Kwa kasi hii ya Azam Wachina wa StarTimes wajiandae kufungasha virago?

Kwa kasi hii ya Azam Wachina wa StarTimes wajiandae kufungasha virago?

Shida nyingine kwa azam ikinyesha mvua au mawingu ya mvua tu. utaona no signal
 
Jamiiforums ni sehemu ndogo sana ya maisha yetu. Hiko kisimbuzi cha Star times mnavyokisakama kila siku humu mpaka juzi nikaona takwimu ndio kinachoongoza kwa mbali sana kuwa na watumiaji wengi Tanzania.
Tupe hiyo takwimu tuione hapa ili tuamini.
 
Mimi nilidhani DStv ndio mpinzani mkuu wa Azam Tv, Kulinganisha Azam na Star Tv ni sawa na kulinganisha Yanga iliyofika fainali na Makolo
Eti platinum member, mduanzi sana wewe kubi
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Na hii ndo shida kubwa ya Azam
Asilimia 60 ya channels zao ni za hovyo.
 
Kwa kasi hii ya Azam wachina wa Startimes wajiandae kufungasha virago?

Naona Azam media wanazidi kuja kwa kasi leo hii wamezindua minara ya bilioni 50 mikoa 21

Baada ya Dish wamekuja na vya Antenna, hawa jamaa wapo vizuri sana naona kwa sasa Wachina wa Startimes wajiandae kisaikolojia tu maana sidhani kama kuna mtu timamu atatumia vile vidubwashwa vyao.

Kongole Azam media sasa huku kwa vya Antenna ndo mnaenda kusepa na nyomi ya kijiji.
Ni ngumu sana,Kwa base ya Wateja star times ana wateja mara 2 ya Azam sas Hadi aje amkute sio Leo.
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Bilioni 50 haitoshi kuonesha EPL mkuu
 
Antenna unafanya kazi km 30 Kutoka city center ya mkoa wa lindi sijui kwa mikoa mingine...maybe hiyo minara itasaidia
 
Mapungufu ya Azam na ST
Mechi za ulaya (EPL)
Channel za documentary
Channel za dini (international)
Channel za movie ( hata za 2020 hazipo sana sana wataonyesha movie za 80s na 90s tena zenye quality mbovu sana
Channel za music
Channel za nchi jirani ( Rwanda, Burundi, Uganda)

Kwa ufupi Azam na Startimes wote hakuna kitu, DStv atawaburuza sana
DSTV ni ulimwengu mwengine kabisa
 
Natamani ving'amuzi vya DSTV, Startimes au Azam wawe na option ya mtu kuchagua channels anazotaka tu, sio mrundikano wa channels nyingi zisizo na maana.
Kwenye DSTV hiyo option zipo zaidi ya 3..unaweza ku BLOCK channel ambazo huzitaka na option ya pili unauqezo wa kutengeneza Groups za Channel unazotaka uangalie wewe na group lengine waangalie familia au group la Muziki pekee au channel za Dini n.k
 
Star times wapo vizuri azam ameteka soko kwa sababu anaonesha ligi ya bongo ndio kinachombeba kama star times atanunua haki ya matangazo kuonesha ligi kuu Tanzania bado kila mtu atakikimbilia kisimbuzi cha star tomes
 
Atanunua lini wakati Hadi mama anarudi kisiwandui mwaka 2030 Azam bado ana mkataba na TFF?
 
Kwenye DSTV hiyo option zipo zaidi ya 3..unaweza ku BLOCK channel ambazo huzitaka na option ya pili unauqezo wa kutengeneza Groups za Channel unazotaka uangalie wewe na group lengine waangalie familia au group la Muziki pekee au channel za Dini n.k
Hizo option za groups ni sawa, nilichomaanisha ni kama umeenda supermarket unachagua bidhaa unazotaka then unalipa, so niwe naweza kuchagua hata channels zangu tano then wananipa total nalipia either kwa siku, wiki, au mwezi, niwe na option ya kuUpdate nikitaka.
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Bil 50 kufunga backhaul na minara ajili kurusha matangazo kwenda antenna miba .....badala ya dish vile vidogo
 
Bilioni 50 kusambaza antena? Badala ya kulipia EPL??

Azam bado sana...hawana channels za maana kabisa ...hata channels za South Africa Tu hawana hata moja
Minara mikoa 21 watasambaza matangazo yao robo 3 ya Tanzania wanasitaili pongezi
 
Back
Top Bottom