Kaka Logic gani unataka,
Mwenyekiti wa bodi ya ligi Mr.Mguto alisema wameita kikao cha dharula kujadili,bila shaka asingeweza kusema mchezo haupo bila maamuzi ya kikao sababu yeye sio mtu wa mwisho wa kimaamuzi.
Baada ya kikao wakajiridhisha kuwa kuna viaahiria vya uvunjifu wa Amani na mechi isogezwe mbele.
Kumbuka hapo Msimamizi wa mchezo pia alinukuliwa kuwa alilidhia Simba wafanye mazoezi,sasa kipi kilizuia Simba wasifanye mazoezi ni vurugu kutoka kwa walinzi wa Yanga,
Walikaidi agizo la Msimamizi wa mchezo mbele ya Polisi.
Sasa ulitaka bodi ya ligi ifanye nini kama taarifa waliyopokea kutoka kwa Afisa usalama wa mchezo ilianinisha matukio kadhaa
Nanukuu
“” Kwasababu Bodi ya Ligi ilipokea taarifa ya usalama kutoka kwa ofisa usalama wa mchezo ambayo imeainisha matukio kadhaa yaliyo ambatana na tukio la club ya Simba kishindwa kufanya mazoezi na kwamba baadhi ya matukio yanahitaji uchunguzi ambao hauwezi kukamilika kwa wakati,Bodi ya Ligi kupitia Kamati yake ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imeamua kuahirisha mchezo tajwa hapo juu””
Mwisho wa kunukuu.
Haya Hapo kweli unahitaji D ngapi kujua kwamba sababu ni Usalama?