Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere

Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere

Pascal Mayalla

Platinum Member
Joined
Sep 22, 2008
Posts
53,857
Reaction score
121,995
Wanabodi,
Nchi hubarikiwa kwa viongozi wake kufanya mambo mema.

Kwa kauli hii, ya jana ya Rais Samia alioitoa Bukoba, kwa kutoa msamaha wa jumla wa deni la kodi, za nyuma, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote!. Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kufanywa na Rais yeyote ukimuondoa Nyerere abaye serikali yake ilikuwa haibanani kabisa na issues zozote za kodi.

Wakati TRA wanajipanga kutekeleza nia hii safi ya Rais Samia, pia tuweke a defined framework ya utekelezaji, tusije tukarudi kule kule, kwa TRA ikiona muda wa mwaka unakaribia huku hujalipa madeni yako ya kodi, then for sure makufuli ya TRA yatashuka tena madukani na ule mkono mrefu wa TRA utarejea tena kuingia ndani ya accounts za benki za wadaiwa sugu na kukomba kila kitu kilichomo!.

Mungu mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali
 
Haiwezekani, atalaaniwa tu kwa ukatili anaowafanyia Watanzania wa Ngorongoro, laana tupu hata afungue Misikiti 100.

Isitoshe jambo ambalo nimejifunza maishani ni kwamba low IQ people wanapenda sana bure na cheap popularity ambayo haina uhalisia, nchi masikini na yenye shida kila mahali haiwezi hata kulipa mahitaji muhimu ni ya kusamehe kodi? Anasamehe kodi kwa kigezo gani ? Vipi mwajiriwa anayekatwa kila mwisho wa mwezi? Fairness iko wapi ?

Ni lini Nyerere alitaka watu wasilipe kodi ?

Ashushe bei ya Mafuta, Umeme hayo mengine hatuhitaji!
 
Hakika kwa kauli hii, watanzania tunapaswa kuiunga mkono.

Hao TRA ndiyo walioua biashara nyingi, Katika utawala wa awamu ya 5 chini ya Mwendazake, kwa kudai kodi hata za miaka 5 ya nyuma!🥺
 
Huo ni utapeli wa mchana kweupe, sheria haziondolewi jukwaani bali ni kwa kubadilishwa na kuweka kwenye maandishi. Kama sheria haijaandikwa kwenye vitabu, ukienda kwenye mamlaka za wakusanya kodi, wanakuambia kabisa hayo ni mambo ya majukwaani, na ni lazima utalipa. Hivyo huu utapeli wapelekeeni wanaomini siasa za kiki.
 
Sheria haibadilishwi jukwaani,
 
Haiwezekani, atalaaniwa tu kwa ukatili anaowafanyia Watanzania wa Ngorongoro, laana tupu hata afungue Misikiti 100.

Isitoshe jambo ambalo nimejifunza maishani ni kwamba low IQ people wanapenda sana bure na cheap popularity ambayo haina uhalisia, nchi masikini na yenye shida kila mahali haiwezi hata kulipa mahitaji muhimu ni ya kusamehe kodi? Anasamehe kodi kwa kigezo gani ? Vipi mwajiriwa anayekatwa kila mwisho wa mwezi? Fairness iko wapi ?

Ni lini Nyerere alitaka watu wasilipe kodi ?

Ashushe bei ya Mafuta, Umeme hayo mengine hatuhitaji!
Hapa umemaliza
 
Haiwezekani, atalaaniwa tu kwa ukatili anaowafanyia Watanzania wa Ngorongoro, laana tupu hata afungue Misikiti 100.
Wewe acha kumbwela mbwela. Ardhi yote iko chini ya rais kikatiba. Hata hicho kibanda cha babu yako Samia anaweza kuamua pawe sehemu ya watoto wa mtaaani kwako kuchezea (open space). Cha msingi tiini mamlaka Kama maandiko yanavyoagiza.
 
Mambo ya kujikosha tu ana andaa mazingira ya 2025.
Wewe ulitakaje? Huko huko kujikosha ndio kutamfikosha 2030..

Kama.vipi na wewe kajikoshe..By the way kwa kujikosha huko huko ndiko kumemuwesesha sasa amepandish mapato kutoka Til.1.3 kwa mwezi hadi Til.1.8 kwa mwezi kwa mwaka mmja tuu..

Jiwe amestruggle weeee hamna kitu 👇👇
 
Attachments

  • Screenshot_20220406-164902.png
    Screenshot_20220406-164902.png
    90.3 KB · Views: 19
  • Screenshot_20220406-163449.png
    Screenshot_20220406-163449.png
    53.8 KB · Views: 19
Huo ni utapeli wa mchana kweupe, sheria haziondolewi jukwaani bali ni kwa kubadilishwa na kuweka kwenye maandishi. Kama sheria haijaandikwa kwenye vitabu, ukienda kwenye mamlaka za wakusanya kodi, wanakuambia kabisa hayo ni mambo ya majukwaani, na ni lazima utalipa. Hivyo huu utapeli wapelekeeni wanaomini siasa za kiki.
Utapeli kwani ni dhalimu wako huyo?

Si unapumua wewe?
 
Wewe ulitakaje? Huko huko kujikosha ndio kutamfikosha 2030..

Kama.vipi na wewe kajikoshe..By the way kwa kujikosha huko huko ndiko kumemuwesesha sasa amepandish mapato kutoka Til.1.3 kwa mwezi hadi Til.1.8 kwa mwezi kwa mwaka mmja tuu..

Jiwe amestruggle weeee hamna kitu 👇👇
Hamna kitu kila siku serikali inakopa mbona Jpm alikuwa hakopi kopi hovyo hela??Kama nimekukera ondoka hapa Jf usinikere na majibu hovyo aisee mi nna hasira sana na mwenendo wa huyu mama.
 
Sheria haibadilishwi jukwaani,
Hili ni TATIZO SUGU la wasaidizi wake. TRA inatimiza majukumu yake kwa mujibu wa sheria. Rais hana mamlaka ya kikatiba ya kusamehe mtu kulipa kodi!! Akitaka kumsamehe inabidi huyo mtu ashitakiwe kwanza na kufungwa kisha yeye ndiye ampatie msamaha wa rais. Vinginevyo irekebishwe katiba na kuongeza kipengere cha mamlaka ya Rais kuwa anaweza kumsamehe mfanya biashara kulipa kodi!! Tatizo ni kwamba kama mfanya biashara mmoja umemsamehe kodi utakuwa umeharibu usawa kwenye soko. Aliyesamehewa kodi atawapiku wenzake sokoni maana atashusha bei na wenzake hawawezi kushusha bei na hii si sawa. Wasaidizi wake inabidi wamwambie ukweli!!
 
Hamna kitu kila siku serikali inakopa mbona Jpm alikuwa hakopi kopi hovyo hela??Kama nimekukera ondoka hapa Jf usinikere na majibu hovyo aisee mi nna hasira sana na mwenendo wa huyu mama.
Narudia nenda Kwa Mkeo kamwambie huo ujinga ndio atakuelewa..

Hakuna siku Serikali iliwahi kuacha Kukopa na Wala haitakaa itokee Serikali isikope..

Yule taahira unaemtaja sio tuu alikopa Kwa kificho bali alikuwa ni muongo na mjinga 👇
 
Attachments

  • 2306969_FB_IMG_1581695064971.jpg
    2306969_FB_IMG_1581695064971.jpg
    27.2 KB · Views: 14
  • Screenshot_20220430-075700.png
    Screenshot_20220430-075700.png
    136 KB · Views: 15
Kwa jinsi nisivyowaamini hawa watawala, hii kauli unaweza kuta kwa asilimia kubwa inawahusu na kuwanufaisha wenyewe na washirika wao.
 
Back
Top Bottom