Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

[emoji2] [emoji2] [emoji2] wakija wavuvi na stori zao wanayoyaona baharini usiku,, nyinyi mtajihisi mnaona midoli tu barabarani. kote nime experience najua udereva mpaka uvuvi,, maana kwetu ni karibu na bahari tangu nina miaka kumi na tatu nilikua navua samaki baharini,, nikaanza kwenda na usiku pia na makarabai,, tunayoyaona huko baharini usiku,, nafkiri barabarani tunaona tom n jery[emoji2] tu

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji23] [emoji23] [emoji23]

Sent from my VKY-L29 using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu USIKU ni kwa ajili ya VISIVYOONEKANA KWA MACHO,,,unapaswa utulie,,sio muda wa kurandaranda

Sent using Jamii Forums mobile app
True kuna watu walikuwa wakivua Samaki usiku SAA saba mtoni,kwa mbali wakaona gari pickup inakuja spidi juu ya MAJI imeshona mzigo hasa hadi nyuma imebonyea juu kakaa mwanamke wa kizungu anavuta sigara ilipowafikia ikasimama gari yule mwanamke akawaambia Jamaa, INA maana nyie mchana hauwatoshi hadi mtuingilie usiku, napeleka mzigo nikirudi nisiwakute hapa,kisha gari ikaendelea na safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nakumbuka mwaka 2008,nirikuwa natokea Newala,kwenda Mtwara,kupitia njia ya Nanyamba/mahuta,
Kwenye gari tulikuwa watatu,dereva ni mwenyeji wa huko Kusini,Mtwara,kwenye gari Mimi nirikaa mbele,kama SAA sita usiku,gari ikiwa spidi,ghafla Mimi nikaona mwanamke aliyevaa mavazi meupe ameingia barabarani ghafla,nikashituka nikamwambia dereva kuwa makini utamgonga huyo mwanamke,dereva hakushituka,yule mwanamke akawa kama kayeyuka vile,gari ikapita,
Nikamuuliza dereva kulikoni,akaniambia turia kwanza nitakuambia tukifika mjini.
Mbele kidogo gari ikazima ghafla,tukashuka tukaisukuma iwake,ikashindikana,maeneo hayo tukawa tunasikia sauti ya simba,likatupita basi,tukalisimamisha kuomba msaada,wakatuambia maeneo hayo ni hatari sana,ni bora tuondoke tu,
Tuliangaika na gari yetu mpaka kunakucha,gari ilikuja kuwaka alfajiri SAA 12 na nusu,tukaendelea na safari mpaka Mtwara,.
Dereva akatuambia yule hakuwa MTU,na tungemkwepa,tungepata ajari,sitasahau hiyo siku.

Sent using Jamii Forums mobile app
Siku ingine ikigoma kuwaka inatakiwa dereva avue nguo zote abakie uchi linawaka anapiga gia hadi mkitoka maeneo hayo anavaa nguo kuendelea na safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwaka juz Nimekula shavu la kupeleka it border lusumo gali aina ya Subaru imprezza basi kama Kawa kwa kuwa gali lenyewe lilikuwa la race lilinikosesha hela lilikuwa linachukua watu wawili tu asiliamia kubwa ndani lilikuwa na mabomba ambayo yamefungwa gali zima endapo likipinduka lisiumie... Basi nimetoka yard kurasini break Rombo nikapata kichwa cha kwenda tinde njia panda kahama mwanza... Basi piga gia piga gia gali lilikuwa linakimbia sana... Kuna sehemu ukitoka dodoma mbele kuna kijiji kinaitwa saka mahela basi eneo hilo niko kibati mbaya tunapiga story mishale ya 9 kwenda 10 Ghafla abiria akaniambia watu hao kuja kutaamaki kundi la watu liko mbele basi nilipita katikati no watu no nini.... Abiria alishangaa sana nikamwambia hiyo ni michezo ya usiku Road

Sent using Jamii Forums mobile app
Gari sio gali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwani nani mkuu amekwambia alishuka kweny gari?
Mtoa mada amesema ivi "Badala ya kujibu akabaki ametukazia macho jamaa yangu akanishika mkono na kunivuta tukaondoka. Lakini mpaka sasa hivi tumebaki na maswali vichwani mwetu. "
 
True kuna watu walikuwa wakivua Samaki usiku SAA saba mtoni,kwa mbali wakaona gari pickup inakuja spidi juu ya MAJI imeshona mzigo hasa hadi nyuma imebonyea juu kakaa mwanamke wa kizungu anavuta sigara ilipowafikia ikasimama gari yule mwanamke akawaambia Jamaa, INA maana nyie mchana hauwatoshi hadi mtuingilie usiku, napeleka mzigo nikirudi nisiwakute hapa,kisha gari ikaendelea na safari.

Sent using Jamii Forums mobile app
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] hi chai hii hebu leta maandazi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ilikuwa no way out MKUU,, maana tayari nilikuwa KATI KATI ya BARABARA,,, mbele yangu magari mawili yamenitokea,,hata kama ningeenda pembeni nisingewahi,,,,ikabidi nikanyage mafuta,,,lakini kwny nafsi yang nilijiona ni kama ndy mwisho wa maisha yngu,, sikuamini kama ningeweza kupita pale kati kati ya zile Lori,,ilikuwa NO WAY OUT,,,,,kwnz nimemulikwa mataa usoni,,mbele KMO sioni vizuri,,akili yng ilidhani pengine mmoja wa DEREVA wa lori ndy angenikwepa Mimi,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
ulitisha sana mwamba,,ungeenda pemben ndo ingekuwa mwisho wako,,ila Mungu pia aliingilia kati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku nilikua natembea njiani Muda wa saa sita hivi
Nilikua navuka uwanja kwenda jirani tu na hapo kama dakika 5hivi.

Ila ajabu kuanzia saa sita nilifka maeneo saa tisa,
Na pale wakati natembea nilikua napishana na watu wako busy kama mchana halafu ni eneo la kijijini,
Lile tukio sitasahau kamwe.

[emoji252] [emoji479]
bidada wasema kwel?? ilikuwa wp hyo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Habari wana JF,

Nimekua nikisikia kwamba barabarani Kuna vitimbwi vya mauza uza nikawa siamini, sasa ni juzi nilikua natoka Arusha kuelekea Kibaha. Nilifika sehemu jina silifahamu, ni kijiji baada ya kutoka Mombo.

Ni kwamba nikiwa kwenye mwendo alitokea mtu upande wa kushoto akawa anaingia barabarani Kama vile haioni gari nikapunguza mwendo na kupiga honi, nikitumaini jamaa atasimama ama kustuka, badala yake akaongeza spidi na kuliingia gari upande ule ule wa kushoto mimi na jamaa yangu tukasikia kishindo, side mirror ikavunjika ikaweka na kreki mbaya sana kwenye kioo cha mlango wa kushoto.

Nilisimamisha gari fasta tukashuka na kuangalia tunamuona yule mtu anakwenda tu kwa spidi ile ile, kama vile hakikutokea chochote. Tukawa tunashangaa basi yule mtu akaingia kama kwenye kichochoro Kati ya nyumba mbili, hii nyumba ya kulia Kuna jamaa alikua ameketi kibarazani amepaki pembeni gari aina ya vitz.

Tukamfuata jamaa yangu akamuuliza, Ndugu huyu mtu amekatiza hapa unamfahamu ? Maana tumemgonga na gari tumesimama ili tumtazame lakini cha kushangaza jamaa hakuanguka wala kuyumba ameelekea huku. Cha kushangaza tena, Jamaa akatuambia, nyie mpo salama? Tukamjibu ndio. Akasema basi shukuruni nyie endeleeni na safari. Nikamuuliza mbona hatuelewi?
Siku nyingine ndo unapangua gia unaweka 1 unashika uskani vizuri huku ukisali moyoni alafu usikanyage brake kama hakuna kivuko

Badala ya kujibu akabaki ametukazia macho jamaa yangu akanishika mkono na kunivuta tukaondoka. Lakini mpaka sasa hivi tumebaki na maswali vichwani mwetu.

Ni nini hasa kilitokea....

Asanteni

Kama ni highway siku nyingine usikanyage brake kama speed yako imezidi 90kph, piga honi, pangua gia weka1, shika uskani vyema pia sali moyoni wala usifumbe macho,kama hakuna kivuko kanyaga mafuta kama kawa usiachie..tofauti na mtaani haiwezekani Mtu (kama sio mtoto japo
nao hutumika) akavuka mbele wakati gari ipo kasi..
 
Ndo maana wanasiasa wanadanganya watanzania kirahisi sana.
Yaani huu uongo umeandika kama vile unawaandikia watoto wa shule za chekechea.au umetoa kwenye movie. Eti ukatoa bastola 9mm ukawaoneshea dirishan huo usiku nao wakaiona, pia ukawasikia wakiongea,ukajua wapo wangap kwenye gari majambazi hata hawakuweka tinted? Walifungua tu vioo uwaone nadhan waliwasha na taa kabisa uwahesabu, ulipunguza sana mwendo nao wakapunguza wakuoneneshe wapo wangap, na pia wakusikie... Na waone una bastola...

Huu uongo wa kitoto muwe mnaambiana huko shuleni wakati wa break au vijiweni. Anyway watu huwa mnatafuta jukwaa la kuuzia chai.uliona ukisema mauza uza hutaweza sema nliyaonesha bastola ukaona uje na version yako.

Haya baadaye ukakutana na mengine kwenye lorry, hayo ukayaonesha mabomu hand grenades au machine gun yakasema ...tusepe tu.
Acheni utoto na kutafuta sifa za kijinga
ha ha haa,,,mkuu naona umeamua umtolee uvivu kwa kumchana,, any way hao wananogesha stori tuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi nilikuwa naendesha baiskeli mida ya saa moja usiku kutoka Cheyo kwenda Isevya gafla nikakutana na demu mkali sanaaaaa mwarabu amejazia vishungi balaaa . .sikumkwepa akacheka sanaaaa akanambia nimefaulu mtihani wa kumkarawila nilitafuna balaaaaa...leo nipo N.I.T nasomea udereva niwe dereva wa malori nikatafune majini njiani

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom