Kwa kasi ya Mchina na Electric Vehicles (EV), sio muda tutapishana nazo Dar

Duh! gari za umeme maintenance ni gharama sana hata marekani ambako Tesla ndio chimbuko lake...kwa gari za umeme bado sana kulikamata soko maana uzalishaji wake inavoonekana ni gharama sana pamoja na miundombinu wezeshi hasa Africa safari kufikia huko bado sana
 
Dar nishakutana na gari kadhaa za umeme pure, sio hybrid, ni umeme pure kwa sasa tuna mudu Nissan Leaf model ya kwanza, nyingi ni 30kwh yaani ikiwa battery ikiwa na 0% itahitaji umeme wa unit 30 kujaa yaani umeme wa shilingi 10,715 kujaa, ambapo wengi wanasema inawapeleka kati ya 200 na 250km ndipo chaji kwisha ambapo ni very economy, andaa kama 20mill hivi kupata 1st generetion ya nissan leaf kuipata yenye battery health nzuri kabla hatujaanza kuwawaza akina BYD na Tesla
 
Nakukatalia, maintainance gani ya gari la umeme ni ghali? Gari la umeme ni gharama kulinunua sio kuli maintaine
 
Haya magari yanahitaji pull factors pia, mfano kuanza kufunga mfumo wa kuchajia wa public.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…