Dkt JK alivyoingi madarakani alihakikisha washikaji/marafiki wananeemeka. Ingawa yeye Mzee wetu Dkt JK hakuwa fisadi na hana hulka ya wizi (angalia historia yake tangu akiwa CCM). Rafiki wa Dkt JK ndiyo waliomponza. Alivyoingia Dkt Magufuli yeye aliondoa wote wenye vinasaba vya wizi. Uzuri uchunguzi na faili la kila mtendaji wa serikali lilikuwa na kila kitu hivyo kuifanya kazi ya Dkt Magufuli kuwa rahisi na kutamka kwa kujiamini yeye ni mtumbua majibu. Wezi wote wa mali za serikali waliogopa/wakaunda kila aina ya zengwe, wakatumia kila aina ya vyombo vya habari kumchafua Dkt Magufuli ila mwisho wa siku wote wakaona wameshindwa kabisa. Wakaenda mbali na kufanya vikao vya vikundi vya chama kumsengenya, ila mwisho wa siku wakasalimu amri. Mama Samia serikali yake iko tofauti na Dkt JK na Dkt Magufuli. Tumsimlaumu Mama kufagia wateule wa Dkt Magufuli na kurejesha wenye kashfa. Hata Dkt Magufuli alimrejesha Mwigulu na Simbachawene wakati waliondolewa kwa kashfa. Hakuna anayepinga Dkt Mwigulu alihusika na kuhujumu mali za CCM, ila Dkt Magufuli alimteua tena kushika nafasi mara ya pili baada ile ya mambo ya ndani. Nadhani siasa na vetting zina zaidi ya uzalendo. Inategemea nani anamfanyia vetting na uhusiano/rushwa ili kusafisha faili na kupeleka recommendation kwa mamlaka za uteuzi. Njia pekee ni kuwa na mfumo unaoruhusu ushindani! Hivyo sidhani kama ni sahihi kumshitumu Mama eti anaondoa watu wa Dkt Magufuli.