Kwa kauli za Mbowe na Mdude ni wazi Ole Sabaya ataachiwa huru


Kwa taarifa yako hata kama hao cdm wangelala chini rais apite juu ya migongo yao, bado huyo Sabaya angetoka tu. List ya waovu waliofaidika na uovu wa Magu ni pamoja na huyu mama. Hivyo hakuna namna mama angeweza kuchukua hatua za ukweli dhidi ya mtu muovu, wakati yeye binafsi ni mfaidika wa huo uovu huo aliofadika nao Sabaya. Kama alikuwa anacheza maigizo kutuonyesha kuwa anapambana na uovu, mshauri tu aache, bali tunawaka katiba mpya.Na kama atachukua hatua zozote kutokana na maneno ya Mdude, basi atakuwa ni rais mwenye uwezo duni kweli kweli.
 
Mtoa mada kuliko kuposti huu ujinga ungetupostia hata jinsi unavyokataga gogo tuone mauwezo yako
 
Mkuu kwasasa hapa mimi nazungumzia political atmosphere tulio nayo kwa sasa ndo mada yangu ilipo sa hayo mambo ya mafuta na sijui wizi na nini mimi hapa sijayazungumzia kabisaa na wala mada yangu haijalenga kupima nguvu ya rais kwenye mambo hayo uliyo yataja hata kidogo na binafsi nina maoni na msimamo tofauti kabisaa juu ya uwezo na nguvu ya rais juu ya mambo hayo ulio yasema hapo labda tutayajadili kwenye mada nyingine hapa mimi naongelea mwenendo wa kisiasa tulio nao.

Na nadhani hata huyo Magu hakupenda kupandwa pandwa kichwani kwa kauli za namna hiyo ndio maana alikuwa mkali sana na kusweka watu ndani ambao ndio hao wanaachiwa sasahivi na huyu mwana demokrasia ambaye haheshimiwi hata kidogo licha ya kujaribu kwa nguvu zote kujipendekeza na bado watu wanataka kumnyoa kwa wembe 😂😂.
 
Kwanza unaonyesha huna akili timamu! Kesi ya Sabaya ipo Arusha kwa uharamia aliyofanya huko. Bado ana kesi nyingine nyingi atakazofunguliwa Moshi kwa uharamia aliyofanya mkoa wa Kilimanjaro.

Hivyo tuliza masaburi mambo bado!
 
Mama alianza kwa makosa mno kutaka kuwaridhisha hawa watu, sasa wameanza kumuonyesha ni watu wa aina gani. Ili nchi hii uiongoze, lazm utumie Magu strategy period
 

Vichekesho sana kwenye kesi hii Mbowe hata hayupo!! sijui kama umefuatilia kesi vizuri
 
Aah mkuu punguza hasira maisha ni haya haya bana tuhame bongo tuende wapi tena?😂
 

Kama ungekuwa na uelewa mpana wa kusoma between the lines, ni kama nakuambia achana na cheap politics. Kuleta mada ndefu hivyo kisha kututajia Mdude kama sehemu ya kupimia siasa za rais, nazo ni kichekesho kingine.

Na kwa taarifa yako Magu hakuwa mkali bali alikuwa ni mtu mwenye jazba, kuna tofauti ya ukali na jazba, ndio maana kaishia kushusha uchumi wa nchi. Magu alikuwa mtu muovu mwenye kiburi cha madaraka, na tunamshukuru Mungu kwa kutuondolea yule dhalimu bila damu kumwagika, apumzike kwa mateso makali huko motoni.
 
Naam hayo ni maoni yako na nayaheshimu pia, lakini kama kauli za kina Mdude na Mbowe mwenyekiti wa chadema hazina impacts zozote kwenye siasa Kama unavyodai hapo ni sawa ngoja tuone maandamano ya nchi nzima yatafanyika kweli ama ni porojo zao za kijinga Kama unavyosema kiasi kwamba hazistahili hata kujadiliwa humu sababu kumbe kauli za mwenyekiti nazo ni za ovyo tu hazina mashiko kujadiliwa.
Tujipe muda tuone.

Okay, huyu mmoja alikuwa na Jazba akasweka watu ndani na kwa kubambikia watu kesi na huyu mwingine naye kaja kawatoa na sasa wanataka kumnyoa na kuandamana kwa lazima hadi tupate katiba mpya (ila kuandamana kwa lazima walishindwa wakati wa yule mwenye Jazba, wanaweza sasahivi wakati wa mtu mpole zao la yule yule muovu!!) Okay ngoja tuone muda ni mwalimu mzuri sana.
 
We umeongea kitu nachowaza na mimi. Yani kuna watu wanaamini kabisa sabaya atavaa jezi ya machungwa. Aha.

Sent from my TECNO K7 using JamiiForums mobile app
 
Chadema ni genge la wahuni rais SS akiwaachia watamsumbua sana ndio maana jpm aliwapiga pini hawana malengo mazuri zaidi kutaka dola kwa fujo
 
Ndio akishtakiwa sabaya na akiachiliwa mdude,mbowe ndio mahakama zinatenda haki hata wakitoa lugha za uchochezi
 
Na wew unashindwa nini kushangilia nje ya mahakama Kama hao unaowwita vibaraka
 
Jiandae wewe umpokee ukalale nae
 
Sabaya akitoka kudadake wachaga watammaliza wenyewe, mbuzi yule kaumiza sana watu, watu wameshajua kuwachekea hawa ngombe kama sabaya ni kujipiga kitanzi mwenyewe, watu wana ushahidi aliyoyafanya, sometimes haki na heshima inakuja mtu akigundua sina nguvu zaidi ya wengine na wote ni sawa
 
Kama awamu hii imeamua kuachana na kesi za kubumba basi iachane na kesi hii ya sabaya maana ni ya kubumba.
 
Hawa vijana ndo Mana tuliachaga kuwa nao kikundi kimoja cha siasa,Siipendi CCM kindaki ndani ila Chadema ni genge la wahuni tu.
Wanamatusi na ushabiki wa kipuuzi sana.Ndo mana now days wanaitwa Nyumbu.

Huyo mama hatumkubali na hao Chadema ni Wana Sacco's ya kisiasa tu.


NCHI HII ITAKOMBOLEWA NA WANANCHI WA KAWAIDA NA SI WAHUNI WA SIASA(Chadema,ccm,act,CUF n.k)
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…