Kwa kikosi hiki, Brazil wasipobeba Kombe la Dunia naachana na mpira na JamiiForums natoka kabisa

Kwa kikosi hiki, Brazil wasipobeba Kombe la Dunia naachana na mpira na JamiiForums natoka kabisa

Mmeshasahau kile kikosi cha Argentina au Ivory coast vya miaka iliyopita?

Je wale Mastaa wa France Walifanywa nn na Senegal?

Ujeruman hawanaga hzo mambo ya kutajana.
Ila hicho kikosi cha Brazil kitachapwa 5 bila na Ujerumani
 
Mkuu hapo inshu ni co-ordnation ya timu ikishindkana utawaona vimeo tu pia kumbuka mpira wa leo mbinu zina mata zaid
Kumbuka Greece walivyochukua euro
Pia coordination ya timu IPO Kwa Brazil
 
KIBOKO YAO FC

Goalkeepers: Alphonse Areola (PSG), Hugo Lloris (Spurs), Steve Mandanda (Marseille)

Defenders: Presnel Kimpembe (PSG), Laurent Koscielny (Arsenal), Djibril Sidibe (Monaco), Samuel Umtiti (Barcelona), Raphael Varane (Real Madrid), Christophe Jallet (Lyon), Lucas Digne (Barcelona), Layvin Kurzawa (PSG)

Midfielders: N'Golo Kante (Chelsea), Blaise Matuidi (Juventus), Paul Pogba (Manchester United), Adrien Rabiot (PSG), Corentin Tolisso (Bayern Munich), Thomas Lemar (Monaco)

Forwards: Olivier Giroud (Arsenal), Antoine Griezmann (Atletico Madrid), Alexandre Lacazette (Arsenal), Kylian Mbappe (Monaco), Florian Thauvin (Marseille), Nabil Fekir (Lyon), Kingsley Coman (Bayern Munich)

Coach: Didier Deschamps
Ongezea Osmoune Dembele (Barcelona)
 
Na hakibebi kikombe ...mark my words. Wameshajiexpose too much....atakuja mzee wa Mercedes Benz na VW atabeba....wazee wa kimya kimya ....sikujui hunijui...but cheza mbali kabisa na Mjerumani....ni mtendaji na hana kelele zenu.
Mkuu yule ameshajitia gundu na kikombe chake cha mabara world cup hana chake
 
Mashindano yakifanyikia Ulaya, Brazil sikumbuki lini walichukua ubingwa wa Dunia.......Labda 1958, michuano ikifanyikia Sweden! Mnikumbushe maana huu uzee nao......ni majanga!!
Mkuu hayo mambo ya kizamani achana nayo
 
Kuna tofauti kubwa ktk kutaja kikosi na kuchukua ubingwa. Football sio matako/ kwamba kila mtu anayo
 
Ukiangalia Asilimia 40 ya Magoli waliyofungwa Madrid La Liga yamepitia kwa Marcelo.
:
Real Madrid wana tatizo kubwa upande wa ulinzi wa kushoto ambapo ni jukumu la beki wa Kibrazil Marcelo Vieira.
Magoli ya Celta Vigo katika mchezo wa wikiendi iliyopita yote yalitokana na udhaifu wake upande wa kushoto anapopanda kushambulia na kushindwa kurudi nyuma kwa uharaka na kuzuia hatari zinazoelekezwa langoni.
Msimu huu pekee kwenye La Liga, Real Madrid wameruhusu magoli 16, magoli 6 sawa na asilimia 40 ya magoli hayo, yalipitia upande wa Marcelo.
 
watu mkivuta bangi... mna sizi na kuanza kuota ota mara upo mamtoni kumbe upo kwa mtogole... una toa kikosi leo wakati hata maligi hayajaisha... watu wanapambana kuonesha mauwezo ili wasikose kombe la dunia... wengine hawataki kuumia wana chagua mechi za kucheza wakina neymar...

akumbuke kulikuwa na dinho alileta ubisho na usuper star ambao ni mzigo wa mwiba na mwisho ukawa mbaya... wazungu sio watu wazuri ktk kazi, aubameyng anajionea hilo pale dotmund, kiburi sio maungwana...

beckham alivunjika mkuu kwenda ktk kombe la dunia 2002 kama sikosei, na kiwango hakikuwa kile alicho tarajiwa kukionesha... wakina owen walivunjika miguu, wakina rooney...

wengine walitemwa wakati walikuwa on fire ktk vilabu vyao... mpaka dunia ikashangaa...

leo mnakuja andika ushabiki usio na tija mapema hivi... eb vuteni subira, watanzania ninani aliye waloga?
 
Back
Top Bottom