Uchaguzi 2020 Kwa kauli hizi za Dkt. Magufuli, Je atakuwa tayari kuachia madaraka kama atashindwa Uchaguzi?

Uchaguzi 2020 Kwa kauli hizi za Dkt. Magufuli, Je atakuwa tayari kuachia madaraka kama atashindwa Uchaguzi?

Ataachia atake asitake , nchi sio yake na mzmlaka yote yanatoka kwa wananchi , soma katiba hapa , ikibidi nguvu ya umma
IMG_20200802_165717_7.jpg
 
Japo Waliosema Mwana mpumbavu ni hasara kwa mamaye enzi zao zimepita miaka miaka mingi sana lakini wakati wanasema hayo ni kama walikuwa wanamuona mtu fulani wa siku hizi
 
Japo Waliosema Mwana mpumbavu ni hasara kwa mamaye enzi zao zimepita miaka miaka mingi sana lakini wakati wanasema hayo ni kama walikuwa wanamuona mtu fulani wa siku hizi

Walimuona nani?
 
Kwa kuangalia tu uitikio wa wananchi kwenye mikutano ya JPM ni wazi wananchi washaamua kwenda na Magufuli.
Kwenda naye wapi? Yani mimi mimi mimi nichague jiwe [emoji848][emoji848][emoji848][emoji848]
Bado sana bora Rungwe kama Lissu asipokuwepo
 
Watu wanajikaza tu kisabuni lkn ukweli hata wanaccm wenenyewe hawaitaki ccm
 
Haya sasa jaman move yetu inaanza kunoga bado pushup tu mambo yakamilike
 
Ndugu zangu wapendwa naomba tutafakari kwa kina kuhusu kauli zilizotolewa na Magufuli kwamba hayupo tayari kuacha taifa likaangamia, liingie mikononi mwa matapeli na waongo.

Kwa kauli hizi inaonyesha wazi, kwamba Magufuli yeye tu ndio mtakatifu na mwaminifu, ila wagombea wengine ni matapeli na waongo. Sasa swali langu ni hili je hao matapeli na waongo wakichaguliwa na wananchi yeye atakubali kuachia madaraka?

Ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ndugu yetu anaamini peke yake ndiye anayestahili kuliko wananchi wengine wote. Kama wananchi wameona hao ni watu sahihi wewe ni nani hata useme ni matapeli? Je hii siyo dalili ya kubaki madarakani kwa nguvu? Nini maana ya Uchaguzi? Kwani taifa linakuwa tu salama likiwa mikononi mwake?

Je hili taifa siyo mali ya Mungu? Ni nani anayeweza kulifanya taifa liwe salama zaidi ya Mungu?

Naomba tujadili maana hii kauli imenishitua sana.
Je! Anti atakubali kushindwa uchaguzi huu
 
Akishindwa na nani?? kuna mgombea anayetarajia kumshinda Magufuli kweli!!!!! hebu kuweni serious jamani, baada ya uchaguzi hao wanaojita wagombea wazuri, wanagombea lakini wana tiketi za ndege mkononi tarehe 1novemba watakuwa hawapo. Bahati nzuri watanzania wameshabaini
 
Hana tabia ya kujionyesha ila kazi kubwa aliyoifanya inajionyesha. Ana hofu kuwa wakishika madaraka wataharibu alichoanzisha.
 
Chadema wanayo haki ya kutoamini kushindwa kutokana na utendaji wa tume. ni mgombea yupi wa ccm amewahi kuenguliwa? kwa nini wakurugenzi walikuwa wanawahujumu wapinzani wakati wa mchakato wa kuchukua na kurudisha fomu? Kwa nini Magufuli aliwahi kutamka kwamba hawezi kukubali mkurugenzi amtangaze mpinzani kwa sababu anamlipa yeye? Kwa hiyo chadema wanasimamia kauli na matendo ya serikali
Wagombea wenu ni wa kuokotez, ccm hawajaenguliwa hata upinzani hawajaenguliwa wale wote waliokuwa wabunge, mlipashwa kuwasaidia wagombea wenu wapya, imekula kwenu msilalamike subirini kipigo.
 
Yaani watu waache kuchagua Chama cha Siasa wachague chama cha kijamii
 
Kwanza inashangaza kuona tume iko kimya kukemea haya, ina maana tume iliteua matapeli na waongo kugombea nafasi ya urais Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?
Unazungumzia tume hii aliyoiteua yeye? Tume wako kama wamemwagiwa maji
 
Nataka Siku Moja Nikifika Mbinguni Niwe Hata Mfagizi Wa Malaika, [emoji3][emoji16][emoji23][emoji28][emoji1][emoji2]
Mgombea Nafasi Ya Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
Kwa Tiketi Ya Chama Dola
Nani kamdanganya jiwe kuwa ataenda mbinguni?
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Yeye ni motoni tu
 
ANASHINDWAJE UCHAGUZI WAKATI ANAWAFIKIA WAPIGA KURA NA LISSU ANAWAFIKIA MASHABIKI NCHI HII WAPIGA KURA HAWAPO MIJINI ANAPOPITA LISSU WAPO MAWILAYANI NA VIJIJINI ANAPOPITA MAGUFURI KAMA UNAKILI USHAELEWA NANI MJANJA
Kwa akili yako na mimi siyo mpiga kura? Pathetic
 
Back
Top Bottom