Kwa la Bandari, Pongezi TLS. Katiba yetu imenajisiwa. Bunge limetunga Sheria batili. Haki za Watanzania zimeporwa. Kwanini TLS wamenyamaza kimya?


Ukiusoma mkataba wa IGA, kwa umakini hata kama wewe siyo Mwanasheria, utagundua kuwa hoja yako iko sahihi.

KWAMBA:

Kwa mkataba wa IGA, ambao DPW inataka kuutumia Tanzania kuwekeza, tofauti na nchi zingine km UK wakisajiri kama DPW Southampton Gateway au DPW London Gateway, inajivika koti la Dubai, nchi yake. Na taarifa ni kwamba DPW ni mali ya Sultani wa Dubai na familia yake. Kwa msingi huo tunamkaribisha Tanzania atutawale kupitia moja ya njia kuu (Maji - bandari, Ardhi, na Anga) za kuingia nchini.

KARIBU Sultani na familia yako
 
mkuu walikaa kimya kwa sababu tayari walikuwa wamesha pewa ahadi Fulani fulani , Ila kilichowatoa shimoni hata hao TLS ni aibu . so wapichokifanya kwa Sasa ni at least kutoa aibu kiaina . Kama wametubu kwa kumaanisha pongezi kwao!!
 
wanasheria

Na wanasheria wasomi walio na uelewa mpana wa historia ya ubeberu na mikataba tata iliyowahi kufanywa baina ya mataifa beberu na nchi nyonge zisizo na uelewa wa Geopolitics na ukoloni yaliyofanya kwa njiaza hila na kilaghahi kupata makoloni kupitia vibaraka au viongozi / machifu waliodanganywa kuhusu wanachosaini ni mahusiano ya makubaliano rafiki kumbe ni kuuzwa moja kwa moja sovereignty ya nchi.
 
Hongera kwa uchambuzi mzuri mkuu, wenye madaraka wanadharau sana raia ndio maana hawaogopi kuivunja katiba.

JokaKuu Nguruvi3 zitto junior Kalamu Mag3
Huwa sisomi magazeti ya huyo mkuu, kwa hiyo huwa mara nyingi sishiriki kwenye mada zake.

Nimekwishasoma na kushiriki kwenye mjadala wa hayo yaliyojadiliwa na hao TLS.

Nimeheshimu sana mchango wao katika swala hili la Bandari.

Nashukuru kwa kunikaribisha huku.
 
Pascal tuanue kwanza mkataba wa TICTS wa Gati namba 8 Hadi 11pale bandarini Ilikuwaje
Mimi ni mtu wa maslahi ya taifa mbele
Kwenye hili la Bandari, msimamo wangu ni very open, kuna vitu sisi Watanzania hatuwezi, lazima tusaidiwe!. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?

Ila katika kusaidiwa lazima tusaidiwe kwa haki na wote tufaidike na sio kusaidiwa kwa janja janja, hili pia nimeliweka wazi Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!

P
 
Unajaribu kufanya mambo yaonekane kuwa magumu sana kuliko yalivyo. Sielewi wewe unasimamia wapi hasa kuhusu swala hili.

Hizo sheria ngumu unazozungumzia zipo kwa manufaa ya nani kama haziwezi kueleweka na pande zinazohusika?

Sasa sijui tufanyeje, maana kama hatuna uwezo wa kuzielewa hizi sheria, tukubali tu kuingia kichizi bila ya kujua jambo tunaloliingia?

Artificial Intelligence bado ni eneo changa sana, ambalo nalo hatujawa nalo uwezo na hatuwezi kusubiri tulitegemee hilo kwenye haya mambo unayosema wewe ni magumu sana kuyaelewa.

Uhitaji wetu ni sasa, kama kuna jambo tusiloweza kulielewa kwa kukosa uwezo nalo, na wala hatuwezi hata kuajiri wenye uwezo nalo toka nje, ina haja gani ya kujihusisha kwenye jambo lenyewe?

Kifupi ni kwamba, sikubaliani na maudhui ya hoja yako.
 
Pascal tuanue kwanza mkataba wa TICTS wa Gati namba 8 Hadi 11pale bandarini Ilikuwaje
hakukuwa na figisu figisu nyingi hivi. Angekuwa ni mzungu, wala usingesikia kelele, lakini kwa vile ni Mwarabu, kelele zinazidi baadhi ya watu muflis wakifikiri ni ankali!!.
P
 
Paskali wewe ni mwanachama mwaminifu wa TLS, na mimi nakuuliza "kwanini mkikaa kimya?"
 
Unajaribu kufanya mambo yaonekane kuwa magumu sana kuliko yalivyo. Sielewi wewe unasimamia wapi hasa kuhusu swala hili.

Hizo sheria ngumu unazozungumzia zipo kwa manufaa ya nani kama haziwezi kueleweka na pande zinazohusika?
Mambo ni magumu sana hata bila ya mimi kuyafanya magumu. Yangekuwa marahisi kama wewe unavyotaka kulazimisha hapa, basi huenda kila mtu ikiwemo wewe angekuwa ni mwanasheria wa sheria za mikataba na uwekezaji. YOU CAN TAKE THIS TO THE BANK!

Kifupi ni kwamba, sikubaliani na maudhui ya hoja yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…