Pre GE2025 Kwa kipigo hiki cha CHADEMA, Mbowe achia chama kwa Heche kubadili kabisa aina ya siasa ya kufanya hiyo yako haina matokeo tena na haiaminiki kwa umma

Pre GE2025 Kwa kipigo hiki cha CHADEMA, Mbowe achia chama kwa Heche kubadili kabisa aina ya siasa ya kufanya hiyo yako haina matokeo tena na haiaminiki kwa umma

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Shabiki ni wewe maana zaidi ya kulalama haujatoa mchango wowote wa maana. Swali ni hao wengine ni wakina nani wakati wote wako pamoja nae! Na hayo mawazo mbadala ni yapi?

Amandla...
Unataka mchango gani ?, jambo la kwanza ni kuondoka Mbowe aje mtu mwengine ambaye ataleta muelekeo mwengine na maamuzi mengine ili Chama kisimame tena , kwasasa hali ni mbaya mbona kila kitu kipo wazi
 
Tupe mfano wa hayo mawazo mapya.

Amandla...
Nikupe mimi tena , anatakiwa Mbowe kutoka watu wagombee nafasi ile tupime uelekeo mpya , kila mmoja kwa sera zake wajumbe watachagua kilicho bora sio Mbowe ambaye amesha ishiwa kwasasa
 
Unataka mchango gani ?, jambo la kwanza ni kuondoka Mbowe aje mtu mwengine ambaye ataleta muelekeo mwengine na maamuzi mengine ili Chama kisimame tena , kwasasa hali ni mbaya mbona kila kitu kipo wazi
Hujui hata unachotaka.

Amandla...
 
Nikupe mimi tena , anatakiwa Mbowe kutoka watu wagombee nafasi ile tupime uelekeo mpya , kila mmoja kwa sera zake wajumbe watachagua kilicho bora sio Mbowe ambaye amesha ishiwa kwasasa
Hujui unachotaka. Mbowe angekuwa ameishiwa kama unavyosema, wahasimu wake wasingekuwa wanashinda humu na jukwaani kutaka atoke madarakani.

Amandla...
 
Hujui unachotaka. Mbowe angekuwa ameishiwa kama unavyosema, wahasimu wake wasingekuwa wanashinda humu na jukwaani kutaka atoke madarakani.

Amandla...
Sio wahasimu hata watu ndani ya Chadema wanataka mabadiliko , chama kinamfia mikononi mwake hana tena mawazo ya maana kwasasa
 
Hawezi kukubali Bwana yule..ile ni kama Asset yake. Wanachadema fikirieni vizuri..ni kweli Mh anaweza onekana yuko imara dhidi ya watawala, ila tukumbuke pia madaraka matamu, kuwa nje ya mfumo wa madaraka kwa waliozoea ni madhara..heshima ktk hadhira inategemea cheo ktk utawala..mfano Zuberi leo hii hana mvuto sbb sio kiongozi mkuu wa chama ..alipokubali kukaa pembeni kupisha democrasia leo hii anasahaurika..pengine ndio mana Mh anaona bado ipo fursa kwake kuonekana zaidi..na hata chama kutokwenda vema hawez umia sana..hapo ndo maana kuna umuhimu kupata moto mpya
 
Tatizo la mbowe anadhani yeye ndiye mwenye akili ya kukiongoza chama, hawaamini kabisa wengine ndio maana Mchungaji Msigwa aliamua kuondoka.

Demokrasia lazima ianzie ndani ya Chama, haitaji utafiti mbowe kachokwa.
 
Kipigo gani?. Yani uchaguzi usimamiwe na mkwe wa mwenyekiti wa CCM halafu wewe unakuja na ngonjera zako.
 
Kwa ufupi,

Wanachadema wakati mnaendelea kuugulia maumivu haya ya kupoteza kila kitu lazima muanze kufikiria aina mpya ya siasa ya kufanya baada ya hii ya Mbowe kufeli kabisa.

Niwakati Sasa wa Heche na Lissu kuchukua njia mpya za kukipeleka chama hicho kwaajili ya 2025 vinginevyo kutakuwa na kilio na kusaga memo.

Mungu ibariki Tanzania,

Toronto-Canada
Kama haujapiga sungura huwezi anzisha mada kama hii.
Woke mind virus.
 
Mbowe bado anahitajika Chadema kwa usalama na uhai wake. Mawakala wa CCM ndio wanataka Mbowe aondoke, asiondoke abaki hadi demokrasia itengemae nchini.

Hivi wewe kwa akili yako unadhani kuwa Lisu na mbowe nani anayeuza chama na kukihujumu hasa linapokuja suala la Pesa.?

Mbowe alimletea Lowasa .
Lisu hakupenda .
Baadae Lisu akaonekana yupo sahihi.

Mbowe akaingia kwenye maridhiano bila kujua kuwa Makamu wa Rais ndiye anayesimamia masuala ya Muungano yaani masuala ya Tanzania . Yaani Dr. Samia ndiye aliyekua anaweka mikakati na kumshauri Rais JPM juu ya chaguzi zote . Lakini pia tumeona hata baada ya JPM kufa pamekuwa na mambo mabaya zaidi na yasiyo ya kizalendo na Udini unanyemelewa taifa kwa karibu sana .
Lisu hakupenda maridhiano yasiyo ya kisheria zaidi ya kutaka kupiga picha .

Mbowe anafanya mambo mengi lakini nyuma yake anatizama kwanza biashara zake ili zisife. Na zikifa anatumia mgongo wa chama kuzinusuru.

Ukiangalia juu juu unaweza ukaona mbowe anapoteza mali zake lakini ukweli ni kawamba anazirudisha kwa mkono wa chama . Matokeo yake Ruzuku ya chama haifanyi kazi tena ya kujenga chama bali kulinda mali za Mbowe .

Mbowe alipokea chama kilichokuwa limekua sana kutokana na wimbi kubwa la wanachama toka NCCR .
Tangu mwaka 1995 Watanzania waliikataa CCM. NCCR mageuzi ilikuwa kwa sababu ya wasomi kukataa kuongozwa na Mrema ambaye hakuwa na Elimu wala pesa.
Mbowe kinachompa nguvu ni pesa mbinu na maono.
Lisu ana maono na anajua siasa na sheria na ni msomi wa kiwango kizuri cha sheria .

Mbowe kamwe hataleta mabadiliko wala katiba mpya haitapatikana.
Bila Chama kuingia kwa Tundu Lisu Chadema kitapoteza kabisa nguvu maana wamekata tamaa na wanataka Demokrasia ifanyika kuanzia ndani ya chama .

Kubadilisha mtu pia utaondoa dhana ya Ukabila .
Hii ni doa kubwa sana kwa Chadema hakuna ubishi.

Mbowe aweke mazingira mazuri abaki kama mtu mwenye kura turufu ndani ya chama ili kukilea chama . Mbowe awe huru kufanya biashara zake anazotuambia kuwa zinahujumiwa kwa sababu za kisasa . Mbowe agombee ubunge wa Jimbo la Hai na kuwa mbunge. Mbowe kimsingi hata mikakati hata jimboni kwake anakwama sana . Sikutegemea jimbo la Hai kurudi CCM kwa namna yoyote ile kwa wilaya yenye wasomi na matajiri kama Hai.
Kukosa jimbo la Hai ni ufala naulofa mkubwa sana. Bilionea kama Mbowe kuibiwa kura ni usengenyaji mkubwa sana .
Yaani Mbunge Mbowe anashindwa kufika vituo vyote vya polisi na kuwawekea maOCD mafuta kwenye magari yao na wale wa kupira . Yaani anashindwa kukaa na wajumbe mpaka wale wa CCM na kuwapa mbege kama mtoto wao . Wakati wote amekua mbunge ni kulalamika tu badala ya kuwa karibu na wadao wa siasa .?
Bilionea na mbunge Mbowe alikua anashindwa kuwa karibu na walimu . !!

Hivi hakujifinza kwa Ndessamburo aliyekua anawapa pesa mpaka wale CHADEMA waliotaka kununuliwa akiwemo Lema .
Kifo cha Ndessamburo kikawa ni kifo cha chadema kanda ya kaskazini .
Mbowe waka hakukijenga chama kwa pesa zake kama Ndesamburo.
Ndesamburo hakuwahi kushindwa kwenye uchaguzi wote jimbo la moshi na hata Salimia akiwa makamu alijua ndio wakiishangilia kifo chake . Ndio maana walisema kifo ni kifo tu na wao wakitaka kumlenga mtu shabaha hawakosi.
R.I.P. Ndesa Pesa wa CHADEMA
R.I.P JPM wa CCM
 
Kipigo gani?. Yani uchaguzi usimamiwe na mkwe wa mwenyekiti wa CCM halafu wewe unakuja na ngonjera zako.

CCM ina intelijensia kali sana maana inatumia TIS na polisi.
Mbowe sio tishio kwa CCM kama tunavyodanganywa na Machawa wake.

Mbowe angekua tishio wangemuondoa mapema sana.
Mrema alikua tishio kwa CCM maana akiijua seikali na alikua hana mali . Duniani kote wanaharakati wasiojihusisha na biashara ni tishio sana kwa mafisadi.

Maalim seif alikua tishio kwa CCM 'z serikali yake .
Tundu Lisu alikua Tishio ndio maana wakampiga risasi .

Ndesa Mburo alikua tishio kwa sababu alikua na utajiri mkubwa sana usiopungua hata kwa dakika . Na alikua na uwezo wa kujenga mpaka miundombinu yoyote kwa pesa zake bila kutetereka . Ndiye mbunge pekee aliyegasa kompyuta kwenye shule za msingi zote jimboni kwake . Wakati huo compyuta hata tasisi nyeti za umma hawana .
Mbowe watuambie amefanya nini cha ajabu jimboni kwake ? Watu wa kule KIA hawana hata maji ya malambo . Tulitegemea kuona maendeleo nje ya Kule Machame ambapo wameendelea tangu mkoloni.

Mbowe apumzike tu maana ameshachoka kimikakati kwa miaka yote inatosha na atajijengea heshima kubwa sana na itamsaidia mtoto wake kuja kuishika Bavicha baadae na hata kuja tena kuwa mwenyekiti . Lakini kwa sasa anamchelewesha na kumzuia mtoto weke kuongoza chama bila kujua .
Kama anaakili ataniemewa . Tunampenda sana Mbowe ila akisubiri mpaka tumchoke na kumuona wa kawaida na wa kulalamika tu
 
Kwa ufupi,

Wanachadema wakati mnaendelea kuugulia maumivu haya ya kupoteza kila kitu lazima muanze kufikiria aina mpya ya siasa ya kufanya baada ya hii ya Mbowe kufeli kabisa.

Niwakati Sasa wa Heche na Lissu kuchukua njia mpya za kukipeleka chama hicho kwaajili ya 2025 vinginevyo kutakuwa na kilio na kusaga memo.

Mungu ibariki Tanzania,

Toronto-Canada
Wamepoteza kwa msaada mkubwa wa nguvu ya dola kwa zaid ya 100%
 
Unaweza sema hivyo sababu hukushiriki uchaguzi huu laiti ungeshiriki kwa kusimamia uchaguzi huu ungewapa heko wapinzani kua wana roho ya paka
 
Unaweza sema hivyo sababu hukushiriki uchaguzi huu laiti ungeshiriki kwa kusimamia uchaguzi huu ungewapa heko wapinzani kua wana roho ya paka

Ndio maana akasema inatakiwa aje kiongozi mwingine ili aendane na mbinu za wahuni .
Mbowe kwa umri wake analindwa mambo mawili .
Mali zake na
Uhai wake .

Bora waje watu wanaoendana na 80% ya wananchi wasio na cha kupoteza zaidi ya kudai haki na uhuru wao.
Hapa ni Lisu na Heche .

Lisu hawezi kuuza chama Labda Mbowe naye alikosa ahamie CCM kama msigwa ndio atakua amepunguza nguvu ya chama kwa muda .

Lakini Mbowe akikabidhi kijiti kwa haki na kukaa pembeni kwenye uchaguzi huru ndani ya chama chake hakika wananchi watakua na hamasa kubwa sana na kelele za ukabila na ufalme zitatoweka
 
Chadema wanifuate niwape mbinu wanayo fanya CCM kwenye uchaguzi inayo pelekea matokeo kuwa hivyo,,mkiendelea hivi hiv tutabaki hiv hiv..
 
Kwanini waondolewe ? kama mwenyekiti angekuwa imara haya usinge yaona nakwambia , kuna wakati watu walikuwa imara CCM wakawa hawana la kufanya, wakati ule Dr Getrude Buriani anapigwa chini na Lema pale Arusha unafikiri ilikuwa rahisi HAPANA uongozi kuanzia juu ulikuwa imara sana
Mkuu ulielewa ccm waliposema Aina kusema Mungu akipenda?
 
Hauna lolote wenye misimamo Kama kina Lisu mkawapiga risasi. Mwangosi mlimuuwa mbele ya dr slaa iringa alifanya nini na misimamo yake. Mnaleta siasa za kipuuzi tu.

Back
Top Bottom