GE2025 Kwa kinachoendelea mtaani, ni wazi Tundu Lissu/CHADEMA wana kazi kubwa ,No reforms No election it was wrong timing

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Chadema imekufaje? Huku majaji na mapolis wakitumika kukihujumu? Ile kesi ya lissu ukifuatilia mpaka unajisikia aibu, hakimu anazunguka zunguka tu
SUICIDE ni mbaya, ndyo maana hakuna judge hapo, sasa hivi mgnekuwa na slogan ya "FREE TAL" ingefaa zaidi, lakini NRNE imeshafeli, life goes on as usual, ila inawaumiza sana kisaikoligia, lkn taratibu you will come to reality
 
Huwezi kutumia Mbinu zile zile zilozo wafelisha miaka zaidi ya 20 utegemee matokeo mapya.

kwanza mpaka sasa NRNE imezaa matunda, Au hujaona chama cha majani mabichi kimeweka Hoja ya katiba mpya kwenye irani yao ya miaka mitano ijayo?

Unazani wanapenda, Ukweli ni kwamba presure imekua kubwa sana.
 

Kesi ambazo hazina mbele wala nyuma. Mwalimu Nyerere na wenzake, walikuwa wanabambakiwa wakiwa wanadai uhuru.
Na bado uhuru ulipatikana. Kimsingi, hakuna mtu anayeweza kuzuia matakwa ya nyakati. Ukitaka kuendelea kuendesha punda kama babu zetu wakati kuna motokaa, ni hiari yako.

Ila haina maana umeweza kuisimamisha dunia. Ni suala la muda tu, mabadiliko yatakuja.
 
usilinganishe harakati za JKN na changamoto za Mungu wenu TAL, hiyo ni divergence ambayo haitatuunganisha
 
Unabii wangu unaniambia mgombea urais na rais wa taifa hili ni mwanaume 2025 hili haliepukiki

Sijajuwa atAtoka chama gani ila ni mwanaume wawili ndio marais
 
Mtaa gani uliopita wewe? Acheni uongo jamani
 
Sasa washiriki uchaguzi wa hovyoo namna siwatakuwa hawana akili na mwakaa huu wangeshiriki CCM ingeshinda kwa 100%. Kwanini wapoteze muda pesa na kushinda hawatashinda.
kama chaguzi ni wa hovyo, ni vema msishiriki, na ni haki yenu ya kikatiba, ila muache kusumbua wengine na hizo verse zenu za NRNE
 
SUICIDE ni mbaya, ndyo maana hakuna judge hapo, sasa hivi mgnekuwa na slogan ya "FREE TAL" ingefaa zaidi, lakini NRNE imeshafeli, life goes on as usual, ila inawaumiza sana kisaikoligia, lkn taratibu you will come to reality
Hiyo dhana ya NRNE ni complex Sana mkuu, imagine uchaguzi unaotarajiwa kuwa na wapiga kura mil 37 wakajitokeza watu mil 10 hapo NRNE haijafanikiwa? Serikali imebanwa ndo maana inatumia vyombo vya Dola kudhibiti chadema
 
..uchaguzi bila chadema utakosa ushindani na utakuwa mufilis.
Hakuna chochote

Sema chadwma bil uchaguzi ndio inakua mufilisi

Chakandumuz ni chama kinachong’aa Kipindi cha uchaguzi tu

Na huwa kinabeba rejects wa ccm na kuwa nao briefly kabla ya hao rejects kurudi ccm teady for next wave yq election

Very poor strategy
 
kama chaguzi ni wa hovyo, ni vema msishiriki, na ni haki yenu ya kikatiba, ila muache kusumbua wengine na hizo verse zenu za NRNE
Sasa wasiposumbua wakati wa uchaguzi wasumbue lini tena?
 
hawajalazimishwa, ni bora wapumzike na kujiuguza mpaka 2030
 
Fanya utafiti mtaani kuhusu mwitikio wa wananchi kuhusu uchaguzi utajua
 
usilinganishe harakati za JKN na changamoto za Mungu wenu TAL, hiyo ni divergence ambayo haitatuunganisha

Kwani Nyerere na wenzake waliunda Taifa la watawala ma watawaliwa? Kwani Nyerere aliondoka madarakani ili wala rushwa waile nchi kwa upole?

mabadiliko yale sio yanayotakiwa sasa. Watanzania wanataka uongozi wenye kuwajibika kwao. Unaochukia dhuluma, wizi na ulaghai. Unaochukia wachache kujimilikisha mali za walio wengi kwa janja janja na gilba.

Hii sio personal vendetta...hii ni ajenda wazi ya kutaka sheria na namna ya kila mtanzania awajibike. Mabadiliko sio kitu cha watu wachache kupenda au kuchukia. Inapobidi, kwa huruma yake Mwenyezi Mungu, lazima yatakuja.

Hakuna chawa atakayeweza kuyazuia
 
Kwa Arusha chadema ingeshiriki uchaguzi huru, makonda ubunge angeusoma kwenye magazeti tu...
 
Fanya utafiti mtaani kuhusu mwitikio wa wananchi kuhusu uchaguzi utajua
Usijali

Hata mwaka 2020 mwitikio haukua mkubwa sana despite domo kuzunguka na helicopter tena akiwa a hero returning from abroad

2015 pia mwamko haukua as expected despite wamama kutandika khanga barabarani ili wakubwa Wapite
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…