Kwa machungu nasema 'Kwaheri mji wangu Dar es Salaam'

Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Bora umeondoka yasije kukutokea kama yule bodaboda wa chanika aliye trend
 
Mkuu, kwa kweli ndio uhalisia wenyewe huu

Huu mji sio tena ule tuliokuwa tunaoujua, na sasa hata wale watu waliokuwa karibu yetu kama marafiki na ndugu pia wameshapotea na kupotea.
Nakumbua Oysterbay tulikuwa na Joseph Kabila(mwenyewe) kabisa mitaani alikuwa kijana mpole.
Nilienda mpaka Don Bosco, Vijana, kushangaa tu kujikumbusha.
Nilibahatika kukutana na Coach Evarist Mapunda mitaa, anafundisha new generation.
Mtaa wa Mindu umejaa maghorofa tupu, zile msajili almost zote walinunua na kuvunja.
Pale mbele ya Diamond Jubilee kile kiwanja walikokuwa wazungusha gari wadosi wa upanga, naona jeshi wamefungia uzio.
Halafu kutokana na mji kuwa overpopulated, maeneo mengi yaliyokuwa na public access wameyafunga.

Ndio hivyo, nimekubali nikirudi , ni kukaa huko mbali na mji na kuwa hobbyist wa kilimo binafsi kwa matumizi yangu.
na project ndogo ndogo za kuniweka busy.
Wewe ni wale mlivyoenda Ulaya/USA mlijidqi kukata mawasiliano sasa unarudi unataka uwone watu mtaani bila mawasiliano yao huwezi kuwapata. Watu wamesambaa dunia nzima hata waliopo au waliorudi wamesambaa Dar yote.
Kama ulikuwa mcheza kikapu njoo Tanesco opposite USA embassy old Drive in cinema. Utakuta ma veteran wazee wa chama tunacheza hapo. Hutakosa unaemjua kama ulikuwa unacheza kikapu enzi hizo.
 
Mk
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Mkuu,maisha ndivyo yalivyo,kubali kutengeneza marafiki wapya,Baadhi ya marafiki tuliokuwa nao utotoni pia wanatupotezea,so sio wa kuwafikiria sana
 
They say you never cross the same river twice.

Marafiki wenyewe ndio sisi tuko London, New York etc.

Kuna siku nilirudi Dar likizo nikawa nawatafuta marafiki. Nikapata experience kama yako. Vijiwe vimekufa. Watu wametapakaa dunia nzima. Vichochoro vyote tulivyokuwa tunakatiza vimejengewa kuta.

Abby Spartan hayupo, chimbo long time. Mani yuko South Carolina. Ngoto Spy hayupo, kazamia Vietnam. Baba Kiaro hayupo kashavuna maokoto ya Baba Ben na kukimbilia Nairo. Emma Jo hayupo yupo Chuga. Papii katembea mbele South. Mpaka Buddha Monk karuka Joburg. King Louis XIV katambaa . Tesha hayupo kajimix Mwanza. Pisholi yupo Dar lakini kapotea tu anasukuma mzigo.

Mzee wa Gala (RIP) kajenga tuta baada ya kupiga ukuta maskani kulinda Mercedes Benz yake. Ngati boy kajimix UK long time.

Nikamkuta Zico tu kabaki katikati ya wadosi anapepea flag bado.

Nimerudi kiwanja changu watoto wananishangaa wananiona mimi mgeni. Wakati nimetimba magulu hapo tangu Yoweri Museveni na Tito Okello (the real Museveni and Okello, sio majina ya maskani tu) wanagongea fegi maskani na kukimbia bill za madereva teksi wa Muhimbili.

Kwa sasa naona kama Dar imekuwa overpopulated.

Nimefikiria sana nikija naweza kukaa nje kabisa ya mji, Bagamoyo au Tanga.
Umaskini siki hizi umehamia mjini, Dar hovyo hovyo. We Kiranga pepeta upepo huko huko tu
 
Ukizeeka usirudi Kigamboni ,

Zeekea huko huko na marafiki wapya

Hata huko huko unaposema (I assume you mean US) ukizeeka hapakaliki, hata kama una hela unaweza kufa na upweke tuu, uncle wangu in his 60 kakaa US 30 years karudi kaishia kijijini alipozaliwa, nyumba za mjini hapo Dar kauza zote, yupo happy naamini na ndugu zake wanalima na kuchunga wanyama
 
Wewe ni wale mlivyoenda Ulaya/USA mlijidqi kukata mawasiliano sasa unarudi unataka uwone watu mtaani bila mawasiliano yao huwezi kuwapata. Watu wamesambaa dunia nzima hata waliopo au waliorudi wamesambaa Dar yote.
Kama ulikuwa mcheza kikapu njoo Tanesco opposite USA embassy old Drive in cinema. Utakuta ma veteran wazee wa chama tunacheza hapo. Hutakosa unaemjua kama ulikuwa unacheza kikapu enzi hizo.
Nadhani hujasoma ukanielewa mada yangu
Nimeeleza ilikuwa kila nikipata nafasi kurudi kutembea, nakutana na marafiki tuliojuana miaka nenda rudi na mawasialiano yalikuwepo japo kipindi naondoka, ilikuwa kuwa na simu ni anasa, kwa hiyo siyo kila mmoja alikuwa na simu, baadae tukakutana huko mitandaoni enzi za graduate.com, na ikaja Facebook, mawasialiano yalizidi kuongezeka na ilikuwa kila nikirudi kutembea tunakutana.
Ninasema kadri muda unavyokwenda watu wamehama Dar es salaam, wako nina mawasiano nao wako mikoani Mwanzza, Arusha, na wengine nje ya nchi, kwa sababu hii ndio kwa sasa nikirudi, hakuna tena mtu wa kumtembelea au kuonana nao.
Hapo Tanesco nani yupo kwa sasa?, maana napajua hata kabla Pazi hawajahamia, na pia wakati Pazi wanacheza hapo, nnilikuwa napita sana kuwaona kina Patrick Nyembera, Papii, kina Mukolo na hata hivi karibuni nilikutana na jamaa yangu Atiki alikuwa Pazi na yeye sasa yuko Ulaya aliniambia alipita hapo na kukuta hakuna hata anaye mjua, kakuta vijana wadogo tu, lakini wakakumbuka,
Unataka kusema ni maveterani gani hao wa kikapu wa Pazi bado wako Tanesco?
 
Ukizeeka usirudi Kigamboni ,

Zeekea huko huko na marafiki wapya
Aiseee!

Hakuna kitu mbaya kama mwafrika kuzeekea ulaya au Amerika.

Kwanza hakuna mwafrika yeyote aliyeishi ulaya au anayeishi ulaya anatamani azeeke ulaya.

Kwanza hata vibabu vya kizungu vikizeeka vinakimbilia Afrika kuja kusaka vipusa maana wanajua depression na loneliness itakayo wakumba.
 
Kama maudhui ya mada yangu inavyosema, nimeona nikubali hali ya sasa ya maisha yangu na jiji la Dar es salaam.

Kwa kukubali Dar es salaam sio tena ule mji au jiji niliwahi kuishi na kuwa na marafiki na ndugu. Baada ya kukulia, kusoma na kufanya kazi jijini Dar es salaam tangu nilivyozaliwa.

Niliweza kuishi na kusoma maeneo tofauti ya jiji, kuanzia Kurasini wilaya ya Temeke, Upanga wilaya ya Ilala, na Msasani, Oysterbay na Masaki wilaya ya Kinondoni.

Katika maisha yangu niliweza kuwa na marafiki kutoka mashuleni na wengine tuliojuana kutokana na maeneo niliyoshi.

Kwa sasa baada ya kuwa nje ya nchi kwa zaidi ya miaka 25, ilikuwa nikipata fursa ya kurudi na kutembea ilikuwa ikiwa ni furaha iliyoje kila nikirudi kutembea Dar es salaam nakukutana na ndugu na marafiki tuliosoma nao na kukua nao maeneo niliyowahi kuishi, na hali ilikuwa ikibadilika kwa kadri muda unavyoenda kila napo pata fursa kuja kutembelea nyumbani jijini Dare es salaam.

Kwa sasa hii hali ya mabadiliko ninayokutana nayo ni kutoweza kukutana na marafiki na ndugu kutokana aidha nao wao pia wahama jijini, au wameenda kutafuta maisha nje ya nchi na wengine wametangulia mbele yetu.

Hii imefikia mpaka sasa nikirudi, nakuwa sina sehemu ya kwenda kutembelea marafiki wala ndugu na kujikuta muda wote niko peke yangu au niko na familia yangu binafsi, na imekuwa mpaka watoto wangu wananiuliza kuwa baba uliiishi na kusoma huu mji, wako wapi marafiki zako uliosoma nao au uliocheza nao utotoni, kwa kweli nimekuwa sina jibu zaidi ya wote wamehamia nchi zingine au miji mingine ya mbali.

Kwa kweli na jiji limebadilika, kuna maeneo mabadiliko ni chanya yaliyoleta maendeleo kama Kigamboni na Mbweni ndio maeneo ya makazi mapya ya kisasa, na kuna maeneo yamebadilika kwa kuvurugika kama Upanga, Oysterbay na Masaki kwa kuharibika na kuanza kufanana na uswahili baadhi ya maeneo.

Kwa sasa nahitimisha jiji la Dar es Salaam sio tena lile jiji langu nililokulia, nililokuwa na marafiki kutoka kila tabaka la kimaisha kuanzia kuwa na marafiki kutoka familia zakishua niliokuwa nao maeneo ya Upanga, Oysterbay na Masaki ambao wote aidha wanaishi nje ya nchi au wametangulia mbele yetu na pia watoto wa familia za kimasikini niliosoma nao na kuwa marafiki wa kutembeleana na walikuwa wananishangaa badala ya kujichanganya na mabrazameni wa Oysterbay, mimi nilikuwa nakwenda kukaa nao maskani maeneo ya Temeke, Mtoni kwa Aziz Ali, Manzese Magomeni na Mwananyamala, leo hii hawa wote hawapo tena, wengi walieenda South Africa na wengine walifanikiwa mpaka kufika US na Italy, na wengine wametangulia mbele yetu, kwa hiyo hata haya maeneo yamekuwa mageni kwangu kwa sasa.

Natumai nikizeeka, nitarudi nyumbani kwenye kibanda changu nilichojitahidi kujenga huko Kigamboni na kuyaanza maisha ya upweke bila rafiki

Kwaheri Dar es Salaam,
Urafiki siku hizi uko mtandaoni, kama hivi,ukitaka urafiki wa kukutana na watu nenda bar au nyumba za ibada utapata, enjoy life with your blessed family blaza!!
 
Nimekuonea huruma..huna hata magroup ya watsup ya mliosoma nao? At least kidogo inasaidia kutokupotezana sana...au nyie ni wale wa kizazi za analojia...mpk chuo unafika hamjaianza digitali..
Asante, mkikua mtayaona
Na hasa mkianza maisha ya familia, maisha yako yanakuwa zaidi ndani ya familia yako.
Watoto wakikua, na kuwa hawana tena muda wakuwa karibu na wazazi ndio unaanza kuwaza marafiki zako wa zamani.
 
Mleta mada utaeleweka zaidi na sisi wabeba box,kweli hua inauma kwenda mji uliokulia,halafu wale watu uliokua unawajua,wanakua hawapo tena,

Hua inauma sana hii,ila ndio maisha mkuu,tukubaliane tu na hali halisi ilivyo.
 
Back
Top Bottom