Teknocrat
JF-Expert Member
- Oct 20, 2018
- 4,967
- 11,056
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.
Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.
Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.
Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.
Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.
Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.
Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.
Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.
Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.
Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki
Kwaheri Dar es Salaam,