imhotep
JF-Expert Member
- Oct 13, 2012
- 55,997
- 88,219
Ndio maana alisema Matajiri wataishi kama Mashetani?R.I.P Magufuli ulitufumbua macho kuhusu utajiri wa taifa letu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Ndio maana alisema Matajiri wataishi kama Mashetani?R.I.P Magufuli ulitufumbua macho kuhusu utajiri wa taifa letu.
DP World Dubai ni mkoloni pacha mithili ya kampuni ya VOC (Verenigde Oostindische Compagnie) ya Uholanzi.
...
DP World ya Dubai na The Dutch East India Company VOC, Verenigde Oostindische Compagnie) agenda zao ni za kikoloni na mikataba yote inayoingiwa imo kwa minajili ya kuwakilisha watawala wa nchi zao ndogo kidiplomasia, kijeshi, kutwaa ardhi nchi za mbali na kuingia mikataba kama vile wao (kampuni) ni nchi hasahasa na nchi duni za dunia hii.
Hapana, hili hatuwezi liruhusu.Ifikie wakati tukubali tu Wazanzibari wameuza bandari zetu za Tanganyika kwa ndugu zao Waarabu. Full stop.
Amepatwa na msuto wa moyo...Paskali kuwa na msimamo ,hueleweki unataka nini.
wanasheria
Huwa sisomi magazeti ya huyo mkuu, kwa hiyo huwa mara nyingi sishiriki kwenye mada zake.Hongera kwa uchambuzi mzuri mkuu, wenye madaraka wanadharau sana raia ndio maana hawaogopi kuivunja katiba.
JokaKuu Nguruvi3 zitto junior Kalamu Mag3
Mimi ni mtu wa maslahi ya taifa mbelePascal tuanue kwanza mkataba wa TICTS wa Gati namba 8 Hadi 11pale bandarini Ilikuwaje
Unajaribu kufanya mambo yaonekane kuwa magumu sana kuliko yalivyo. Sielewi wewe unasimamia wapi hasa kuhusu swala hili.Katika sheria ambazo ni ngumu kueleweka hata kwa wanasheria wengi ni PUBLIC INTERNATIONAL LAW. Ubaya zaidi linapokuja suala zima la mikataba ya kimataifa ndiyo mambo yanazidi kuwa makubwa kwasababu kipengele ambacho kinahusika ni THE LAW OF TREATIES, kama umesoma sheria utafahamu kwamba hii ni mada ngumu na ndefu mno kama ilivyo THE LAW OF THE SEA.
Linapokuja suala zima la uwekezaji ndiyo mambo yanazidi kuwa magumu zaidi kwasababu mada ambazo zinahusika sana ni THE LAW OF TREATIES, INVESTMENT LAW, DISPUTE RESOLUTION. Unaweza kukuta mtu kasoma PhD ya sheria lakini hizi mada bado haziwezi. Ndiyo maana hata ukija hapa Tanzania wanasheria wanaofanya INTERNATIONAL COMMERCIAL ARBITRATION ni wachache mno.
Kuweza kuelewa vizuri ule mkataba inahitaji uwe zaidi ya mwanasheria. Inahitaji kwanza kabisa uifahamu vizuri PUBLIC INTERNATIONAL LAW, bila hivyo utaingia chaka. Tafasiri za vifungu vya sheria za kimataifa hasahasa mikataba (Treaties), ni tofauti kabisa na tafasiri ya kwenye mikataba ya kawaida (Contracts). Kuna mambo kadhaa wa kadhaa ambayo kifalsafa mwanasheria anahitaji kuyafahamu kabla ya kuanza kutafasiri vifungu vya mkataba kama ule wa DP World.
Sasa ndugu zetu wametafasiri wenyewe, sijui tafasiri zao wamezitoa wapi. Leo hii mambo yamelipuka vibaya mno. TLS wamekuja na tafasiri yao, AG yuko na tafasiri yake, SPEAKER yuko na tafasiri yake, BUSH-LAWYER MBARAWA naye yuko na tafasiri zake. Kiufupi ni vurugu mechi tupu. Nchi za wenzetu suala kama hili lingekuwa limefanyiwa mjadala mpana, huenda hata kupelekwa kwenye mahakama ya katiba uli kupatiwa ushauri. Huku wanazima mjadala kwa nguvu.
Binafsi waache wanasheria wajadili hoja ili tufahamu nani ameliingiza taifa chaka....
Hili nimelisemea vizuri hapa Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!Mkuu, ikikupendeza, nijibu kwa nini DPW haingii ubia na TPA, wakati tayari walikwisha kusaini MoU, au kujisajiri TIC kama makampuni mengine yanayowekeza Tanzania?
hakukuwa na figisu figisu nyingi hivi. Angekuwa ni mzungu, wala usingesikia kelele, lakini kwa vile ni Mwarabu, kelele zinazidi baadhi ya watu muflis wakifikiri ni ankali!!.Pascal tuanue kwanza mkataba wa TICTS wa Gati namba 8 Hadi 11pale bandarini Ilikuwaje
Hakuna hata sentimita 1 ya m4raba imeuzwa1.Ifikie wakati tukubali tu Wazanzibari wameuza bandari zetu za Tanganyika kwa ndugu zao Waarabu. Full stop.
Paskali wewe ni mwanachama mwaminifu wa TLS, na mimi nakuuliza "kwanini mkikaa kimya?"Wanabodi,
Nikiwa ni mwanachama wa TLS, nimeisoma taarifa ya TLS kuhusu issue ya Bandari na DPW, kiukweli kabisa TLS inastahili pongezi za dhati!, imefunga huu mjadala, ingekuwa mimi ni Mnyamwezi, Kinyamwezi hii inaitwa "funga kalomo", yaani funga mdomo!. Taarifa hii ya TLS ni funga kazi, na huu ndio uzalendo!, hongera sana TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Kama mwanachama mwaminifu wa TLS, kwa heshima ya chama changu cha wanasheria wa Tanganyika, naomba nisikosoe jambo lolote kwenye taarifa ya TLS, ila sio vibaya kuzungumzia baadhi ya hoja ambazo TLS haikuzigusia kabisa!.
Ni baada ya kuisoma taarifa ya TLS, ndipo nikagindua mtu mwandishi wa habari kwanza, halafu ukaingia kwenye sheria, unakuwa na jicho kali zaidi kuliko jicho la mwanasheria mwanasheria tuu ambaye sio mwanahabari!.
Jicho la Mwanasheria linaangazia vifungu vya katiba, sheria, taratibu na kanuni, jicho la mwanahabari linaangalia mtazamo wa jamii, Mwananchi wa kawaida, anaona nini, anataka nini, hivyo jicho la mwanahabari linaona kuliko jicho la mwanasheria.
Baada ya Bunge letu kuridhia, niliandika makala hii, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! humo niliainisha mapungufu ya IGA hiyo kisheria kwa jicho la kiuanahabari.
TLS katika taarifa yao, kuna maeneo mengi wamepita mule mule nilimopita mimi, ila lile kubwa kuliko, "The Capacity" to contract, TLS wamelikwepa na kuliweka kiporo kusubiria wawasiliane na Dubai.
TLS hawakuyaona yale niliyo yaona mimi!. Tanzania ni nchi, inakwenda kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi, yaani Tanzania na UAE, lakini signatories wa Tanzania ni nchi, halali signatories wa UAE ni kampuni ya DPW!, tena imesaini bila POA yoyote toka UAE!.
Kwa maneno mengine ni kampuni ya DPW imejigeuza ni nchi ya Dubai wakati ni kampuni binafsi!, sio nchi, Dubai sio nchi, nchi ni UAE!, nchi yetu haiwezi kuingia mkataba wa kimataifa wa kuwa ratified na Bunge letu kama an international Treaty wakati signatories ni kampuni na sio nchi na hakuna POA yoyote ya UAE kuruihusu DPW to transact an international Treaty on behalf of UAE!.
Nimeipongeza TLS kwa uzalendo kwenye hili, ila nikiri kuwa nimeshangazwa na umakini huu wa TLS katika hili la Bandari.
Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.
Mpaka leo ninapoandika hapa, Katiba yetu bado inacho kifungu batili hicho!, sheria zetu bado zina ubatili huo na TLS wako kimya!.
- Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kwanini TLS walikaa kimya?.
- Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mtikila, ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini TLS walikaa kimya na sheria batili hiyo mpaka sasa bado iko kwenye sheria zetu licha ya Mahakama Kuu kutangaza ni batili?.
- Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu baada ya kubwebwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likafanya mabadiliko ya katiba na kuichomeka hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini TLS walikaa kimya?!.
Nimalizie kwa pongezi tena, TLS kwa hili la Bandari, ila kuna makubwa kuliko hili la Bandari, TLS bado hamjachelewa!.
Mungu ibariki TLS
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Mambo ni magumu sana hata bila ya mimi kuyafanya magumu. Yangekuwa marahisi kama wewe unavyotaka kulazimisha hapa, basi huenda kila mtu ikiwemo wewe angekuwa ni mwanasheria wa sheria za mikataba na uwekezaji. YOU CAN TAKE THIS TO THE BANK!Unajaribu kufanya mambo yaonekane kuwa magumu sana kuliko yalivyo. Sielewi wewe unasimamia wapi hasa kuhusu swala hili.
Hizo sheria ngumu unazozungumzia zipo kwa manufaa ya nani kama haziwezi kueleweka na pande zinazohusika?