Shoctopus
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 3,435
- 1,995
Wanabodi.
Kwa Kasi Hii ya Rais Wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli na Falsafa yake ya "Hapa Kazi Tuu", na kama hiki tunachokiona sio nguvu ya soda tuu, yaani ataendelea kwa kasi hii hii hadi 2020, kuna haja ya kufanya tena uchaguzi wa rais?, si tumwache tuu aendelee?.
1. Kwa kazi hii nzuri anayoifanya rais wetu, Dr. John Pombe Joseph Magufuli, hivi kweli Tanzania, tuna haja tena ya kufanya kchaguzi wa rais kwa mwaka 2020?, au tumwache tuu aendelee mpaka 2025?.
2. Jee hatuwezi kufanya uchaguzi wa wabunge tuu na madiwani, bila kufanya uchaguzi wa rais, kwa Magufuli kupita bila kupingwa, na badala yake , ili kuokoa pesa, mali na muda?, na Magufuli apewe tuu a walkover ya kuendelea hadi 2025?!.
3. Au kwa vile Uchaguzi wa Rais ni takwa la kikatiba, hivyo uchaguzi huo lazima tuu ufanyike hata kama ni wastage of time, money and resources?!.
4. Na hiyo 2025 tukimuona bado anaweza, na anatufaa, jee kuna ubaya kuibadili katiba yetu tumpatie extension of time ya kutosha kuinyoosha Tanzania hadi inyooke kabisa?!.
5. Kwani katiba ni nini?,si ni kipande tuu cha karatasi?!, nini muhimu kati ya kipande cha karatasi na umuhimu wa Magufuli kwa taifa?!.
6. Na Katiba ni ya nani?!, ni yetu?!, na iko kwa manufaa ya nani?!, si ipo kwa manufaa yetu?!, hivyo sisi ndio muhimu kuliko katiba, tukimtaka Magufuli, si tunaweza kuiweka tuu katiba pembeni tukaendelea na Magufuli wetu?!.
7. Sasa kama Magufuli anatufaa sana, na katiba haitamruhusu kuendelea baada ya 2025, kuna ubaya gani kuibadili katiba kwa manufaa yetu?!,
8. Au kwani Katiba ni Msahafu kusema haiwezi kubadilishwa?!. Jee kuna ubaya kama Magufuli akipatiwa muda wa kutosha kama Kagame, Museveni au kama Mugabe?.
9. Na jee kuna ubaya wowote wapinzani wa Tanzania mkiamua kwa kauli moja msisimamishe tena mgombea urais, na badala yake CCM tuu ndio iwe inatoa rais siku zote kufuatia long eksipirience ya CCM na uzoefu wa muda mrefu kwa CCM kwenye urais?.
10. Na kufuatia somo la urais wa Zanzibar, na kilichofanyika kwenye urais wa JMT, kweli wapinzani makini bado kweli watahitaji kusimamisha mgombea kushindana na Magufuli?! 2020?, kutakuwa ni kugombea au kujifurahisha tuu?!, au hata ikitokea huyo mgombea wa upinzani ameshinda atatangazwa?!.
Hayo ni maswali tuu nimeanza kujiuliza aloud?!.
Jee wewe una maoni gani kuhusu hoja zangu hizi?!.
Paskali
Kuna wengine labda watakuona queer, lakini sio Mimi:
1. Katiba haiandikwi kwa ajili ya MTU mmoja au kizazi kimoja tu. Katiba lazima izingatie maslahi ya nchi ambayo ni mapana zaidi ya uchaguzi mmoja uliomweka rais madarakani.
2. Uchaguzi huru na wa haki hatujawahi kuushuhudia hapa kwetu, wewe wajua. Na hili so lawama au credi kwa mtu au chama bali kwa mfumo mzima.
3. Katiba sio "kipande cha karatasi" kama wewe unavyoelewa! Katiba ni sheria, tena ni mama wa sheria zote, ni falsafa, ni mwongozo, ni mila etc. na si lazima iwe written eg.: (UK constitution)
Ukiiona katiba kama kipande cha karatasi kamwe hutaiheshimu na hutaheshimu sheria nyingine zote.
4. Rais ni taasisi, sio MTU. JPM ni binadamu, na we we unajua maumbile ya binadamu; hatuko perfect. Inaonekana mwenzetu hutofautishi vitu hivyo viwili kwa sababu zako.
5. Sio busara kubadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja au kikundi kimoja cha watu (chama). Katiba ndio msingi wa Mihimili mitatu ya Utawala (DOLA). Katiba ndio kielelezo cha mipaka ya mamlaka ya Bunge, Mahakama na Serikali. Katiba ya nchi ni zaidi ya vitu mnavyoita "TUNU" kmf. Kiswahili. Leo nikisema kiswahili kimedumaza elimu yetu mtasemu siheshimu tunu za taifa! lakini Katiba ya nchi mnaiita "kipande cha karatasi" Hiki ni kiroja.
6. Kwahiyo ukibadili au kufuta Katiba kwa faida ya MTU mmoja (sio taasisi)!!! matokeo yake umefuta mamlaka ya mihimili mitatu ya DOLA. Maana yake unasimika UDIKTETA. Na kuna udikteta wa MTU mmoja na wa kikundi cha watu, vyote ni haramu.
7. Mfano: Huwezi kumfanya jaji wa mahakama asifuate tena sheria, eti kwasababu umeshinda kesi au alifuta kesi yako!
Huwezi kusema eti: 'Kwasababu Bunge limetunga sheria nzuri tusiwe na uchagizi wabaki wabunge hawahawa mpaka lini sijuwi!! Dunia itawashangaa.
9. Swali unalowauliza wapinzani ungewauliza CCM kwanza kama wako tayari kuendesha uchaguzi ulio huru na wa haki na kuwapa wapinzani Serikali iwapo watashinda kihalali? Kwasababu wapinzani hawatumii polisi ili washindwe kila uchaguzi. Bali siku zote mwenye nguvu ya dola ( incumbent); asiyeheshimu katiba, akiona mambo yake hayaendi anavyotaka yeye hutumia nguvu.
Kwa hayo machache naishia hapo. Umeleta mada nzuri, ila kama lugha yangu imekukwaza kwa namna yoyote niwie radhi baba.