Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Sukamahela...nina demu wangu pale

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nyie haya mambo ya kiswahili yasikie kwa wenzako kama huamini uwepo wa Mungu, nakumbuka ilikuwa mwaka 2013 natoka sehemu moja inaitwa buyuni ipo ukipita kimbiji kigamboni huko, narudi zangu magomeni, nilikuwa nimeenda kuchukua kuku nina kijifarm kule, sasa kufika mitaa ya cheka nasikia kuku wanalia kama bundi ni asubuhi tu ya saa tatu, nikageuka niangalie huwezi amini nikamwona bibi mmoja anatembea yupo nyuma ya gari yaani namwona kupitia site mirror yule bibi namfahamu ni jirani yangu kule buyuni wakat natoka kule nilimwacha anafagia kieneo chake, nilipata mshtuko mkubwa sana kwa kuwa sikuwa kwenye speed kali nikapaki gari pembeni nikasali sana nilipomaliza nikawasha gari nakuondoka nilipiofika kivukon nikamwona tena, kwa kifupi mpaka nafika home kuku wote 31 wamekufa, nikauza lile eneo na ndio ukawa mwisho wa mimi kwenda tena kule

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha chai mzee baba humu tunasoma mpk mawaziri
 
Duuuh dunia hii inamengi sanaaaa!! Pole sana mkuu

mndamba kutoka Ifakara
 
Huyo jamaa mliemuuliza ndio huyohuyo mliomgonga ndio maana hakutaka mazungumzo marefu. Napaki gari hapohapo namuita tajiri namkabidhi funguo yake maana siwezi kubet maisha yangu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ungebeba tuu ukatoe huduma, acha uoga
 
Fanya kuleta hako kauzì mkuu.
 
Pole sana kiongozi... hiyo ndio dunia tunayoishi mkuu
 
Siku moja usiku nilikua kwenye daladala huko kigoma ,tukafika sehem tukakuta chungu kinawaka moto kati kati ya road, dereva hofu juu juu anaogopa kukatiza. Wenyeji wakamwambia ukisimama tu au kukwepa tumekwisha, dereva ikabid ajikaze kiume apite bila kusimama. Tulipita fresh bila kudhurika na chochote
 
Ukiendesha Gari ukaona umechoka ni vizuri kukubali uegeshe Gari then upumzike kiasi cha kutoa Uchovu..,
Lasivyo utakuwa na Mawenge na kuanza kuona Vioja na maluweluwe ya Majini sijui Vibwengo Mara Majeneza kumbe umelala fofo unaota tu!!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…