Kwa machungu nasema 'Kwaheri mji wangu Dar es Salaam'

Kwa machungu nasema 'Kwaheri mji wangu Dar es Salaam'

Mkuu mimi sio kuludi tuu! Huwa najitahidi kuwatafuta ndugu jamaa na marafiki.. Wewe ulipoondoka umewa potezea mazima...
Hapana, mawasiliano yapo lakini hawaishi tena Dar es Salaama walishahama, na wengine ndio hivyo muda uliwatupa mkono.
Kuwa na mawasialiano sio tatizo, lakini unaporudi mji uliokulia na kukuta hakuna hata mmoja unayemjua na kwenda kumtembelea, ndio hali halisi.
 
Wengine sio wabeba box Ila tumekua kwa maisha ya kuhama hama hivyo, hatuna sehemu moja tunayoona kama ni home au marafiki tuliokua nao pamoja.

Unasoma shule nyingi na unafahamiana na wengi ambao hamna strong bond nao kiasi ile hali ya ugeni unaizoea.

Kwa hiyo, tunapoishi ndipo maisha yetu yalipo Ila kwa upande wako. nadhani zile memories za kuona sehemu uliyokulia inakuwa strange ndio inakutesa mkuu. Ila sidhani kama una la kufanya zaidi ya kukabiliana na hali
 
Pole sana mzee,. Maisha yanaumizaga ukiyafikiria sana.
Shukuru MUNGU ameendelea kukupa afya na sababu za kuendelea kupambana.,
Sometimes its good not to have answers of a few questions in life rather getting hurt after knowing the reality,.
 
Mleta mada utaeleweka zaidi na sisi wabeba box,kweli hua inauma kwenda mji uliokulia,halafu wale watu uliokua unawajua,wanakua hawapo tena,

Hua inauma sana hii,ila ndio maisha mkuu,tukubaliane tu na hali halisi ilivyo.
Bingwa
Umepigilia misumari kwenye maudhui ya ujumbe wangu
Na hii ndio hali halisi.
Lakini ukweli ni kwamba, Baba yangu mzazi aliyeishi maisha yake yote, aliweza kuendelea kuwa na maisha ya kuwa na marafiki zake wa kutembeleana mpaka uzee na muda wake ulipofika.
Labda sisi hivi vizazi vyetu ndio mfumo wa maisha mapya!
 
Wengine sio wabeba box Ila tumekua kwa maisha ya kuhama hama hivyo, hatuna sehemu moja tunayoona kama ni home au marafiki tuliokua nao pamoja.

Unasoma shule nyingi na unafahamiana na wengi ambao hamna strong bond nao kiasi ile hali ya ugeni unaizoea.

Kwa hiyo, tunapoishi ndipo maisha yetu yalipo Ila kwa upande wako. nadhani zile memories za kuona sehemu uliyokulia inakuwa strange ndio inakutesa mkuu. Ila sidhani kama una la kufanya zaidi ya kukabiliana na hali
Asante mkuu
Umenielewa vizuri sana
Kwa kweli hii ndio kuanza maisha mapya ya miaka ya kati.
Sijui ndio hivi wazungu wanaita midlife crisis 😀
 
Nimekuonea huruma..huna hata magroup ya watsup ya mliosoma nao? At least kidogo inasaidia kutokupotezana sana...au nyie ni wale wa kizazi za analojia...mpk chuo unafika hamjaianza digitali..
Huyu mtu ni mwongo, nitakubaliana na yeye labda tu kama ni mtunzi wa vitabu vya kiswahili au ni mwalimu wa kiswahili huko aliko.
 
Mkuu,

Siku hizi hata likizo naona uduanzi naishia Turks and Caicos.

Dar ukishuka airport tu unapokelewa kwa kuombwa rushwa kuingiza mizigo yako mwenyewe.
Huko Turks and Caicos kuna siku utachoka na utaona ni waste of time and money …each his own
 
Wote mmesema kweli. Kuna ukweli kwamba ukiwa na pesa hakuna upweke, marafiki watakutafuta hata ulio soma nao chekechea. N watakukumbusha hata ukiwasahau. Tafuta pesa na usiwe bahili.
 
Bingwa
Umepigilia misumari kwenye maudhui ya ujumbe wangu
Na hii ndio hali halisi.
Lakini ukweli ni kwamba, Baba yangu mzazi aliyeishi maisha yake yote, aliweza kuendelea kuwa na maisha ya kuwa na marafiki zake wa kutembeleana mpaka uzee na muda wake ulipofika.
Labda sisi hivi vizazi vyetu ndio mfumo wa maisha mapya!
Acheni kulialia sana maisha popote, mbona baba zetu walitoka vijijini walipokulia na kuhamia mjini kwa shule au kazi na wengine hawakuwahi kurudi, na nyie mliamua kuhamia nchi za watu kwa ajiri ya box au maisha tuu, ndio life ilivyo life goes on, friends comes and go, have fun
 
Kuna mtu aliniambia, upweke ni hali ya kujitakia. Alisema ukiwa busy huwezi kupata upweke. Lakini una kuwa busy ukifanya nini, apo ndio nikakwama.

Kila mtu anawaza alivyokua, na kuishi huko nyuma hadi alipo, ni life reflection, sasa sijui wasio pata upweke wao wana ishi bila ku reflect waliko toka au vipi, sifahamu.

Binafsi huwa natamani wale watu wangu niliokuwa nao tungeendelea kuwa karibu, lakini huwa haiwezekani, hata usinge hama Dar es salaam, bado mgepotezana tu.

Kama sio kazi, basi ukioa na kuanza familia priorities zinaanza kubadirika, unaacha au kupunguza hobbies na kuanza vitu vipya, au kutengeneza au kucha hobbies fulani fulani, in a process, unajikuta una marafiki wapya na maisha mapya, unaporudi kutafuta watu wako unakuta nao kama wewe wameshakuwa na aina tofauti ya maisha, na mnaanza kuonana tofauti na mwisho mnabaki kupigiana simu tu na tena za lazima sana.

Mwisho wa siku hamuonani, na inakuwa kama hivi sasa.
 
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Kweli watu hatufanani, mimi marafiki zangu ni familia yangu akiwemo mwanaume wangu. Mpenzi wangu ndiye rafiki yangu mkubwa, na hata tukizeeka pamoja sina hofu ya upweke wala sitohitaji yeyote karibu yangu zaidi yake.

Nimeshangaa sana unaposema ukizeeka utarudi kwenye kibanda chako kuanza maisha ya upweke, kwanini unayaweka maisha yako ya furaha kwa watu wa nje badala ya wale wa nyumbani kwako?

Au pengine huna familia?
 
Kuna mtu aliniambia, upweke ni hali ya kujitakia. Alisema ukiwa busy huwezi kupata upweke. Lakini una kuwa busy ukifanya nini, apo ndio nikakwama.

Kila mtu anawaza alivyokua, na kuishi huko nyuma hadi alipo, ni life reflection, sasa sijui wasio pata upweke wao wana ishi bila ku reflect waliko toka au vipi, sifahamu.

Binafsi huwa natamani wale watu wangu niliokuwa nao tungeendelea kuwa karibu, lakini huwa haiwezekani, hata usinge hama Dar es salaam, bado mgepotezana tu.

Kama sio kazi, basi ukioa na kuanza familia priorities zinaanza kubadirika, unaacha au kupunguza hobbies na kuanza vitu vipya, au kutengeneza au kucha hobbies fulani fulani, in a process, unajikuta una marafiki wapya na maisha mapya, unaporudi kutafuta watu wako unakuta nao kama wewe wameshakuwa na aina tofauti ya maisha, na mnaanza kuonana tofauti na mwisho mnabaki kupigiana simu tu na tena za lazima sana.

Mwisho wa siku hamuonani, na inakuwa kama hivi sasa.
Mtu kutoweza kuwa busy katika dunia hii ya leo ni ishara ya uvivu.

Na wala si suala la kuwa au kutokuwa na pesa.

Kama huna pesa, basi ni mvivu katika kutafuta pesa, kama una pesa, basi ni mvivu katika kutumia pesa.
 
Na weza kuto kukubaliana na wewe. Kuna watu sio wavivu kutafuta lakini kazi zao haziingizi kiasi cha wao kuweza kujitosheleza. Kuna wale wanaoingia mashimoni kule kwenye migodi, wana jituma sana, lakini hali zao duni kila siku, ila wale walio maofisini huko migodini, ndio wenye mafanikio. Kuna wavuvi kila siku wako baharini, sio wavivu kabisa, lakini hawana pesa.

Nadhani kuna bahati pia, kuna wengine walipata bahati walitengenezewa mazingira na wakaendeleza, na wana ishi vizuri, na kuna wengine hawana bahati na pesa hawana, ila sio wavivu.
 
Unaelewa nilichoandika?

Huyo mvuvi yuko busy kuvua ili apate pesa, atakosaje kuwa busy?

Anayeingia mashimoni kuchimba migodini kutafuta pesa atakosaje kuwa busy?
 
Nilikutana na Rafiki yangu wa A level mwanzoni mwa mwaka huu tulizungumza mengi, tukabadilishana namba za simu na kuwekeana ahadi ya kufanya reunion ila mpaka sasa hatujafanya hivyo.

Binadamu sio jiwe, hubadilika na mambo pia hubadilika, mtu huwezi kuishi na fikra zile zile kila siku.

Au kwamba wewe uende ulaya miaka 25 ukute tu watu wamekaa wanakusubiria wewe urudi wakufurahishe.

Una utoto mwingi sana grow up.
 
Nadhani hujasoma ukanielewa mada yangu
Nimeeleza ilikuwa kila nikipata nafasi kurudi kutembea, nakutana na marafiki tuliojuana miaka nenda rudi na mawasialiano yalikuwepo japo kipindi naondoka, ilikuwa kuwa na simu ni anasa, kwa hiyo siyo kila mmoja alikuwa na simu, baadae tukakutana huko mitandaoni enzi za graduate.com, na ikaja Facebook, mawasialiano yalizidi kuongezeka na ilikuwa kila nikirudi kutembea tunakutana.
Ninasema kadri muda unavyokwenda watu wamehama Dar es salaam, wako nina mawasiano nao wako mikoani Mwanzza, Arusha, na wengine nje ya nchi, kwa sababu hii ndio kwa sasa nikirudi, hakuna tena mtu wa kumtembelea au kuonana nao.
Hapo Tanesco nani yupo kwa sasa?, maana napajua hata kabla Pazi hawajahamia, na pia wakati Pazi wanacheza hapo, nnilikuwa napita sana kuwaona kina Patrick Nyembera, Papii, kina Mukolo na hata hivi karibuni nilikutana na jamaa yangu Atiki alikuwa Pazi na yeye sasa yuko Ulaya aliniambia alipita hapo na kukuta hakuna hata anaye mjua, kakuta vijana wadogo tu, lakini wakakumbuka,
Unataka kusema ni maveterani gani hao wa kikapu wa Pazi bado wako Tanesco?
Tanesco wapo tena generation hio hio ya akina Atiki. Huwa tunacheza jumatatu, jumatano na ijumaa saa mbili usiku. Siwezi kuwataja majina humu.
Halafu ulichoeleza ni kawaida watu wana move on. Kadri unavyokuwa marafiki wanapungua. Ukifika 70yrs ndio balaa unaowajua karibu wote washakufa wamebaki watoto na wajukuu kama unao na wao huwaoni wana maisha yao.
 
Back
Top Bottom