Mbowe bado anahitajika Chadema kwa usalama na uhai wake. Mawakala wa CCM ndio wanataka Mbowe aondoke, asiondoke abaki hadi demokrasia itengemae nchini.
Hivi wewe kwa akili yako unadhani kuwa Lisu na mbowe nani anayeuza chama na kukihujumu hasa linapokuja suala la Pesa.?
Mbowe alimletea Lowasa .
Lisu hakupenda .
Baadae Lisu akaonekana yupo sahihi.
Mbowe akaingia kwenye maridhiano bila kujua kuwa Makamu wa Rais ndiye anayesimamia masuala ya Muungano yaani masuala ya Tanzania . Yaani Dr. Samia ndiye aliyekua anaweka mikakati na kumshauri Rais JPM juu ya chaguzi zote . Lakini pia tumeona hata baada ya JPM kufa pamekuwa na mambo mabaya zaidi na yasiyo ya kizalendo na Udini unanyemelewa taifa kwa karibu sana .
Lisu hakupenda maridhiano yasiyo ya kisheria zaidi ya kutaka kupiga picha .
Mbowe anafanya mambo mengi lakini nyuma yake anatizama kwanza biashara zake ili zisife. Na zikifa anatumia mgongo wa chama kuzinusuru.
Ukiangalia juu juu unaweza ukaona mbowe anapoteza mali zake lakini ukweli ni kawamba anazirudisha kwa mkono wa chama . Matokeo yake Ruzuku ya chama haifanyi kazi tena ya kujenga chama bali kulinda mali za Mbowe .
Mbowe alipokea chama kilichokuwa limekua sana kutokana na wimbi kubwa la wanachama toka NCCR .
Tangu mwaka 1995 Watanzania waliikataa CCM. NCCR mageuzi ilikuwa kwa sababu ya wasomi kukataa kuongozwa na Mrema ambaye hakuwa na Elimu wala pesa.
Mbowe kinachompa nguvu ni pesa mbinu na maono.
Lisu ana maono na anajua siasa na sheria na ni msomi wa kiwango kizuri cha sheria .
Mbowe kamwe hataleta mabadiliko wala katiba mpya haitapatikana.
Bila Chama kuingia kwa Tundu Lisu Chadema kitapoteza kabisa nguvu maana wamekata tamaa na wanataka Demokrasia ifanyika kuanzia ndani ya chama .
Kubadilisha mtu pia utaondoa dhana ya Ukabila .
Hii ni doa kubwa sana kwa Chadema hakuna ubishi.
Mbowe aweke mazingira mazuri abaki kama mtu mwenye kura turufu ndani ya chama ili kukilea chama . Mbowe awe huru kufanya biashara zake anazotuambia kuwa zinahujumiwa kwa sababu za kisasa . Mbowe agombee ubunge wa Jimbo la Hai na kuwa mbunge. Mbowe kimsingi hata mikakati hata jimboni kwake anakwama sana . Sikutegemea jimbo la Hai kurudi CCM kwa namna yoyote ile kwa wilaya yenye wasomi na matajiri kama Hai.
Kukosa jimbo la Hai ni ufala naulofa mkubwa sana. Bilionea kama Mbowe kuibiwa kura ni usengenyaji mkubwa sana .
Yaani Mbunge Mbowe anashindwa kufika vituo vyote vya polisi na kuwawekea maOCD mafuta kwenye magari yao na wale wa kupira . Yaani anashindwa kukaa na wajumbe mpaka wale wa CCM na kuwapa mbege kama mtoto wao . Wakati wote amekua mbunge ni kulalamika tu badala ya kuwa karibu na wadao wa siasa .?
Bilionea na mbunge Mbowe alikua anashindwa kuwa karibu na walimu . !!
Hivi hakujifinza kwa Ndessamburo aliyekua anawapa pesa mpaka wale CHADEMA waliotaka kununuliwa akiwemo Lema .
Kifo cha Ndessamburo kikawa ni kifo cha chadema kanda ya kaskazini .
Mbowe waka hakukijenga chama kwa pesa zake kama Ndesamburo.
Ndesamburo hakuwahi kushindwa kwenye uchaguzi wote jimbo la moshi na hata Salimia akiwa makamu alijua ndio wakiishangilia kifo chake . Ndio maana walisema kifo ni kifo tu na wao wakitaka kumlenga mtu shabaha hawakosi.
R.I.P. Ndesa Pesa wa CHADEMA
R.I.P JPM wa CCM