Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kuna siku nyingine nilikuwa nakwenda twn ASUBUHI, nikakuta kuna GARI NDOGO imepinduka MAENEO YA KIMARA KOROGWE ni kitambo kiasi,,,wakati ule BARA BARA ya MOROGORO ilikuwa bado ni MOJA,,,before hii Barabara ya MWENDO KASI KUJENGWA,,,majira kama SAA MOJA asubuhi,,,ndipo nikaona watu BADO WANASHANGAA I GARI NDOGO ILIYOPATA AJALI,,,,yaani gari ilikuwa chini kwenye korongo kabisa,,halafu imepondeka vibaya,,,ikabidi nijisogeze kwenda KUSHUUDIA NINI kilitokea pale,,,,ndy nikapata HABARI kupitia watu waliokuwa pale,,,kwenye AJALI,,,jamaa KAPINDUKA na GARI,,,na alikuwa PEKE YAKE ndani,,,,,inasemekana jamaa alikuwa ametoka mjini na anaelekea MBEZI NI SAA TISA ZA USIKU,, ,,,kufika maeneo Yale DEREVA WA GARI NDOGO ambaye kwa muda huo alikuwa yupo hospital,,,,,,anasema YEYE ALIONA WATU WENGI wamevaa KANZU na VILEMBA WANAKATISHA BARABARA huku WAMEBEBA JENEZA WANAKWENDA KUZIKA NI KAMA VILE MSIBA WA WAISLAM unavyokuwa WA nakwenda KUZIKA,,,,,yaani GHAFLA TU kaona WANAVUKA BARABARA wakati yeye yupo speed,,,anasema ikabidi AWAKWEPE,,,ndy akaingia KORONGONI,,,,,GARI ilipinduka zaidi ya Mara 3.JAMAA kupona ni bahati tu,,,hakupata majeraha ya kutisha,,,maana alikuwa bado anajieleza,,,kwa hyo wakuu haya mambo yapo usiombe yakukute,,,na wala huna sababu ya KUBISHA JAMBO HUJAWAHI KUKUTANA NALO,,,wewe jiulize Kwanini WANYAMA WENGI wanagongwa USIKU?ni matokeo ya KUAMINI HAYA MAUZAUZA,,sometimes unaweza kuhisi ni MBWA,, JINI ,,,KUMBE NI MNYAMA KWELI,,,DEREVA makini huwa USIKU hakukwepi...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku niko kwenye basi kutoka Moro kwenda Dar , maeneo mbele ya Chalinze, ulikatiza upepo mkali sana uliopelekea lile basi kutikisika, na basi lilikuwa speed, Sijaelewa ile mechanism mpaka leo , na wala si eneo ambalo labda lina tahadhari ya upepo mkali!
 
nyoka mkubwa ku cross barabara maeneo ya Hedaru, gari iliyumba kwa upepo sana, nilikuwa na watu 3, mmoja alikaa pembeni mwangu na wengine nyuma, pamoja na kuwaambia mnamwona huyo nyoka mkubwa? wote waling'aa macho hakuna aliyemwona, nilipofika alipo cross, gari iliyumba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuuh mkuu hukuogopa?

mndamba kutoka Ifakara
 
Mimi mwaka juzi nakumbuka natoka zangu club nilimuona mwanamke wa kizungu barabarani kavaa baibui mrefu mzuriiiii...ilikuwa kama saa tisa usiku kasimama peke yake. Naamini alikuwa jini
Mixa ukagongana nae macho halafu ukahisi msisimko wa ajabu
 
Ukiwa na Yesu moyoni mwako ameweka makazi yake KATU haya yatabaki masimulizi tu hutayaona kwa macho yako. Katu giza halichangamani na Nuru. Kwa Jina la Yesu naachia ulinzi kwa kila mmoja wenu aendeshaye gari, ulinzi wa Roho Mtakatifu uwafunike katika Jina la Yesu
 
nyoka mkubwa ku cross barabara maeneo ya Hedaru, gari iliyumba kwa upepo sana, nilikuwa na watu 3, mmoja alikaa pembeni mwangu na wengine nyuma, pamoja na kuwaambia mnamwona huyo nyoka mkubwa? wote waling'aa macho hakuna aliyemwona, nilipofika alipo cross, gari iliyumba sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Wao pia walihisi gari kuyumba?
 
Nilikua natoka Mombo naingia Soni njiani nikakutana na watu kama wametoka sijui kwenye sherehe au ni nini wamevaa kama wanaijeria na makanzu wakanipiga mkono nikasimama wakaomba lift nikawapakia ilikua ni coaster kama dk tano tupo kweye safari naona kimya tu kucheki nyuma sikuti watu. nikawatukana tu kum.... zenu nikaenda kupaki
 
Hivi vitu vipo, ilikuwa mwaka 1998 nikitokea South Africa kupitia njia ya Zimbabwe - Msumbiji, tukiwa katikati ya mapori ya Msumbiji mchana wa saa 7 tulimkuta mzee katikati ya barabara amevaa kanzu nyeupee akiwa anatusumamisha, tukaambiana na mwenzangu hakuna kupunguza mwendo, kule kitendo cha kutaka kumgonga alifanya kama watoto wanavyocheza mchezo wao wa rede, akakwepa gari, basi hatukufika hata mita 100 gari ikazima, kusimama hayupo na gari ikawa imenoki engine palepale.

Sent using Jamii Forums mobile app
Baada ya hapo ikawaje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MKUU KUNA siku nilikuwa nakwenda TANGA,,,nipo na jamaa kama 4 kwenye GARI ndogo nikiwa naendesha ,, nakumbuka tulitoka hapa DAR ,mapema kama SAA 12 jioni,,tukaenda mdogo mdogo kufika CHALINZE tukatulia SEHEM vurugu za MABASI NA MAFUSO ZIPUNGUWE,,,kufika kama SAA 4 USIKU tukaanza safari ya kwenda NGAMIANI TANGA,,,TUKIWA kwenye gari story ziliendelea kama kawaida ili DEREVA NISILALE.,,tukaipita MSATA,,salama,,WAMI,,, MKATA,,SEGERA hyo,,,,Salama salmini, HALE ,, tukatoboa MUHEZA SAA nane USIKU,muda huo wenzangu wote nilihisi wamelala,maana ilikuwa kmya,,nlikuwa nasikiliza MVUMO WA INJINI YA GARI NA UPEPO TU,,, sasa balaa likaanza TUMEFIKA kuna SEHEM inaitwa MKANYAGENI,,nikaona mbele kama mita 50 kuna MWANAMKE katikati ya Barabara,,kakaa chini tena yupo UCHI WA MNYAMA,,,amekaa mkao wa kunyoosha miguu kuangalia tulipokuwa tunakuja,,Nikasikia KELELE MMOJA,,,wa JAMAA yangu aliyokuwa mbele ananambiya KANYAGA MAFUTA,,USIFUNGE brake TUTAKUFA,,MCHAWI YULE,,,,,jamaa wote waliamka,,,wakati huo nilikuwa nipo SPEED KAMA 120 HIVI...basi nikakanyaga mafuta nikampitia yule MAMA katikati ,,,means NIMEMGONGA,,,lakini sikusikia DALILI YEYOTE YA KUGONGA,,,,muda huo watu wote walikuwa macho,,,,huku tukiwa na Taharuki ya kugonga MTU,,,nilizidisha speeds ya gari hadi NGAMIANI MJINI,kwa kuwa ilikuwa ni USIKU ilibidi kusubiri kukuche, ,ilipofika ASUBUHI nikaanza kuikaguwa GARI,,AJABU haikuonyesha DALILI YEYOTE YA KUGONGA MTU,,aisee tulishangaa sana,,wala hakuna DALILI KWAMBA TULIGONGA MTU PALE,,PIA,,TULISHANGAA SANA,,, KUNA SIKU ingine nipo PEKE YNGU kwenye GARI,,,ilikuwa kama SAA NANE za USIKU ,, Barabara ya MOROGORO maeneo ya MAGARI SABA DARESALAM , ,,njia ilikuwa imetulia sana muda huo,,,NIKIWA SPEEDS PEKE YNGU BARABARANI,,,,,,mbele kidogo nikaona LORI LINAKUJA KWA KASI WRONG SITE,,means limehama UPANDE wake linakuja kwngu,,ikabidi NIHAME UPANDE wa pili KULIPISHA,,,kuangalia kulia naona kuna LORI LINGINE limewasha taa nalo linakuja kwa speed,,Duu,yaani nipo katikati UPANDE wa kushoto kuna LORI LINAKUJA UPANDE WNGU,,na kulia pia KUNA Lori kwa kifupi niliwekwa katikati ya magari mawili yanayokuja mbele yngu kwa KASI KUBWA,,nilihisi mikono imekufa GANZI,,,pale pale nikapata UJASIRI NIKASEMA MIMI hapa SIENDI PEMBENI,,maana huko pembeni kuna MAKORONGO ,, wakati natafakari ZILE LORI hizi hapa karibu yngu,,yaani zinakuja kwa pamoja mbele yangu,,,,zikiwa zimewasha taa fully..basi na Mimi sijuwi nilipata ujasiri GANI,, nikajikuta nimeng'ang'ania steering huku nakanyaga mafuta,,,kufumba na kufumbuwa nikajiona nimepita katikati ya yale malori lakini sijasikia kishindo,,au DALILI ya KUGONGA,,, na sehemu niliyopita katikati YAKE hata BODABODA HAIPITI..NIKAGEUKA NYUMA SIKUONA HATA DALILI YA GARI KUPISHANA NALO,,..HAPO nilikuwa natetemeka na gari ilizima kwa woga,,,,KESHO,,, nilipo muhadithia jamaa yng mmoja akaniuliza HIVI UNAJUWA YALE MARINGI YA SHABA,, WANAYOVAA MADEREVA WA MASAFA MAREFU MKONONI NI YA KAZI GNI? MFANO MADEREVA WA MALORI AU MABASI MAKUBWA YA MIKOANI,,,,WENGI WAO WANA MARINGI YA SHABA MKONONI,, nikamwambiya sijuwi,,akasema WAULIZE,,vinginevyo usipende kutembea usiku wa manane,,especially peke YAKO,, nikakumbuka kuna kitu natakiwa nikifanye kama DEREVA WA USIKU....

Sent using Jamii Forums mobile app
Duuu!!! Hiyo ya malori noma

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Duuu!!! Hiyo ya malori noma

Sent using Jamii Forums mobile app
Hatari sana mkuu,,vitu vingine hadi vikukute ,,vingine utaona ni story z kawaida,,ila Mimi sipendi kutembea USIKU sana,,,sio na gari hata kwa miguu,, ikifika SAA sita sijafika kwngu nakuwa na hofu sana ,,,mauzauza huanza SAA sita nanusu kwa sehem za MITI MIREFU AU PORINI,,,lakini sehem za mjini ni UKIWA USIKU MKUBWA,,,WENYE UPWEKE,,,nane,,Tisa,,Tisa na nusu,,hatari Sana MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana mkuu,,vitu vingine hadi vikukute ,,vingine utaona ni story z kawaida,,ila Mimi sipendi kutembea USIKU sana,,,sio na gari hata kwa miguu,, ikifika SAA sita sijafika kwngu nakuwa na hofu sana ,,,mauzauza huanza SAA sita nanusu kwa sehem za MITI MIREFU AU PORINI,,,lakini sehem za mjini ni UKIWA USIKU MKUBWA,,,WENYE UPWEKE,,,nane,,Tisa,,Tisa na nusu,,hatari Sana MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
Huo ujasiri wa kupita katikati ulikujaje mkuu?maana sipati picha ilikuwa hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huo ujasiri wa kupita katikati ulikujaje mkuu?maana sipati picha ilikuwa hatari sana

Sent using Jamii Forums mobile app
Ilikuwa no way out MKUU,, maana tayari nilikuwa KATI KATI ya BARABARA,,, mbele yangu magari mawili yamenitokea,,hata kama ningeenda pembeni nisingewahi,,,,ikabidi nikanyage mafuta,,,lakini kwny nafsi yang nilijiona ni kama ndy mwisho wa maisha yngu,, sikuamini kama ningeweza kupita pale kati kati ya zile Lori,,ilikuwa NO WAY OUT,,,,,kwnz nimemulikwa mataa usoni,,mbele KMO sioni vizuri,,akili yng ilidhani pengine mmoja wa DEREVA wa lori ndy angenikwepa Mimi,,,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hatari sana mkuu,,vitu vingine hadi vikukute ,,vingine utaona ni story z kawaida,,ila Mimi sipendi kutembea USIKU sana,,,sio na gari hata kwa miguu,, ikifika SAA sita sijafika kwngu nakuwa na hofu sana ,,,mauzauza huanza SAA sita nanusu kwa sehem za MITI MIREFU AU PORINI,,,lakini sehem za mjini ni UKIWA USIKU MKUBWA,,,WENYE UPWEKE,,,nane,,Tisa,,Tisa na nusu,,hatari Sana MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna siku nilikua natembea njiani Muda wa saa sita hivi
Nilikua navuka uwanja kwenda jirani tu na hapo kama dakika 5hivi.

Ila ajabu kuanzia saa sita nilifka maeneo saa tisa,
Na pale wakati natembea nilikua napishana na watu wako busy kama mchana halafu ni eneo la kijijini,
Lile tukio sitasahau kamwe.



[emoji252] [emoji479]
 
Back
Top Bottom