Kwa ma-atheist

Naamini hata wewe unaelewa Kiswahili....

Niliandika hivi..
Mbona nimekujibu na hujaendeleza hojaji lako kwenye swali hili?

Ni wapi nimesema vitu vipo hivi hivi tu?

Mwenzako kaandika kwamba kutokuwepo uthibitisho wa kuwepo mungu kunathibitisha kwamba mungu kapita uwezo wa binadamu, kutokuwepo uthibitisho wa kuwepo kwa mungu kunathibitishaje kuwepo kwake at all? Sembuse kuwepo kwa mungu aliyepita uelewa wa binadamu?

Kwa nini nilazima awepo "muanzilishi" na "muanzilishi" tu na si kingine chochote?

Hujajibu.
 
Nimekuwekea jibu la swali lako lakini hulioni....

Nikusaidie namna gani?
 
Nimekuwekea jibu la swali lako lakini hulioni....

Nikusaidie namna gani?
Hujaeleza ni kwa nini ni lazima kuwe na chanzo cha muanzilishi, na muanzilishi tu, si kingine chochote.
 
If you break a human being to the finest indivisible particles he becomes a wave ... an electromagnetic wave
 
Kitu kingine ni nini?

Maana yake nini?
Kitu kingine maana yake chochote tofauti.

Kwa nini chanzo kiwe "muanzilishi"/mungu na si kingine ambacho hata labda hatujapata kukijua?

Ukiongelea "muanzilishi" usha assume kwamba mi "mu-" , una denite nafsi, a conscious being.

Kwa nini una assume chanzo ni "muanzilishi" na si kwa mfano "kiqnzilishi" ambacho si mungu wala nafsi iliyo conscious ?
 
Wewe mbona ukiulizwa maswali ya maana unajificha ka mtoto wa kindergarten?
Umeshawahi kuulizwa je! Kila kilichopo lzm ukihakiki utakavyo wewe? Au kuna kuna vitu ambavyo vipo na wewe inavikubali lkn Ukiombwa ushahidi Huwezi Kuutoa?

Hebu jibu hapa km wewe ni dume lenye busara, ukikimbia ntakuita mke asie na busara.

Je! Unakubali kuwa Kifo kipo au hakipo?

Naomba jibu.
 
Wapi nimesema kila kilichopo ni lazima nikihakiki nitakavyo mimi?

Tuanzie hapo kwanza.

Toa ushahidi au rekebisha kauli yako kabla sijaendelea.

Ama sivyo utakuwa mzushi usiyefaa kujibiwa.
 
kwn Asili Ya Uhai n nn nyie wana sayansi....
Uumbaji wote umefanyika na Mungu kw kutamka na ikawa Zaburi 33:6-9. Mwanzo 1:3-23,
Maandiko yanaonyesha wazi kwmb Mungu ndiye Mwumbaji wa vyote. Yeye ndiye aliyeanzisha na ndiye anayetupatia uhai. isaya 40:25-28, isaya 45:18
 
Vyoyote vile,lakini ukishakubali kipo kianzilishi/muanzilishi ni hatua moja ya kuumaliza huu mjadala....
 
Kwa nini ukubali kitabu chenye maandiko yanayojipinga?
 
Vyoyote vile,lakini ukishakubali kipo kianzilishi/muanzilishi ni hatua moja ya kuumaliza huu mjadala....
Unajuaje kuna kianzilishi kabla ya kuchunguza na kuona hilo?

Mathalani, utajuaje kwamba kuna kianzilishi na si vianzilishi?

Unajuaje kwamba dhana nzima ya kianzilishi /kifuatishi si umasikini wa mawazo yetu tu uliotokana na nafasi yetu katika ulimwengu mpana sana na si ukweli wa msingi wala msingi wa ukweli?
 
Unajuaje kuna kianzilishi kabla ya kuchunguza na kuona hilo?
Kwa mujibu wa mntiki mimi nasema kuna kianzilishi/muanzilishi
Mathalani, utajuaje kwamba kuna kianzilishi na si vianzilishi?
Iwe itakavyokuwa,jibu ni kwamba kuna kilichosababisha au vilivyosababisha kila kitu kikawepo
 
Kwa mujibu wa mntiki mimi nasema kuna kianzilishi/muanzilishi

Iwe itakavyokuwa,jibu ni kwamba kuna kilichosababisha au vilivyosababisha kila kitu kikawepo
Ukishaongelea vilivyosababisha umeshaongelea zaidi ya kimoja.

Ukishaongelea zaidi ya kimoja tayari ushamtupa mungu wenu wa "primary mover" lama hayumkiniki.

Pia, hujanieleza unajuaje kwamba dhana nzima ya kianzilishi/ kifustishi haitokani na umasikini wa fikra tu unaoletwa na nafasi yetu katika ulimwengu, na wala si ukweli wa msingi, sembuse msingi wa ukweli.
 
Yaaas ni kweli kuna mengine we kiranga unayaamini lakin hujawahi kuthibitisha kuwepo kwake.kwa mfano hebu nipe ushahidi wewe una moyo na huo moyo unasukuma damu...yani siamini kabisa kama kiranga una moyo..nithibitishie hilo
 
Ukishaongelea vilivyosababisha umeshaongelea zaidi ya kimoja.

Ukishaongelea zaidi ya kimoja tayari ushamtupa mungu wenu wa "primary mover" lama hayumkiniki.
Wewe unamfahamu namna gani Mungu mpaka useme hawezi kuwa "vianzilishi"?
Pia, hujanieleza unajuaje kwamba dhana nzima ya kianzilishi/ kifustishi haitokani na umasikini wa fikra tu unaoletwa na nafasi yetu katika ulimwengu, na wala si ukweli wa msingi, sembuse msingi wa ukweli.
Utakuwa na tatizo ambalo huenda hujalijua bado....

Tazama post uliyoiquote kama hakuna jibu la suala hili....

Nashangaa unarudia kuuliza kitu abacho tayari nimeshakujibu.....
 
Wewe unamfahamu namna gani Mungu mpaka useme hawezi kuwa "vianzilishi"?

Utakuwa na tatizo ambalo huenda hujalijua bado....

Tazama post uliyoiquote kama hakuna jibu la suala hili....

Nashangaa unarudia kuuliza kitu abacho tayari nimeshakujibu.....
Do you believe in god the primary mover, yes or no?
 
kianzirishi n Muumba mbingu na dunia yaan Mungu... wakolosai 1:15-17
inasema... Naye n mfano wa Mungu asiyeonekana, mzaliw wa kwnz wa viumbe vyote. kw kuw ktk yy vitu vyote viliumbwa, vilivyo mbingun na vilivyo juu ya nchi, viavyoonekana na visivyoonekana; ikiw n vitu vya enz, au usultan, au enz, au mamlaka; vitu vyote viliumbw kw njia yake, na kw ajili yake. naye amekuwako kabla ya vitu vyote, na vitu vyote hushikana ktk yy.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…