Kajibu hoja na maswali kuntu tunayokuuliza acha kujibu paragraph za watoto wasiojitambua wala kuijua historia ya Rwanda [emoji1206]
Katuambie kwa nini unamsifia Paul Kagame aliyeanzia mauaji tangu kambini kwenye RPF akiwauwa kina Freddy Rwigema.
Hivi tunavyoongea Pastor Bizimungu yuko kizuizini nyumbani huku akiwa kapofushwa macho.
Amemteka mpinzani wake almaarufu Hotel Rwanda,na kumleta Rwanda kutoka Dubai kinyemela na kumfungulia mashtaka ya uhaini.
Mama Ingabhire yeye aliamua tu kuanzisha chama cha upinzani lakini yuko jela mpaka saa hii.
Wanamuziki wakiimba kinyume na matakwa ya Kagame wanaishia kuuwawa,au kuswekwa jela.
Hakuna ulinganifu kati ya Rwanda [emoji1206] na Tanzania [emoji1241] kijiografia.
Kale ni kama mkoa mmoja wa Tanzania bara.
Anapora maliasili za Congo [emoji1078], usiku na mchana.
Askari wote wa Monusco akaunti zao ziko Rwanda [emoji1206].
Hata mabilionea wa Congo [emoji1078] akaunti zao ziko Kigali.
Baada ya Genocide mataifa ya ulaya EU [emoji1099],yanayoongea kiingereza na America [emoji631]., walimminia misaada lukuki ili kumpiku mfaransa na hatimae sasa wanamtumia kupora madini adimu ya Cobalt na dhahabu pamoja na Cotan.
Narudia tena
GENTAMYCINE...unapotea kwenye reli taratibu.
Mimi huwa nafurahia topic zako ila sio kwa hii ya kumsifia Kagame.