Kwa kauli hii ya Rais Samia, ni wazi kwamba watu wanamdharau (wanamchukulia poa)

"2025 mtaamua wenyewe muwalete walioleta matozo au muwatoe"

Unapata picha gani kwa kauli hii, Mama keshachokwa na hapa ni miezi tisa tu.
Aache kupitisha bakora ili wananchi waamue wamtakaye.
Spika huwa ananifanya niichukie CCM kwa udhaifu wake.
 
Unapomuita mtukufu mama yetu unadhani kuna lipi bora sana amelifanya kwa taifa kiasi mtu ukikaa unasema kweli hapa huyu amefanya jambo jema?

Kingine yupo mwenzake alijidanganya kuyaona ya mwaka kesho sasa hivi tumeshamsahau hiyo 2025 aliyekwambia atafika nani?
 
Tatizo sio Samia tatizo ni CCM. Ni bora huyo Samia kuliko wahuni wengine wa ki CCM. CCM wizi umo ndani ya Damu zao
 
'…akitaka kufanikiwa akubali kuwa 'chizi' kama yule Jamaa…'
 
Huwenda haamini kawa Raisi maana kila siku anasema kuna mambo yanaendelea chinichini na hatumuoni akichukua hatua yoyote

Watoto wa mjini washamzidi kete..
Akina miguru wanapiga hela za tozo mpaka anasinzia. Makatani February anapiga za kulazimisha kwenye umeme. Ila sisi wabongo wametusoma uboya.
 
Aanze na mshauri wake anayemdanganya kusafiri nje kwa kigezo cha kufungua nchi kumbe anampoteza, akimalizana na huyo ndio aje kwa vijana wa mjini maana ndio wanamtia nuksi katika uongozi wake…
We utakuwa haupo sawa kichwani,kwaiyo Rais asisafiri ajifungie ndani Kama yule msukuma mwenzenu na mkristo mwenzenu!?

Wasukuma mmevurugwa
 
Anamuonea tu MBOWE mijizi inajichotea tu na hana cha kuifanya

Huko kwenye hilo Stigler"s gorge na SGR ndiko wanakojichotea watakavyo kwani wameishaambiwa liwe na lisiwe hiyo miradi lazima iishe!!! Wanaiba sana na hao WATURUKI na wale waarabu wa Egypt; kunahitajiaka usimamizi wa karibu sana wanapolipwa hawa contractors!!i
 
Embu weka rekodi zako sawa sawa, huyu mama sio mpole, bali mtu asiyejua chochote na asiye na ushawishi wowote kwenye jamii na siasa za nchini. Hajui kusoma alama, nyakati wala majira ya kisiasa. Anabahatisha kwa 99%.
 
Tulishauri hapa Kuwa kipindi kile mama asafishe Team ya JPM yote alete Team yake watu kama kina Makubi au Dorothy Gwajima Wananchi hatuelewi sarakasi zao kabisa, Mama anasogeza karibu watu ambao wanatamani nafasi yake 2025, Mama asafishe kabisa
 
Mwigulu na Makamba ni kundi moja?

Sent from my TECNO KA7O using JamiiForums mobile app
Hao ni watu wawili tofauti wenye nia moja. Wote wana tamaa iwe ya mali ya haraka,iwe madaraka. Wote wawili hawana nia hata moja ya kuwatumikia Watz hata nusu,ila wamejaa tamaa za upigaji tu. Wote ni wapigaji. Wote wawili wanautaka urais iwe asubuhi,iwe mchana. Mwingine alichora na mawe yote. Wote wana nia ya kumuangusha mama ili waangalie fursa ya kugombea hiyo nafasi.
 
Tulishauri hapa Kuwa kipindi kile mama asafishe Team ya JPM yote alete Team yake watu kama kina Makubi au Dorothy Gwajima Wananchi hatuelewi sarakasi zao kabisa, Mama anasogeza karibu watu ambao wanatamani nafasi yake 2025, Mama asafishe kabisa

Samia asipoangalia atakuja vuta shuka wakati kumekucha!!! Hizo kauli za wakina Ndugai ni ishara tosha kuwa akae mguu sawa!!!
 
Nenda kenya tatizo mnataka kumfanya raisi kama Mungu kama anakosea anapaswa kusemwa hadharani kama raisi wa US anaweza kunyooshewa dole la kati na mwananchi ana haki kama hampe di kufanya hivo sio kosa itakua kwa raisi wa tz?
Acheni hizi tabia za kipimbi za kuwataka watu wahame nchi aisee, kwani huwezi kujenga hoja zako bila ya kumtaka mtu ahamie Kenya?
 
Kipindi kile Zackia Menghji nae alilalamika kuandamwa na watu sababu ya jinsia yake alipotunukiwa moja ya wizara nyeti za nchi hii. Leo namsikia tena Mama
 
Wewe mshauri wako akiwa mwiguru na makamba ujue umepigwa,tena mchama kweupe

Ile nafasi ya Mwigulu amuondoe amuweke yule mama aliyeko DEFENCE; mambo yake yatatulia ama sivyo kila siku atalalamika!!! Huyo Mwigulu ndio genge moja na wakina MSUKUMA; mama zinduka!!!
 
Hakuna kukaa pembeni,mama akomae akicheka na wahuni,atavua mabua.
 
Alisimamia mradi gani wa kimkakati ukakamilika?
Umeme tulikuwa hatu lali giza, Agrecco, Symbion, iptl kampun zote za kitapel alifukuza na umeme ukawepo, na wagonjwa wa kwenda India walipungua %99 na Marehem Dk mengi akapunguziwa mzigo wa kusafirisha wagonjwa kwenda nje, na hospital mama zetu na dada zetu waliacha kujifungulia chini ya sakafu, na kulala kitanda kimoja wajawazito 6

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…