Pre GE2025 Kwa kipigo hiki cha CHADEMA, Mbowe achia chama kwa Heche kubadili kabisa aina ya siasa ya kufanya hiyo yako haina matokeo tena na haiaminiki kwa umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Huu sio uchaguzi ni geresha ili Tanzania ionekane ina demokrasia.

Watu inasemwa wameuawa, wengine kuumizwa na kukamatwa katika hiki kinachoitwa uchaguzi. Maeneo mengi wagombea walienguliwa, mawakala kuzuiwa kusimamia uchaguzi kwa kunyimwa barua za utambulisho au kuondolewa vituoni, kura feki kupigwa nje ya vituo na kuingizwa katika majumuisho, polisi waziwazi kusaidia CCM hata pale wapinzani walipotaka kuzuia uhalifu wa kura kuungizwa kwa kuwakamata wapinzani na kuwageuzia kibao kuwa wanafanya fujo; haya yote yanafanya huu usiwe na hadhi ya kuitwa uchaguzi.

Kabla hata ya kura kupigwa tayari CCM ilikuwa haina wapinzani kwa asilimia sitini hivi kutokana na kuwaengua wapinzani sasa mtu anaposema CCM itashinda kwa kishindo wakati tayari wana ushindi wa mezani kwa asilimia sitini mimi namshangaa huyo mtu kama ana uwezo sawasawa wa kuanalyse mambo.

NB: mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kupiga kura majira ya saa tano hivi na eneo nililopiga kura kulikuwa na amani na hakukuwa na foleni sikukuta wapiga kura kwa wakati huo eneo lilikuwa na vituo Vinne na chumba nilichopigia kura hakukuwa na wakala wa upinzani.
Mbele ya mwenyezi Mungu nimetimiza wajibu wangu kwa kumchagua yule niliyeona anafaa
 
Mbowe hanunuliki, labda walimpa fidia kwa kumharibia vitegauchumi vyake kipindi cha Mwendazake.
 
Kwa kweli nakupongeza. Mimi mtazamo wangu ni kuwa huu uchaguzi ni "wake up call " kwa CCM. Ikiwa hata baada ya baadhi ya viongozi wa CDM na wanachama wake wa kawaida kuuawa, kupigwa, kufungwa n.k. lakini bado kuna watu wanajitokeza kuchukua form za kugombea kwa tiketi ya CDM lazima wajitafakari sana.

Amandla...
 
Sasa wewe si ndio utufumbue macho. Tueleze anakosea wapi badala ya kusema aondolewe tu. Huyu mchaga amefungwa, amenyang'anywa biashara zake lakini bado anapambana. Wewe umefanya nini zaidi yake?

Amandla...
Kwa hiyo anapambana kwa biashara au?
 
Acha ujinga we jamaa !

Mbowe hamiliki Dola Wala jeshi wala risasi!!

Hujasikia Kuna risasi za moto!!?
 
Ni kweli CCM inahitaji jino kwa jino jicho kwa jicho!
 
Utakuwa una shida ya "AFYA YA AKILI "
huelewi ulichoandika, nikikuita kwa ruhusa yako SHOGA ASALI ya INZI na ya P Diddy utachukia??

🤣😀🤣😀
 
Chadema haijapata kipigo bali demokrasia imebakwa. Nakubalia na wewe juu ya mabadiliko ya uongozi wa juu wa Chadema,Mbowe ni kiongozi mzuri tu na ameiongoza Chadema kwa weledi ila Mbowe ni mstaarabu mno na kwa aina ya siasa za sasa za kishenzi za CCM tunahitaji kiongozi ambaye atakuja na siasa za jino kwa kwa jino, hawa washenzi makaburu weusi CCM siyo wa kucheka nao tena kama kuuana bora tuuane kwani wao hawana hati miliki ya utawala wa nchi hii.
 
Ni sawa kabisa, ila akija nmwenye NJAA atanunulika kirahisi sana, Mbowe yeye hana bei,
 
Ni sawa kabisa, ila akija nmwenye NJAA atanunulika kirahisi sana, Mbowe yeye hana bei,
Hivi vichwa viwili Lissu na Heche labda watumie risasi lakini havinunuliki, mmoja awe Mwenyekiti na mwingine Katibu Mkuu.
 
Kabla haujashauri Mbowe kuachia, ungeshauri akabidhiwe Polisi na wasimamizi halafu ndiyo upime na kutoa ushauri wako.
 
Ww kwa akili yako(sijui kam unayo) unafikir ulikuwa uchaguzi wa haki. Wanaokosea kujaza form how come wawe ni wa upinzani tu.? Wewe unaongozwa na mahaba kwa ccm ila ukweli ni kuwa huu ulikuwa ni uchafuzi sio uchaguzi. Bila jeshi na kura feki mnajua mngeaibika.
 
Mbowe bado anahitajika Chadema kwa usalama na uhai wake. Mawakala wa CCM ndio wanataka Mbowe aondoke, asiondoke abaki hadi demokrasia itengemae nchini.
Alisikika punguani mmoja akisema...
 
Mjue kuna watu leo wanakula stone kule module sasa nyie legend za kuleta hao tunawapa kazi ya mwaka kesho kiti kirudi palepale na wao maslahi yao yanafanyiwa kaz the rest mnajisumbua
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…