Kwa kichwa cha habari cha gazeti la MWANANCHI la leo Aprili 1, 2022 unajifunza na kugundua nini?

Kwa kichwa cha habari cha gazeti la MWANANCHI la leo Aprili 1, 2022 unajifunza na kugundua nini?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
60,660
Reaction score
121,325
Kinasema...

'Wamerudi Aiseeee"

Tafadhali wale Wabobezi na Wanazuoni wa Lugha adhimu ya Kiswahili tunaomba mje hapa mtuelimisha maana na dhana pana na Neno 'Wamerudi' halafu hapo hapo tena Mtu anasema Neno 'Aiseeee' katika kumalizia.

Karibuni.

Mwananchi.jpg
 
ingependeza kama ungeweka rejea ya hilo gazeti.
Hata Wewe hapo ulipo unaweza Kuliweka kwani hujazuiwa kufanya hivyo au kama ungekuwa na Akili sawa sawa kama huiamini hii Taarifa basi huu muda wako ulioupoteza Kuniandikia hivi ungeitumia kwenda Mitandaoni katika Kurasa za Magazeti ya Leo ili Ujiridhishe nayo.
 
Tanzania Nchi yangu Nzuri na Watu Wapole sana lakini ina mkosi wa kupata Vingozi thabiti. Bandarini vurugu, MSD Vurugu, TANESCO vurugu yaaaani kila Shirika la Umma linavurugwa tuuuu na sidhan kama kuna nia njema tena na Maslahi ya Taifa hili.

Anyway ippo Siku yaja.
 
Ukimuuliza Musiba na Ally Hapi watakupa majibu mujarabu na wanajisikiaje saa hizi.

Ni heri ya kuwa ma viongozi watoto wa mjini kuliko kuongozwa na washamba.

Tawala zote tumeziishi, ogopa mtu anayetaka watu wawe maskini yeye peke yake ndio awe na pesa, halafu kuna wajinga wakaaminishwa kuitwa wanyonge na maskini ndio sifa na uzalendo.

Hawa hawa ndio wanafaa, acha malalamiko, jipange kwenye channel, tengeneza connection na wewe ule mema ya nchi.
 
Inaweza kumaanisha, (wale waliotaka kupotezwa kwa hila na maguvu makuu) wamerudia aiseee (kwa uwezo wa Muumba)!
 
Mie sina muono mpana
najikumbusha tu stori moja na wimbo mmoja

Stori: KARUDI BABA MMOJA Karudi baba mmoja, toka safari ya mbali Kavimba yote mapaja, na kutetemeka mwili Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali Wakataka na kauli.

Wimbo: Malaika Music Band - Amerudi analieee ....anatia hurumaa ... alijua amepata mchongoo

 
Kuelewa mbongo anataka nini ni kazi kwelikweli.
Kipindi cha JK tulikua tunamponda na kumtukana kwelikweli, majina yote ya hovyohovyo tukampachika tukafikia mpaka kutamani siku moja nchi yetu itawaliwe kidikteta.
Mungu si Athumani akasikia kilio chetu akatuletea Jiwe tena Jiwe kwelikweli hacheki kabisa na kima yoyote, Wabongo tukaanza vilio na kusaga meno, tukampachika majina ya hovyohovyo lakini Mwamba alifunga macho na akaziba kabisa masikio yake.
Kelele zikaanza mpaka mjengoni za kummisi JK na kila sifa nzuri akapewa na walewale waliokua wanambeza, wanamkebehi na kumtukana.
Leo hii baada ya Mwamba kutangulia mbele za haki walewale waliokua wanambeza, wanamkebehi na kumtukana JPM ndio haohao wamekua wapiga zumari wa kumsifia na kumuona yeye ndie alikua haswa mkombozi wa hii nchi, wamegeukia upande wa pili kumtukana na kumsimanga Mama pamoja na viongozi waliopita wa awamu ya nne.
Mimi ninachosema Mama aendelee tu kuupiga mwingi asisikilize kelele za chura maana chura akiwa majini analalamika maji ni ya baridi sana halafu pia ni machafu yanamsababishia ngozi yake kushambuliwa na wadudu ndio maana mwili wake unapata mabaka mabaka,
Chura huyohuyo akiwa nchi kavu pia analalamika nchi kavu jua ni kali sana linamchoma mpaka ngozi yake inababuka na mwili wake wote unajaa mabaka mabaka.
 
Back
Top Bottom