Kwa machungu nasema 'Kwaheri mji wangu Dar es Salaam'

Bora umeondoka yasije kukutokea kama yule bodaboda wa chanika aliye trend
 
Wewe ni wale mlivyoenda Ulaya/USA mlijidqi kukata mawasiliano sasa unarudi unataka uwone watu mtaani bila mawasiliano yao huwezi kuwapata. Watu wamesambaa dunia nzima hata waliopo au waliorudi wamesambaa Dar yote.
Kama ulikuwa mcheza kikapu njoo Tanesco opposite USA embassy old Drive in cinema. Utakuta ma veteran wazee wa chama tunacheza hapo. Hutakosa unaemjua kama ulikuwa unacheza kikapu enzi hizo.
 
Mk
Mkuu,maisha ndivyo yalivyo,kubali kutengeneza marafiki wapya,Baadhi ya marafiki tuliokuwa nao utotoni pia wanatupotezea,so sio wa kuwafikiria sana
 
Umaskini siki hizi umehamia mjini, Dar hovyo hovyo. We Kiranga pepeta upepo huko huko tu
 
Ukizeeka usirudi Kigamboni ,

Zeekea huko huko na marafiki wapya
Umaskini siki hizi umehamia mjini, Dar hovyo hovyo. We Kiranga pepeta upepo huko huko tu
Hata huko huko unaposema (I assume you mean US) ukizeeka hapakaliki, hata kama una hela unaweza kufa na upweke tuu, uncle wangu in his 60 kakaa US 30 years karudi kaishia kijijini alipozaliwa, nyumba za mjini hapo Dar kauza zote, yupo happy naamini na ndugu zake wanalima na kuchunga wanyama
 
Nadhani hujasoma ukanielewa mada yangu
Nimeeleza ilikuwa kila nikipata nafasi kurudi kutembea, nakutana na marafiki tuliojuana miaka nenda rudi na mawasialiano yalikuwepo japo kipindi naondoka, ilikuwa kuwa na simu ni anasa, kwa hiyo siyo kila mmoja alikuwa na simu, baadae tukakutana huko mitandaoni enzi za graduate.com, na ikaja Facebook, mawasialiano yalizidi kuongezeka na ilikuwa kila nikirudi kutembea tunakutana.
Ninasema kadri muda unavyokwenda watu wamehama Dar es salaam, wako nina mawasiano nao wako mikoani Mwanzza, Arusha, na wengine nje ya nchi, kwa sababu hii ndio kwa sasa nikirudi, hakuna tena mtu wa kumtembelea au kuonana nao.
Hapo Tanesco nani yupo kwa sasa?, maana napajua hata kabla Pazi hawajahamia, na pia wakati Pazi wanacheza hapo, nnilikuwa napita sana kuwaona kina Patrick Nyembera, Papii, kina Mukolo na hata hivi karibuni nilikutana na jamaa yangu Atiki alikuwa Pazi na yeye sasa yuko Ulaya aliniambia alipita hapo na kukuta hakuna hata anaye mjua, kakuta vijana wadogo tu, lakini wakakumbuka,
Unataka kusema ni maveterani gani hao wa kikapu wa Pazi bado wako Tanesco?
 
Ukizeeka usirudi Kigamboni ,

Zeekea huko huko na marafiki wapya
Aiseee!

Hakuna kitu mbaya kama mwafrika kuzeekea ulaya au Amerika.

Kwanza hakuna mwafrika yeyote aliyeishi ulaya au anayeishi ulaya anatamani azeeke ulaya.

Kwanza hata vibabu vya kizungu vikizeeka vinakimbilia Afrika kuja kusaka vipusa maana wanajua depression na loneliness itakayo wakumba.
 
Urafiki siku hizi uko mtandaoni, kama hivi,ukitaka urafiki wa kukutana na watu nenda bar au nyumba za ibada utapata, enjoy life with your blessed family blaza!!
 
Nimekuonea huruma..huna hata magroup ya watsup ya mliosoma nao? At least kidogo inasaidia kutokupotezana sana...au nyie ni wale wa kizazi za analojia...mpk chuo unafika hamjaianza digitali..
Asante, mkikua mtayaona
Na hasa mkianza maisha ya familia, maisha yako yanakuwa zaidi ndani ya familia yako.
Watoto wakikua, na kuwa hawana tena muda wakuwa karibu na wazazi ndio unaanza kuwaza marafiki zako wa zamani.
 
Mleta mada utaeleweka zaidi na sisi wabeba box,kweli hua inauma kwenda mji uliokulia,halafu wale watu uliokua unawajua,wanakua hawapo tena,

Hua inauma sana hii,ila ndio maisha mkuu,tukubaliane tu na hali halisi ilivyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…