Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere

Kwa Kauli Hii, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote! Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kuwa Rais yeyote ukimuondoa Nyerere

Narudia nenda Kwa Mkeo kamwambie huo ujinga ndio atakuelewa..

Hakuna siku Serikali iliwahi kuacha Kukopa na Wala haitakaa itokee Serikali isikope..

Yule taahira unaemtaja sio tuu alikopa Kwa kificho bali alikuwa ni muongo na mjinga 👇
Wewe endelea kubwata hii nchi inapigwa na familia za watu wachache nahisi nawewe umo ndani ndio maana unatetea ujinga funga bakuli lako usiongee ujinga.
 
Wewe endelea kubwata hii nchi inapigwa na familia za watu wachache nahisi nawewe umo ndani ndio maana unatetea ujinga funga bakuli lako usiongee ujinga.
Ndio hivyo,uliwahi kuona wapi wengi wakipiga? Hata vyeo ni vya wachache,matajiri ni wachache .

Yaani kiufupi ndio kanuni ya maisha 😀😀
 
Huo ni utapeli wa mchana kweupe, sheria haziondolewi jukwaani bali ni kwa kubadilishwa na kuweka kwenye maandishi. Kama sheria haijaandikwa kwenye vitabu, ukienda kwenye mamlaka za wakusanya kodi, wanakuambia kabisa hayo ni mambo ya majukwaani, na ni lazima utalipa. Hivyo huu utapeli wapelekeeni wanaomini siasa za kiki.
KUWA MUUNGWANA, HAO WATU WANALENGO LA KUMHARIBIA MAMA. KWA NINI HAWAKUFANYA HIVYO WAKATI WA JPM. RAIS UWEZO WA KUSAMEHE KOSA LOLOTE AFANYALO RAIA WAKE. KAMA ANAMSAMEHE MTU ALIYEHUKUMIWA KUNYONGWA SEMBUSE KODI?
 
Mkuu elvischirwa , kwenye kuandika au kuripoti tukio lolote kuna kitu kinaitwa angle, unaripoti kwa angle gani, wengi wamezungumzia msamaha wa kodi, mimi angle yangu sio kuhusu Samia kusamehe kodi bali ni kuhusu Samia kubarikiwa.
P
Angle yako ni nzuri sana ila sijui mimi inanihusu vipi kwani sijui abarikiwe kwa lipi kama angle yako haihusu kodi! naomba na mimi nibarikiwe tu angalau kwa kushiriki.
 
Mkuu elvischirwa , kwenye kuandika au kuripoti tukio lolote kuna kitu kinaitwa angle, unaripoti kwa angle gani, wengi wamezungumzia msamaha wa kodi, mimi angle yangu sio kuhusu Samia kusamehe kodi bali ni kuhusu Samia kubarikiwa.
P
Usikwepe uwajibikaji wa andiko lako. Andiko lako msingi wake ni Rais kusamehe kodi wale wenye malimbikizo ya kodi. Kwa hiyo utoaji huo wa msamaha unadai utamfanya mtoaji wa msamaha huo kubarikiwa!! Suala linakuja je unapotenda jambo ambalo linakiuka katiba uliyoapa kuivunja unastahili baraka au vinginevyo? Mayala unajinasibu kuwa wewe ni mwanasheria, je inakubalika kisheria kwa Rais kufanya jambo ambalo hana mamlaka ya kikatiba kulifanya.
Kikatiba Rais ana mamlaka ya kumsamehe yeyote aliyetiwa hatiani na mahakama lakini hana mamlaka ya kumsamehe mtu yeyote kabla ya kuhukumiwa. Kutokulipa kodo au kukwepa kulipa kodi ni KOSA linalohukumika kisheria. Rais asubiri sheria ikamilishe mkondo wake ndio asamehe huyo aliyehukumiwa!
 
2. Heshimi Haki za binadamu ambazo zimeainishwa kwenye Katiba. Kuna uvunjifu wa haki za binadamu mdogo mdogo
Kwenye eneo hili la haki za binaadamu, Mama Samia, apewe kongole sana, huyu ni mpenda haki, muwaza haki, msema haki, mtenda haki.
Ameonyesha kwa kauli na matendo!.
Mifano iko mingi tuu ya kumwaga hapa nakupa mifano mitano tuu!, ukitaka 10, nakupa, ukitaka 20 nakupa
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
Kwenye eneo la haki, so far Rais Samia ameisha onyesha kwa kauli na matendo, is the best of the best... ila sasa kwa kwa kadri siku zinavyokwenda, naona kama na yeye anaanza... itaendelea!, nitamalizia ...

P
 
Wanabodi,
Nchi hubarikiwa kwa viongozi wake kufanya mambo mema.



Kwa kauli hii, ya jana ya Rais Samia alioitoa Bukoba, kwa kutoa msamaha wa jumla wa deni la kodi, za nyuma, Rais Samia atabarikiwa sana kuliko Rais mwingine yeyote!. Huu ni wema mkubwa kabisa kuwahi kufanywa na Rais yeyote ukimuondoa Nyerere abaye serikali yake ilikuwa haibanani kabisa na issues zozote za kodi.

Wakati TRA wanajipanga kutekeleza nia hii safi ya Rais Samia, pia tuweke a defined framework ya utekelezaji, tusije tukarudi kule kule, kwa TRA ikiona muda wa mwaka unakaribia huku hujalipa madeni yako ya kodi, then for sure makufuli ya TRA yatashuka tena madukani na ule mkono mrefu wa TRA utarejea tena kuingia ndani ya accounts za benki za wadaiwa sugu na kukomba kila kitu kilichomo!.

Mungu mbariki Rais Samia,
Mungu Ibariki Tanzania.
Paskali

Leo ndio siku yenyewe ya wanawake duniani, hongera sana kwa wanawake wote duniani akiwemo Mwanamke huyu!.
P
 
Back
Top Bottom