Kwa kipato cha Tsh. 200,000/- kwa mwezi naweza kujenga nyumba?

Kwako inawezekana ni hela ndogo.
Ila kwa kuwekeza kwa miez 6 au mwaka ni hela inafanya kitu site.

Una mchoro?.
Kiwanja chako ni ngap kwa ngap?.
Unataka ujenge vyumba vya ukubwa gan?.

Kwa Kawaida chumba kidogo kabisa ni mita 3 kwa 3 (futi 10 kwa 10) na sebule ni mita 5 kwa mita 5 (futi 16 kwa 16)
Na choo ni mita 1 upana na urefu ni mita 2( futi 3 kwa futi 6).

Ww ni Single Mother. Sasa kwanza hebu anza kujua tofaut ya Mita na Futi ili Fund asikuzingue.

Pili , ndio ujue saiz ya nyumba yako unataka uwe na ukubwa gan.

Tatu chora kiraman chako na umuonyeshe Fund kuwa unataka hiki na hiki. Na kiwe wap na wapi.
Based na Vipimo vyako.

Na hapa ndio utajua tofali ngap utatumia kwenye msingi na kujengea.
Ramani naangalia kwenye mitandao mpaka sasa nimevutiwa na hizi,
Hakika itabidi nijifunze kati ya futi na mita sina nilijualo
 
Attachments

  • IMG-20260711-WA0007.jpg
    IMG-20260711-WA0007.jpg
    37.4 KB · Views: 19
  • IMG-20260711-WA0001.jpg
    IMG-20260711-WA0001.jpg
    47.8 KB · Views: 17
Penye nia pana njia
Hapa kuna watu wanakejeli lakini kiuhalisia Mungu ndio anajua walivyo

Kuna watu wengine wangemuunga hata hela za kuanzia
Imagine watu 100 wakachangia 10k kila mmoja
Ndugu yangu nimejifunza hii dunia sio kwa watu dhaifu, ni kupambana kila kona ili tufike malengo na tukiondoka tuache alama kua tulikuwepo.
Nawashukuru nyote mnaonitia moyo, hamjui tu ninavyofarijika.
 
Hakika hii dunia ni kupambana mpaka kieleweke.
Nakumbuka niliondoka nchini nikiwa na miaka 19 tu bila kujua naenda kuwa na maisha gani
Ila nilienda kupambana na kuwa na maisha yangu mwenyewe.
Usivunjike moyo hata siku moja
Ukianguka amka pangusa vumbi endelea
 
Salaam waungwana,

Mimi ni mwanamke mwenye mtoto mmoja kiu yangu kubwa ni kupata kijumba changu kidogo tustirike na mwanangu, naombeni mnitie moyo je kwa shilingi laki mbili kwa mwezi naweza kujenga chumba, sebule, jiko dogo na choo? kiwanja kipo tayari maeneo ya Mkuranga, hili jambo linaniwazisha hadi nakosa usingizi natamani sana nipate kwangu ila kila nikifurukuta kipato changu ndio hicho,

Mtoto bado mdogo hajaanza kusoma, natamani niwe nimekamilisha kabisa ndoto yangu ya kua na kwangu kabla sijaingia kwenye heka heka za kusomesha.

Nimelileta huku najua kuna mafundi na wenye uzoefu wa kujenga kwa kudunduliza,

Napokea maoni, mawazo.
Labda nyumba ya milele 😂😂😂 Natania ....

Muhimu uthubutu, kama nafsi yako imesema unaweza bas ninaamini utaikamilisha. Usisubiri pesa ijae, ukisave hata 30k nunua tofali jaza kwenye kiwanja.

Jipe moyo ukianza ndio kwenye ushindi wenyewe
 
Salaam waungwana,

Mimi ni mwanamke mwenye mtoto mmoja kiu yangu kubwa ni kupata kijumba changu kidogo tustirike na mwanangu, naombeni mnitie moyo je kwa shilingi laki mbili kwa mwezi naweza kujenga chumba, sebule, jiko dogo na choo? kiwanja kipo tayari maeneo ya Mkuranga, hili jambo linaniwazisha hadi nakosa usingizi natamani sana nipate kwangu ila kila nikifurukuta kipato changu ndio hicho,

Mtoto bado mdogo hajaanza kusoma, natamani niwe nimekamilisha kabisa ndoto yangu ya kua na kwangu kabla sijaingia kwenye heka heka za kusomesha.

Nimelileta huku najua kuna mafundi na wenye uzoefu wa kujenga kwa kudunduliza,

Napokea maoni, mawazo.
Bila kupakiana Mafuta,

LAKI MBILI HAIJENGI
 
Kujenga ni project usipokua makini unaweza kua addicted na ujenzi ila kwanza ongeza juhudi katika hizo alakati zako za kila siku kua mbunifu katika kutafuta fursa ili usimame kiuchumi uache kutegemea hiyo laki mbili kama kipato tu.
 
Hakika hii dunia ni kupambana mpaka kieleweke.
Nakumbuka niliondoka nchini nikiwa na miaka 19 tu bila kujua naenda kuwa na maisha gani
Ila nilienda kupambana na kuwa na maisha yangu mwenyewe.
Usivunjike moyo hata siku moja
Ukianguka amka pangusa vumbi endelea
Wewe mzee upo? Hujachaguliwa diwani wa Camden bado?
 
Unaweza kujenga nyumba kwa kipato hicho my dear mtu asikutishe, uzuri kiwanja tayari unacho na ujenzi wa Dar/Pwani hua hauna gharama ardhi tambarare mchanga hapo hapo site,
Fuata ushauri wa waliotangulia, ukikwama mahali niambie usiogope wanawake kusaidiana💪
Mtoto wetu hajambo? atakua anakimbia sasa hivi, mpe salamu.
xx
 
Shukrani sana dokta umenipa nguvu,
Mtoto hajambo alhamdulillah, anakimbia na anajitahidi kuongea siku hizi, maa shaa Allah
 
Hio 200k nipe nikuandalie drawings? Then tumia mbinu iliokusaidia kupata hio 200k uipate nyingine unipe nikuandalie mchanganuo wa vifaa na ufundi wa hio ramani yetu
Then ndo utafute hela ya kujengea😎
 
Salaam waungwana,

Mimi ni mwanamke mwenye mtoto mmoja kiu yangu kubwa ni kupata kijumba changu kidogo tustirike na mwanangu, naombeni mnitie moyo je kwa shilingi laki mbili kwa mwezi naweza kujenga chumba, sebule, jiko dogo na choo? kiwanja kipo tayari maeneo ya Mkuranga, hili jambo linaniwazisha hadi nakosa usingizi natamani sana nipate kwangu ila kila nikifurukuta kipato changu ndio hicho,

Mtoto bado mdogo hajaanza kusoma, natamani niwe nimekamilisha kabisa ndoto yangu ya kua na kwangu kabla sijaingia kwenye heka heka za kusomesha.

Nimelileta huku najua kuna mafundi na wenye uzoefu wa kujenga kwa kudunduliza,

Napokea maoni, mawazo.
Kama unachosema ni kweli.
Hiyo laki mbili kila ukiipata nunua tofali.

Zikifika tofali 1600 nitafute kwa ushauri

Usije ukajidanganya ku save hela. Ni afadhari usave tofali kuliko hela.
 
Back
Top Bottom