Huu sio uchaguzi ni geresha ili Tanzania ionekane ina demokrasia.Uzuri wa Mbowe ni kuwa ana ruhusu mawazo mbadala. Lissu anasema wazi kuwa kuna maamuzi alikuwa haku alianza nayo na hamchukulii hatua. Juzi wakina Lema wametofautiana Arusha, akasema ndio demokrasia. Msigwa alitofautiana wazi wazi na wenzake kwenye suala la Ngorongoro na hakufukuzwa. Naamini baada ya uchaguzi watakaa wote na kutathmini matokeo na kupanga nini cha kufanya. Kwa kiasi kikubwa uchaguzi umeonyesha jinsi dhana ya uchaguzi wa haki ilivyokuwa bado ni ndoto.
Amandla...
Watu inasemwa wameuawa, wengine kuumizwa na kukamatwa katika hiki kinachoitwa uchaguzi. Maeneo mengi wagombea walienguliwa, mawakala kuzuiwa kusimamia uchaguzi kwa kunyimwa barua za utambulisho au kuondolewa vituoni, kura feki kupigwa nje ya vituo na kuingizwa katika majumuisho, polisi waziwazi kusaidia CCM hata pale wapinzani walipotaka kuzuia uhalifu wa kura kuungizwa kwa kuwakamata wapinzani na kuwageuzia kibao kuwa wanafanya fujo; haya yote yanafanya huu usiwe na hadhi ya kuitwa uchaguzi.
Kabla hata ya kura kupigwa tayari CCM ilikuwa haina wapinzani kwa asilimia sitini hivi kutokana na kuwaengua wapinzani sasa mtu anaposema CCM itashinda kwa kishindo wakati tayari wana ushindi wa mezani kwa asilimia sitini mimi namshangaa huyo mtu kama ana uwezo sawasawa wa kuanalyse mambo.
NB: mimi nimetimiza wajibu wangu kwa kupiga kura majira ya saa tano hivi na eneo nililopiga kura kulikuwa na amani na hakukuwa na foleni sikukuta wapiga kura kwa wakati huo eneo lilikuwa na vituo Vinne na chumba nilichopigia kura hakukuwa na wakala wa upinzani.
Mbele ya mwenyezi Mungu nimetimiza wajibu wangu kwa kumchagua yule niliyeona anafaa