Kwa kipato cha Tsh. 200,000/- kwa mwezi naweza kujenga nyumba?

Kwa kipato cha Tsh. 200,000/- kwa mwezi naweza kujenga nyumba?

Ndio inabaki hiyo laki mbili
Kama una kipato ambacho kinabaki laki 2 kama extra, basi unaweza kujenga nyumba tu kubwa zaidi ya hiyo unayoiwaza. Mimi kila mwisho wa mwezi nikifunga hesabu nabakia na elfu 2 na mia 5 hadi elfu 10, lakini nimeweza kupanga tofali na kupata sehemu ya kulaza mgongo.

Hao wafanyakazi unaowaona wakienda kazini na wanalipwa mwisho wa mwezi, mishahara yao haijawahi kukutana hata mara moja; yaani hadi mshahara mwingine unakaribia, account inasoma 223.67. Lakini wameweza kupanga matofali na kupata sehemu ya kulaza mgongo, na pia wana magari.

Sembuse wewe, mwisho wa mwezi unafunga hesabu laki 2. Advantage nyingine ni kwamba, "wewe ni mwanamke, uchumi unao." Simaanishi kwamba uwe kama wale, hapana. Namaanisha kuna me atajiweka na utakua unaokota pia.
 
Nimefarijika sana kwa huu ushuhuda wako, shukran kwa kunitia moyo, Mwenyezi Mungu abariki kazi za mikono yetu,
Amiiin,
Nimeshaanza na tofali 200, kila mwezi nitakua nanunua hizo tofali.
 
Salaam waungwana,

Mimi ni mwanamke mwenye mtoto mmoja kiu yangu kubwa ni kupata kijumba changu kidogo tustirike na mwanangu, naombeni mnitie moyo je kwa shilingi laki mbili kwa mwezi naweza kujenga chumba, sebule, jiko dogo na choo? kiwanja kipo tayari maeneo ya Mkuranga, hili jambo linaniwazisha hadi nakosa usingizi natamani sana nipate kwangu ila kila nikifurukuta kipato changu ndio hicho,

Mtoto bado mdogo hajaanza kusoma, natamani niwe nimekamilisha kabisa ndoto yangu ya kua na kwangu kabla sijaingia kwenye heka heka za kusomesha.

Nimelileta huku najua kuna mafundi na wenye uzoefu wa kujenga kwa kudunduliza,

Napokea maoni, mawazo, ushauri.
Mtoto mzuri ukakae huko porini kwa sababu gani? Njoo inbox nikupe mjengo masaki.
 
Hiyo laki 2 ni kipato chote au pesa unayotaka uweke kwenye Ujenzi......nikijua haya nitakupa muongozo mzuri......Karibu kwenye group letu la ujenzi na ramani Bure kabisa utapata site plan na ushauri kuhusu ujenzi wa Nyumba yako

Wa.me//255789005562

Niambie niunge group la ujenzi
 
Hatua za kufata hapo ni mbilii kama sio 3

1.Tafuta fundi maiko unaemuamini rafiki ako,muite chora nae ramani ya nyumba yako jinsiunavyotaka ikae ionekane

2.Baada ya hapo Weka hizo laki 2 zako bila kuzigusa kwa muda wa mwaka m 1

3.Chukua hela uliopata kwa mwaka mmoja huo kisha mwite yule fundi wako,Jenga msingi wa chumba kimoja kile master utakachoanzia maisha.

4.Kusaanya tena zile laki 2 zako kwa mwaka mzima, kisha mwite tena yule fundi wako asimamishe chumba chako cha master.

5.Nyumba ya kujiegesha utakua umepata ila haina finishing,yani ni kama pagale au mfupa usio na nyama... hauna chooo hauna madirisha,nk

ili hii nyumba ikamilike kwa kipato chako uweze ingia uishi huku ukiendelea ijenga taratbu itakuchukua miaka mi 4 kuanzia sasa, na hiii ni kama utatumia LAKI 2 YOTE

lakini kama utatumia laki basi itakuchukua miaka 10 kuanzia sasa ukiwa serious kupata nyumba..yani iwe iwavyo miaka mi 5 kwenda mbele utahamia kwako kwa kipato hcho cha 200,000 kwa mwezi
 
miaka ya nyuma nilikuwa nafanya kwenye NGO fulani kati ya wateja wangu mmoja akasema nikikopa 80,000 sinaweza kujenga nyumba ya block? ikabidi nikubaliane naye lakini kiuhalisia ndani kwangu kuligoma.
baada ya miaka kumi nakutana naye ananyumba nne na alianzia na ule mkopo wa 80,000.
binafsi naamini kujenga ni kibali muda ukishafika utajenga tu.
 
Inawezekana kabisa.

Mkuranga Mchanga bei Rahisi.
Na sehem nying ni tambarare.

200k kwa mwaka ni 2.4 Mill.

Unajenga msing wa hiyo nyumba unayoitaka alaf unanyanyua kwanza Chumba 1 na kuezeka. Alaf mwaka wa 2. Ukamalizia sebule na jiko. Na mwaka wa tatu ukafanya finishing.

Jipe miaka 4 hapo . Na Inawezekana kabisa.
Kwamba Hali, havai, na matibabu je?
 
Back
Top Bottom