Kwa machungu nasema 'Kwaheri mji wangu Dar es Salaam'

Nilikutana na Rafiki yangu wa A level mwanzoni mwa mwaka huu tulizungumza mengi, tukabadilishana namba za simu na kuwekeana ahadi ya kufanya reunion ila mpaka sasa hatujafanya hivyo.

Binadamu sio jiwe, hubadilika na mambo pia hubadilika, mtu huwezi kuishi na fikra zile zile kila siku.

Au kwamba wewe uende ulaya miaka 25 ukute tu watu wamekaa wanakusubiria wewe urudi wakufurahishe.

Una utoto mwingi sana grow up.
Kuna tofauti na nyinyi mliokulia mikoani na kuja mjini kwa masomo au kazi na kulowea
Na pia inafanana kama leo ukirudi mkoani kwenu nakukuta hakuna unayemjua
Mimi niliishi maisha yangu yote ya ujana sehemu moja tu niliyokulia, na baada ya hapo niliiondoaka
Kwa hiyo hiyo sehemu ni sehemu kubwa sana ya maisha yangu nilikuwa na marafiki na ndugu tuliokuwa tunaongelea maisha ya usoni kama utani na wengi walikuwa na ndoto ya kuondoka kwenda dunia nyingine kuanza maisha.
Unaonekana ni mzee wa makamo kwenye avatar yako lakini mgumu kuelewa hata maudhui ya ujumbe mdogo sana
 
Mkuu hata hapo Kendrick road by the time naondoka nilishaanza kuwa mgeni. Unaenda kwenye mikusanyiko ya kijamii unakuta asilimia 80 huwajui halafu wao wanajuana. Wale mliokuj a mwanzo wengi wameondoka kabisa au wamehama mji. Waliobaki wako busy na kazi na familia. Kwahio unachopitia ni hali ya kawaida kabisa.
 
Asante mkuu
Umenielewa vizuri sana
Kwa kweli hii ndio kuanza maisha mapya ya miaka ya kati.
Sijui ndio hivi wazungu wanaita midlife crisis 😀
Hahaaa kwa kiasi fulani Ila unachopitia kipo normal kabisa

Ni sawa na mimi nirudi mtaa nilioishi miaka 20 iliyopita ni lazma nikutane na replacement ya watu maana wa umri wangu wengi wameshaondoka na waliopo hawanijui.

Probably na wachache nitaokutana nao lazma mabadiliko yatakuwepo kwa sababu pengine nao pia wana watu wao wapya hivyo, lazma tuwe na common ground or interest ya kutufanya tubond tena. La sivyo, hakutoendelea mawasiliano
 
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Mimi sikumbuki jitu hata moja na wala simiss kitu...nasonga mbele

kwanza nikifika hapo Dar nakausha hata home sifiki..tatizo ukifika mizinga ya kutosha mpaka luku...
 
They say you never cross the same river twice.

Marafiki wenyewe ndio sisi tuko London, New York etc.

Kuna siku nilirudi Dar likizo nikawa nawatafuta marafiki. Nikapata experience kama yako. Vijiwe vimekufa. Watu wametapakaa dunia nzima. Vichochoro vyote tulivyokuwa tunakatiza vimejengewa kuta.

Abby Spartan hayupo, chimbo long time. Mani yuko South Carolina. Ngoto Spy hayupo, kazamia Vietnam. Baba Kiaro hayupo kashavuna maokoto ya Baba Ben na kukimbilia Nairo. Emma Jo hayupo yupo Chuga. Papii katembea mbele South. Mpaka Buddha Monk karuka Joburg. King Louis XIV katambaa . Tesha hayupo kajimix Mwanza. Pisholi yupo Dar lakini kapotea tu anasukuma mzigo.

Mzee wa Gala (RIP) kajenga tuta baada ya kupiga ukuta maskani kulinda Mercedes Benz yake. Ngati boy kajimix UK long time.

Nikamkuta Zico tu kabaki katikati ya wadosi anapepea flag bado.

Nimerudi kiwanja changu watoto wananishangaa wananiona mimi mgeni. Wakati nimetimba magulu hapo tangu Yoweri Museveni na Tito Okello (the real Museveni and Okello, sio majina ya maskani tu) wanagongea fegi maskani na kukimbia bill za madereva teksi wa Muhimbili.

Kwa sasa naona kama Dar imekuwa overpopulated.

Nimefikiria sana nikija naweza kukaa nje kabisa ya mji, Bagamoyo au Tanga.
Mhhh,na Kuna majumba yako katikatinhapo poa yako empty bila watu,alieuza ovyo viwanja masaki na oysterbay anatakiwa ajibu tuhuma za kuchafua ushuani
 
Kwakweli mm kila baada ya miezi mitatu lazima nilidi kijijini kwa wazazi wangu nilipo mzika mzee na babu zangu.Nayaandaa maisha ya kijijini kwakuwa karibu na wanakijiji nafahamu kama mungu ata niweka hai nikifikisha miaka 55 naamia kabisa kijijini vulugu za mjini nawaachia vijana. N.B akikisha unawekeza kwenu maisha ya mjini yanaitaji akili nyingi ukizeeka.
Theories za kiujana. Hatoki mtu Dar
 
washikaji niliokuwa nao wengi hata majina siwakumbuki, sasa sijui huo upweke utatoka wapi? Wewe mwenzetu kwani miaka yote hiyo nje huna marafiki huko nje au familia?mimi Dar nikiingia Nakunywa na yeyote ninayemkuta counter
Unatengeneza marafiki wapya kila siku mkuu. Bila ubaguzi.
 
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Masaki umesoma shule gani? Hebu jiupdate ndugu watu wa Dar tunakutana kitambaa cha cheupe na samaki samaki, ukitaka kulita yenu huku kuna Bogos huku Ngwasuna huku Twanga, huo upweke unakujaje?

Tafuta pesa hivyo vingine ni visingizio tu.
 
Kweli watu hatufanani, mimi marafiki zangu ni familia yangu akiwemo mwanaume wangu. Mpenzi wangu ndiye rafiki yangu mkubwa, na hata tukizeeka pamoja sina hofu ya upweke wala sitohitaji yeyote karibu yangu zaidi yake.

Nimeshangaa sana unaposema ukizeeka utarudi kwenye kibanda chako kuanza maisha ya upweke, kwanini unayaweka maisha yako ya furaha kwa watu wa nje badala ya wale wa nyumbani kwako?

Au pengine huna familia?
Kuna uwezekano huyu mjuba hana familia
 
Hivi mmesoma posti yangu ya kwanza na kuilewa?
Au mmekurupuka tu
 
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,

Ujinga
 
Urudi kufanya nini tena huko kigamboni uletee watu tabu tu.
Kuna swala ushawai kuulizwa kwamba miaka yote hiyo ughaibuni umerudi una nini?
Andaa majibu.
 
Ukiwa mtu wa ibada hasa muislamu, basi marafiki zako watakuwa unaofanya nao ibada msikitini na baada ya swala hasa muda wa jioni mnapata kahawa na kubadilishana mawazo.
Nan amekudanganya huko utapata aman na marafiki?,hakuna watu wanafiki kama waumini
 
Back
Top Bottom