Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwahiyo dereva aliendelea na uyo mke au alimwacha!?
 
Mauza uza yapo kuna mwaka nilitoka South Africa na fortuner old model ndio zinatoka nikapita Mozambique kuna sehemu kuna pori kubwa nikawaona watu wawili wamevaa mashuka hawajavaa viatu usiku kama saa sita hivi ukiwapita unakuja kuwaona mbele tena wako upande ule ule nilipokaribia tete nikasimama mara akaja jamaa na D4D akasimama akaniuliza kuna vitu umeviona bara barani maana mimi nilidhani nina usingizi naota nikamwambia ndio alikua Kaburu nikamshauri atafute hotel alale maana aliingiza woga tayari nikaendelea na safari huko mbele sikukutana nao tena na sijapita tena ile bara bara..
 
Usichokiona au usichokiweza katu usimalize kusema hakuna kitu cha namna hiyo. Kuwa na akiba ya maneno, nyie yakiwakuta ndio huwa mnakuwa ma deadliest witnessess
 
Japo si dereva, lakini nakumbuka wakat tuko moshi dereva amekabidhi gari kwa baba mbele ya gari imepondeka kabisa baba akauliza kulikoni akawaambia et kagonga kuku aliniacha njia panda wallah
 
Ndio nilikua naenda shule lakini maswali mengi jioni ndio nikarudi kuuliza baba alinijibu njiani usiku hua kuna mauza uza pengine kakutana nayo nikaacha ile mada hapo hapo leo baada ya kusoma hapa nimeelewa sasa
Ni hatari tupu ila huwezi acha kusafiri kwa kuogopa mauza uza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
kumbe ulinusurika mhenga mwenzangu.
 
Ni hatari tupu ila huwezi acha kusafiri kwa kuogopa mauza uza

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni safari moja tu ndio nimewah kufika home late saa saba halaf home sikusema kama nakuja na niko hivo hua wananishtukia tu nipo, lakini sijawah kukumbwa na hiyo kadhia tena napenda sana kufika home usiku sema sio wa manane

Kuna siku pia tulienda shamba la moja la mkonge liko mnazi, ni mbali tulikua kama watu wanne nikiwa mwanamke alone kwenye ule msafara, wakat tunarud dereva akasema tuchanje mbuga kwa mbuga tusipite ya lami tutazunguka sana tulipokua mbugan gari sjui ilikanyaga nn ikaserereka karib iingie kwenye kidaraja tukashuka hatukuona chochote tukaendelea kuja tokea sehem kunaitwa maramba tayar usiku saa mbili hivi, tukatembea hapo hakuna alieku na waswas kuhusu nn tulikanyaga kufika eneo linaitwa gombero alitoka nyoka upande wa dereva anavuka dereva akamkanyaga tena nikapiga kelele nyoka ikabidi tuangalie hatukuona kama amekanyagwa sikua na waswas kabisa leo ninesoma hapa nimerecall hayo matukio maybe yawezekana n hayo mauza uza au ilikua kweli
 
Binadamu bhana, Sasa kwa vile hujaona ndo unapinga?
Kama hujawahi kutana na hayo mauza uza si kigezo cha kusema hayapo.
Kimya pia ni akili unaweza ukaambulia hata moja

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mauza uza ni nini hayo? nataka siku nikutane nayo nimeendesha sana night kali na napenda sababu ya speed so nipite njia gani nikutane hata na jini, nije kusimulia masela.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…