiii
 
Hao watu wako unawapa sifa nyingine ambazo sio zao, mkataba wa ujenzi wa flyover ya tazara umesainiwa wakati wa Kikwete na Magufuli akiwa waziri wa ujenzi.
 
Kila utawala unaudhaifu wake na hakuna utawala hata mmoja kwa baadhi ya watendaji wake wakakosa chembechembe za ufisadi, unamkumbuka, Lugola alikuwa na kashfa na kesi ilikuwa iko mahakamani na uwaziri akapewa mwisho akatumbuliwa tena, Yuko wapi Kichele wa TRA mnakumbuka kashfazilizokuwa zinamkabili , mnamkumbuka makonda RC Dar huyu amepata utajiri wa haraka lkn mamlaka haikutaka kusikia malalamiko ya wananchi juu ya kashfa alizolishuwa toka kwa wananchi mbalimbali, je tunamkumbuka Sabaya Dc hai huyu alilamikiwa sana kwa kashafa mbalimbali alifanywa nn, tusiuonde utawala wa mh. Samia na kuupa credit utawala wa awamu tano eti ndio utawala bora kuliko zote. Kipindi cha awamu ya tano unajua tenda mbalimbali zilivyokuwa zikipatikana? Nani alikuwa anahusika na manunuzi ya vitu mbalimbali kwenye taasisi mbalimbali za serkali? Manunuzi yalikuwa siri na ilikuwa hakuna kuhoji
 
Minyonyo bhana! Yaani kama siyo Yehova Yire kutenda miujiza ina maana mlikuwa mmeshajimilikisha Taifa na msingetoka artificially.

Kwani hao mawaziri waliwekwa wa kudumu? Kwa hiyo manyonyo hayatakiwi kuguswa?

Mbona mliwatoa wajukuu wa akina Marialle, Sina, Eliufoo ila hatukulalama zaidi ya kuchapa kazi? Au sisi ni nguruwe kwa hiyo mkuki kwetu ni halali?
 
Serikali ya awamu ya tano ilikuwa ya ovyo ovyo sana kwani kazi yao kubwa ilikuwa ni kuleta uchonganishi tu kwa wananchi dhidi ya serikali zilizopita hii haikuwa sawa kwani hata Nyerere akiwa rais alikuwa na madhaifu yake lakini serikali ya awamu ya pili haikuangaika kuponda madhaifu ya serikali iliyopita ilijaribu tu kurekebisha pale ilipoona kuna mapungufu alikadharika Mzee Mkapa naye alifanya hivyo hivyo na hata Kikwete alifanya kama watangulizi wake lakini Magufuli alikuwa mtu wa ovyo yeye ni kama alikuwa akijiona ni binadamu wa aina yake na alijifanya kujua kila kitu.
 
Katiba mpya ndio dawa ambayo itaweka mihimili na vyombo vya usimamizi huru na kuwajibika. Bila hivyo kila rais atakuja na proriries zake, watu wake, interests zake binafsi na za kundi lililombeba. Ndio mamma JPM aliingia na wajomba na wengine wa kanda yake. Mpunguzieni rais madaraka, imarisha bunge, promote demokrasia, tengeneza tume huru ya uchaguzi, fuateni sheria za nchi nakila kitu kitakaa vzr.
 
Hoja yako ni nini hapa! Mfu yupo anaoza Chato na mambo yake yote!
 
Eti Magenereta yalikosa Soko!!!... Wakati ndio yameuzika Kwa wingi na bado yanauzika!!...Hivi unadhani kuna mtu Hati standby Generator kama ana uwezo wa kulipata?!!...
 
Acha kulialia hata JPM aliwatoa watu wa JK acha kulialia
 
We ulitaka wabaki kufanya nini? Si walikwiba na kuharibu uchumi wa Nchi?

Ni watatoka wote kwani nyie mliwaacha wote waliokuwa awamu ya 4?

Ukae na majitu ambayo hayaendani na wewe kwa ajili gani?

Mwisho naona mnatapatapa sasa ,ni hivi hakuna mtu aache kutatua kero za wananchi eti ahangaike sijui kufuta sijui huo upumbaymliuweza nyie watu wa visasi kwenye awamu yenu sisi tunachapa kazi nyie endeleeni kutapatapa kama mfa maji na kazeni maana 2035 sio kesho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…