Kwa kauli za Mbowe na Mdude ni wazi Ole Sabaya ataachiwa huru

Binafsi naamini hao jamaa waliachiwa kwasababu hapakuwa na ushahidi wa kuwatia hatiani wahukumiwe vifungo gerezani, lakini kwa Sabaya na ushahidi uliotapakaa kila mahali dhidi yake, sioni ni kwa namna gani atapona, tuiache mahakama ifanye kazi yake na mashahidi wa kesi yake wasibughudhiwe kwa namna yoyote.
 
Ni kweli mkuu na mimi wala sipingi katiba mpya na lakini pia sikubaliani na matamshi ya hivi kuyapa uhalali wa kuwa ndio njia ya kudai katiba.
Mfano wa wakenya si lazima na sisi tuutumie, utajiuliza Kenya kila uchaguzi lazima wauane je na sisi tuige njia hiyo pia ndio haki itendeke?

Kwa upande wangu naona hapana bali tunaweza kukaa meza moja na majibu yakapatikana vizuri tu bila kuandamana na kumwaga damu za watu wasio na hatia.

Kingine maoni yangu niliyo yatoa hapo ni kulingana na hali ya kisiasa kwa sasa ilivyo, rais anauwezo wa kutumia mahakama kuumiza watu ama kufurahisha watu.
 
Sawa mkuu, ila nadhani kuwa wewe ni wakwanza kuamini kuwa hawa hawakubambikiwa kesi.
Sawa ngoja tusubiri.
 
Mahakama ni kama bendera na serkali ni upepo

USSR
 
Ni kawaida sana mtu aliyeumizwa, kuonewa au kupigwa kutoa kauli zisiofaa kwakuwa Kisaikolojia wanakuwa bado hawapo sawa kutokana na maumivu waliyoyapitia.

Wote tunajua kadhia waliyopitia viongozi wa Chadema kwa kipindi chote cha miaka 6. Hivyo sishangai kusikia hizi kauli zao.

Kuna ulazima wa Rais akutane nao kama alivyoahidi kisha awatulize wafanye Siasa kwa amani.
Rais asiseme tena yeye na mtangulizi wake kuwa wao ni kitu kimoja.
 
Kwahiyo ni haki yao kutoa kauli za hivyo?
 

Mama alisifiwa kwa kutenda haki baadhi ya sehemu, lakini iliwekwa wazi kuwa hatutaki utawala wa hisani bali tunataka utawala wa sheria, na huo ni ndani ya katiba mpya. Ni kipi ulikuwa huelewi hapo?
 
Kwahiyo ni haki yao kutoa kauli za hivyo?
Ndio ni haki yao kuongea hivyo.
Kumbuka hizi kauli zao zimesababishwa na kauli alizoongea Rais Juzi kuhusiana na Katiba mpya na shughuli za Siasa.

Kumbuka hawa Chadema ni waathirika wa utawala wa Magufuli. Na kauli za Rais bado zinaendeleza maumivu yao badala ya faraja kwao, Ndio maana unawaona wamepaniki na kuongea hivyo.

Kule Bungeni 99% ni CCM watupu hivyo hiki ni kipindi kizuri sana kwa wabunge wa CCM kupitisha katiba kule Bungeni, maana wapo wenyewe tupu.
 
Kwahiyo ni haki yao kutoa kauli za hivyo?
Hizo kauli zinazokuumiza leo zimekuwa zikitolewa hadharani na yule rais muovu pamoja na genge lake, lakini wakati huo ulichekelea ukisema nchi inanyooshwa. Leo wengine wanaonyesha hisia zao kwa mateso waliyopatiwa kwa uonevu, unaona wanakosea!

Ni hivi, kama kweli huyo rais unataka tuone hiyo nguvu yake, sio kumtaka achukue hatua dhidi ya wapiga maneno ya siasa maana hayana madhara kwetu, bali mtake achukue hatua ya upotevu wa 24b zilizopotea kwenye halmashauri ya jiji la Dar, ama achukue hatua kwa hao waliojiunganishia bomba la mafuta. Sasa mnaacha kumpima rais kwa mambo ya msingi, mnamjaza muone nguvu zake dhidi ya kauli za wahanga wa utawala wa kihayawani wa Magu!?
 
Mm nashauri mama aachane na hawa wapinzani uchwara na hata asikutane nao.

Hata hivyo vikao vya ndani piga marufuku. Hawa wapinzani uchwara wabatufanya tuone matendo haram ya jiwe kua yalikua sahihi. Wanampiga mkwara mama? Stupidity kabisa.
 
Swala la katiba mpya rais kusema kwamba apewe muda ashughulikie uchumi kwanza sio sahihi kwani inaonekana ni mbinu tu ya kupoteza muda ili 2024 aje aseme muda umeisha tusubiri baada ya uchaguzi.

Ni aibu kubwa sana kwa chama kilichokaa madarakani kwa "Silver Jubilee" nzima kuogopa katiba mpya inayotokana na maoni ya wananchi na kutegemea katiba yao wenyewe eti ndio iwabebe kubaki madarakani.

Kwa hiyo ccm inakiri kwamba haina ubavu wa kupambana na wapinzani wake kwenye uwanja ulio sawa na kwamba wenyewe lazima wabebwe tu ili wabaki madarakani. This is very stupid and naive.
 
Mwachieni tukutane kitaa akiwa sio DC atajua kuwa haajui mamaeeee
 
Mama alisifiwa kwa kutenda haki baadhi ya sehemu, lakini iliwekwa wazi kuwa hatutaki utawala wa hisani bali tunataka utawala wa sheria, na huo ni ndani ya katiba mpya. Ni kipi ulikuwa huelewi hapo?
Nadhani mkuu wewe ndie ambaye hukunielewa tangu kwenye mada hapo juu na ndio mana nikarudia tena maelezo hayo.

Alafu pia ni ukweli usio pingika kuwa uungwaji mkono na kusifiwa alikosifiwa mama kulitokana na hisani hiyo hiyo unayo ikataa kwa kuzitumia mahakama kufuta kesi za wanasiasa ambazo iliaminika na watu kuwa zilibambikwa pamoja na nyingine nyingi ili kufurahisha makundi kadha wa kadhi, mfano kundi la dini e.g mashekhe wa uamsho, kwa wafanya biashara watu Kama kina Papaa Musofe wako huru, wanasiasa ndio kabisaa kina Mdude, Mbowe na wenzake hawa yote yamefanyika lengo moja tu kurudisha imani iliyo potea enzi za mtangulizi wake wakiamini hawajatendewa haki.

Na ndio mana nasema kwa mawazo yangu hata huyu Sabaya pia yupo ndani ya kimbunga hiki hiki cha kutafuta imani ila tu yeye amekuwa mbuzi wa kafara tena ukizingatia katokea pale pale sebuleni kwa Mbowe, huyu Sabaya ni adui wa pili wa Mbowe baada ya marehemu. Kwangu mimi binafsi kinacho mkuta huyu ni mbinu tu ya kutuliza hali ya hewa.

Ni kweli tunadai katiba lakini si kwa njia ya kumpa amri rais na vitisho vya kunyolewa kwa hapo hatuwezi kufika mkuu.
Na hata hizo hisani hatuta ziona tena badala yake itatumika dola Kama nyakati zilizopita tu na nasema hata huyu Sabaya atakuwa huru muda si mwingi.

Okay, ni maoni yangu lakini.
 
Mwachieni tukutane kitaa akiwa sio DC atajua kuwa haajui mamaeeee
🤣🤣 Sasa mkuu utamfanya nini unadhani mbona yule Makondakta wa daladala anadunda mtaani wakati alipigwaga ban hadi na Pompoe?
 
Huu ni uongo mkubwa umeandika. Sijasikiliza hotuba ya mbowe hivo siwezi kusema chochote, lakini kuhusu hoja yako kwamba Mbowe alikuwa ametulia wakati wa JPM huu uongo nenda ukawadanganye vijiwe vya kahawa.
Nikukumbushe tu, Mbowe alimkosoa sana JPM kuhushu jinsi ya kushughulikia Covid na pia alililia sana Democrasia na uhuru wa mahakama.
 
Kwahiyo wakisha mpa vitisho rais vya kumnyoa ndio ataogopa kisha atawapa katiba mpya?
 
Ndugu usitishwe na hivi vitisho..sisi huku uswahilini huwa tunamisemo yetu..DEBE TUPU HALIACHI KUTIKA.. Pia husema...KELELE ZA MLANGO HAZIMKOSESHI USINGIZI MWENYE NYUMBA.....Kwani uliona au kusikia wapi ..KELELE ZA CHURA ZINAMZUIA NG'OMBE KUNYWA MAJI? Relax!
 
Watu wa pwani wanasema UKICHEZA NA MBWA ATAKUFUATA HADI MSIKITINI mama anecheza nao acha wamfuate hadi msikitini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…