MKANDAHARI
JF-Expert Member
- Apr 7, 2011
- 5,727
- 6,615
Kenge kweli kweliR.I.P Magufuli ulitufumbua macho kuhusu utajiri wa taifa letu.
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kenge kweli kweliR.I.P Magufuli ulitufumbua macho kuhusu utajiri wa taifa letu.
Yaani nilitaka nimpejibu kama hili, lakin nae nazan kunamna kaelewa ni aina ipi ya msimamo anaotakiwa awe nao.Paskali kuwa na msimamo ,hueleweki unataka nini.
Sijui kama kunamtu atakuelewa........ anyway una uhuru wa kuwa na maoni.Mimi ni mtu wa maslahi ya taifa mbele
Kwenye hili la Bandari, msimamo wangu ni very open, kuna vitu sisi Watanzania hatuwezi, lazima tusaidiwe!. Watanzania tujifunze kukubali kuna vitu hatuwezi, tunaposhindwa tukubali kusaidiwa au tukomae? Baada ya Bandari ni ATCL na SGR au Tusubirie?
Ila katika kusaidiwa lazima tusaidiwe kwa haki na wote tufaidike na sio kusaidiwa kwa janja janja, hili pia nimeliweka wazi Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee!
P
Tanzania nchi ya hovyo sana watawala hawaheshimu katiba ya Nchi hata kidogo ndo maana hawataki katukatu kusikia neno Katiba Mpya hasa ya maoni ya wananchi ya Warioba.Inakuwaje Bunge tukufu chini ya mwalimu wa sheria linatunga sheria batili??
Tatizo la bunge letu ni la kimfumo, tofauti na mabunge ya nchi kama Uingereza au Marekani ambayo yanafanya kazi ya 'kutunga' sheria, bunge letu 'linapitisha' sheria.
Kila kitu kinafanywa na serikali, sheria zote zinaandikwa na serikali na kupelekwa bungeni 'kupitishwa'.
Hata wakijaa ma profesa watupu, as long as mwenyekiti wa CCM anatarajia bunge 'lipitishe' sheria na maazimio ya kuisifu serikali kwa maslahi ya chama chao, basi madudu haya hayawezi kuisha.
Kwanza nakubaliana na wewe, sisi wananchi wa Tanzania pia tuna matatizo!,Kwenye hili hata sisi wananchi tuna matatizo kaka Paskali. Mfano mdogo, tu, ULIYOAMBIWA WAKATI UMEITWA BUNGENI HUJAWAHI KUYASEMA..!! Why?
Nani mwenye jukumu la kusema yaliyojili? Kulikuwa na any written iliyosema kwamba ukitoka huku, funga mdomo milele? Ikitokea mtu anakuhoji yaliyotokea kule ndani, utakataa kusema kisa aliyekuhoji kakaa kimya?Kwanza nakubaliana na wewe, sisi wananchi wa Tanzania pia tuna matatizo!,
Ile quasi judicial inquiry ya Bunge, proceedings zake are held in camera, hivyo kama aliyekuita kukuhoji, amenyamaza kimya bila kutoa matokeo, na wewe muhojiwa unanyamaza kimya, unafunga mdomo wako!.
P
The Kigoma Protocol on 5 August 1924 : Goods to and from the Belgian colonies in Central Africa could pass tax-free via the railway. The Belgian government entrusted the operation to a private company, the Belgian East African Agency, which later became the International Maritime Agency (AMI)...READ MORE: Source : Belbases - Une page oubliée du colonialisme Belge en Afrique
Naandikia Daily News, na Guardian kwa specific issues. Naandikia Raia Mwema na Jamhuri on critical issues. Naandikia Uhuru na Habari Leo positive features, na kila Jumapili naandikia Nipashe issues za maslahi ya taifa.Mr. Mayalla, makala zako huwa zinakuwa kwenye magazeti yapi maana magazeti mengi ya Tanzania contents zao hata hazivutii kabisa ukiacha THE CITIZEN, ukilinganisha na Magazeti ya Kenya kama DAILY NATION, THE STANDARD, FINANCIAL TIMES na mengine wapo very investigative na flow ya news zao zinavutia sana. Mfano wakati huu wa sakata la bandari huoni hili suala likipewa kipaumbele kwenye magazeti yetu ili kuongeza pressure kwa serikali.
Kaka paskalii mchumiaa tumboooKaka Paskali,
Nimeshangazwa na baadhi ya mitazamo yako kwenye hili andiko lako. Nina maswali haya ambayo naomba unipe majibu au ufanunuzi wake;
1. TLS ni nani? Rais wa TLS, wanachama wa TLS, au wote rais na mwanachama ndiyo TLS? Kama jibu TLS ni rais wa TLS, kwanini kwenye kujadili lolote lazima aite wanachama? Kama jibu ni Rais na wanachama, kwani hukuyasema hayo yaliyokaliwa kimya wakati wa mkutano?
2. Unasema wewe ni mwanachama wa TLS kwa vile ni mwanasheria, HAYA UNAYOSEMA TLS IMEKAA/ILIKAA KIMYA WAKATI YANATOKEA, HUONI KUWA UNAJISEMA MWENYE KWAMBA ULIKAA KIMYA?
3. Kama TLS wana uwezo wa kukosoa kama ilivyofanya kwenye hili la bandari, kwanini mngoje hadi wakosee ndo muamke kusema makosa? Kwani msiwe sehemu ya kinachokwenda kutokea?
Kaka Pascal Mayalla, mimi bado nasubiri majibu yako kwenye hoja hizi nilizokuuliza kwenye post hiyo hapo juu..!!Kaka Paskali,
Nimeshangazwa na baadhi ya mitazamo yako kwenye hili andiko lako. Nina maswali haya ambayo naomba unipe majibu au ufanunuzi wake;
1. TLS ni nani? Rais wa TLS, wanachama wa TLS, au wote rais na mwanachama ndiyo TLS? Kama jibu TLS ni rais wa TLS, kwanini kwenye kujadili lolote lazima aite wanachama? Kama jibu ni Rais na wanachama, kwani hukuyasema hayo yaliyokaliwa kimya wakati wa mkutano?
2. Unasema wewe ni mwanachama wa TLS kwa vile ni mwanasheria, HAYA UNAYOSEMA TLS IMEKAA/ILIKAA KIMYA WAKATI YANATOKEA, HUONI KUWA UNAJISEMA MWENYE KWAMBA ULIKAA KIMYA?
3. Kama TLS wana uwezo wa kukosoa kama ilivyofanya kwenye hili la bandari, kwanini mngoje hadi wakosee ndo muamke kusema makosa? Kwani msiwe sehemu ya kinachokwenda kutokea?
Ila tunawabunge wa hovyo sana..Wanabodi,
Nikiwa ni mwanachama wa TLS, nimeisoma taarifa ya TLS kuhusu issue ya Bandari na DPW, kiukweli kabisa TLS inastahili pongezi za dhati!, imefunga huu mjadala, ingekuwa mimi ni Mnyamwezi, Kinyamwezi hii inaitwa "funga kalomo", yaani funga mdomo!. Taarifa hii ya TLS ni funga kazi, na huu ndio uzalendo!, hongera sana TLS kwa kutanguliza mbele maslahi ya taifa.
Kama mwanachama mwaminifu wa TLS, kwa heshima ya chama changu cha wanasheria wa Tanganyika, naomba nisikosoe jambo lolote kwenye taarifa ya TLS, ila sio vibaya kuzungumzia baadhi ya hoja ambazo TLS haikuzigusia kabisa!.
Ni baada ya kuisoma taarifa ya TLS, ndipo nikagindua mtu mwandishi wa habari kwanza, halafu ukaingia kwenye sheria, unakuwa na jicho kali zaidi kuliko jicho la mwanasheria mwanasheria tuu ambaye sio mwanahabari!.
Jicho la Mwanasheria linaangazia vifungu vya katiba, sheria, taratibu na kanuni, jicho la mwanahabari linaangalia mtazamo wa jamii, Mwananchi wa kawaida, anaona nini, anataka nini, hivyo jicho la mwanahabari linaona kuliko jicho la mwanasheria.
Baada ya Bunge letu kuridhia, niliandika makala hii, Japo Bunge Limeridhia, DPW Kuendesha Bandari Zetu, ni Makubaliano Tu, Tukithibisha Kuna Matatizo, Tunarekebisha Mkataba wa HGA, Kazi Nzuri Iendelee! humo niliainisha mapungufu ya IGA hiyo kisheria kwa jicho la kiuanahabari.
TLS katika taarifa yao, kuna maeneo mengi wamepita mule mule nilimopita mimi, ila lile kubwa kuliko, "The Capacity" to contract, TLS wamelikwepa na kuliweka kiporo kusubiria wawasiliane na Dubai.
TLS hawakuyaona yale niliyo yaona mimi!. Tanzania ni nchi, inakwenda kuingia mkataba wa kimataifa wa nchi na nchi, yaani Tanzania na UAE, lakini signatories wa Tanzania ni nchi, halali signatories wa UAE ni kampuni ya DPW!, tena imesaini bila POA yoyote toka UAE!.
Kwa maneno mengine ni kampuni ya DPW imejigeuza ni nchi ya Dubai wakati ni kampuni binafsi!, sio nchi, Dubai sio nchi, nchi ni UAE!, nchi yetu haiwezi kuingia mkataba wa kimataifa wa kuwa ratified na Bunge letu kama an international Treaty wakati signatories ni kampuni na sio nchi na hakuna POA yoyote ya UAE kuruihusu DPW to transact an international Treaty on behalf of UAE!.
Nimeipongeza TLS kwa uzalendo kwenye hili, ila nikiri kuwa nimeshangazwa na umakini huu wa TLS katika hili la Bandari.
Sheria Kuu kuliko zote nchini kwetu ni katiba, katiba ndio sheria Mama, sheria nyingine yoyote inayokwenda kinyume cha katiba ni sheria batili!. Kinachoibatilisha hiyo sheria yoyote kinyume cha katiba, ni katiba yenyewe!.
Mpaka leo ninapoandika hapa, Katiba yetu bado inacho kifungu batili hicho!, sheria zetu bado zina ubatili huo na TLS wako kimya!.
- Serikali yetu ime draft sheria batili, inayokwenda kinyume cha katiba, ikaipeleka Bungeni kutungwa kuwa sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likaitunga hiyo sheria batili inayokwenda kinyume cha katiba, kwanini TLS walikaa kimya?.
- Rais wa JMT akaisaini hiyo sheria batili kuwa ni sheria!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mahakama Kuu kupitia kesi ya Mtikila, ikatamka sheria hiyo ni batili na kuitaka serikali iifute. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Ubatili wa sheria batili yoyote unabatilishwa na katiba, Mahakama Kuu ikiisha tamka sheria fulani ni batili kwa kwenda kinyume cha katiba, automatically sheria batili hiyo inakuwa imebatilika from there and then. Kazi ya serikali ni procedures tuu za kuifuta!. Kwanini TLS walikaa kimya na sheria batili hiyo mpaka sasa bado iko kwenye sheria zetu licha ya Mahakama Kuu kutangaza ni batili?.
- Serikali yetu ikakata rufaa kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, ikashidwa!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu baada ya kubwebwa, ikafanya kubwa kuliko, ikapeleka Bungeni mabadiliko ya katiba kwa hati ya dharura, batili ile ikachomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu!. Kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Bunge letu likafanya mabadiliko ya katiba na kuichomeka hiyo batili ndani ya katiba yetu!. Hivyo katiba yetu imenajisiwa kwa kuchomekewa ubatili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Mchungaji Mtikila hakukubali katiba yetu inajisiwe, akafungua shauri kupinga mabadiliko hayo ya katiba, Mahakama Kuu ikampa ushindi na kutangaza mabadiliko hayo ni batili!, kwanini TLS walikaa kimya?!.
- Serikali yetu ikakata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi huo wa Mahakama Kuu, serikali ikashinda, kwanini TLS walikaa kimya?!.
Nimalizie kwa pongezi tena, TLS kwa hili la Bandari, ila kuna makubwa kuliko hili la Bandari, TLS bado hamjachelewa!.
Mungu ibariki TLS
Mungu Ibariki Tanzania
Paskali
Rejea
1. Sheria ya Uchaguzi Ni Bad Law! Kuendelea Kuitumia ni Ujinga? Kuwabebesha Masikini Gharama za Uchaguzi ni Dhambi!
2. Shurti la kudhaminiwa na chama kugombea uchaguzi, ni shurti batili kwa mujibu wa Katiba, linatutia hasara, tulifute!.
3. Mgombea Kudhaminiwa na Chama ni Ubatili Uliochomekwa Kiubatili na Bunge Letu Ndani ya Katiba Yetu!. Tuache Ubatili Huu Uendelee Ndani ya Katiba Yetu?
Mkuu Ngalikihinja ,ni vile hujijui tuu, wewe kwangu ni zaidi ya Mwalimu wa sheria, maana pale UDSM, kwenye zile prerogative orders tulifundishwa nne tuu certiorari, mandamus, prohibition na habeas corpus, ni wewe ulionifundisha quo warranto, na procedendo, hivyo wewe kwangu ni zaidi ya Mwalimu!, sasa mwalimu anapomuuliza maswali Mwanafunzi, maswali magumu, mwanafunzi lazima ajitafakari sana!. Bado najitafakari ila nitakujibu mwalimu.Kaka Pascal Mayalla, mimi bado nasubiri majibu yako kwenye hoja hizi nilizokuuliza kwenye post hiyo hapo juu..!!