Hili jambo linahitaji utafiti wa kina tena wa muda mrefu ili kupitia maeneo yote kwa uhakika.kwasababu kusema tu kwamba idadi kubwa ya wagonjwa wa kansa kanda ya ziwa chanzo kinaweza kua matumizi ya formaline kwenye kuhifadhi samaki napata mashaka kwasababu samaki wa ziwa victoria hususani wanaovuliwa ukanda huu wa ziwa kwa upande wetu wanasafirishwa nchi nzima.sasa kwanini wagonjwa wengi wawe ni wa kanda ya ziwa tu.Mimi nadhani maji ya ziwa ndiyo yanatatizo.Tuanze kutafiti kwanza maji kwasababu ziwa victoria ndio chanzo kikubwa cha maji ukanda huo kwahiyo inawezekana yana kitu kinacholeta shida kwa watumiaji.Samaki na formaline tunasingizia tu baada yakukosa majibu sahihi.Ngoja tusubiri majibu ya utafiti.