Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kwa madereva: Tuliowahi kutokewa na mauzauza barabarani tupeane uzoefu

Kuna ndugu yangu mmoja anaendesha magari makubwa, ilikua trip ya kutoka wilayani kuelekea mwanza (approx 200Km)
alianza safari saa 12 jioni mpaka kunakucha hajafika alikua anakutana na barabara nyingi ambazo akizifuata zinaishia mitoni
wachawi pumbavu zao
Duh mafuta yakiisha hapo balaa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app

We kama muongozo vileee

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndoto, usingizi na imani za kishirikina.

Hakuna kitu. Why usiku na si mchana??

Why barabarani tu na si njia ya train, Angani au Majini??.

Story za abunwasi na changamsha genge.

Nishasafiri Barabara nyingi, masaa yote kuspan 24 hours sijashuhudia hayo.

Ulongo tu na kutiana woga, kuwapa ulaji waganga wa kienyeji wafanye zindiko.
Bisha tu usilolijua
Rafiki yangu aliwahi kuchukuliwa kichawi akarudishwa
So subiri uje ushuhudie

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mzoefu wa safari za usiku na sikuwahi kuona maluelue yoyote! Mimi nadhani ni imani tu. Wengi wanakutana na watu kama walevi, viziwi au vichaa wakivuka barabara na kuoanisha na imani za kishirikina. Hofu yangu ni kuona watu wanahamasishana kuua kwa kugonga bila kujali ni binadamu wenzetu.
MKUU Mara nyingi tukio linakukuta UKIWA peke yako,,,,hata kama mpo wengi lakini wenzio wamelala muda huo,,,hapo ndy unaona mauzauza,,,,kuna JAMAA ZANGU 2 walipata ajali ile bara bara ya SALENDER BRIDGE,,,DAR,,pale DON BOSCO kwa mbele PANA MBUYU mkubwa kati kati ya Bara bara,,jKITUO KINAITWA MBUYUNI,,,Jamaa zng wamepoteza maisha kwa siku tofauti,,,gari imegonga MBUYU akiwa peke YAKE,,,USIKU wa manane,ALIKUWA AKIENDA KWAKE ,,TENA kila mmoja kagonga kwa SIKU YAKE lakini vifo vinafanana,,,,haya mambo Yapo mkuu,,,hadi yakukute ndy utaamini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapa jukwaani nani anavifahamu vyombo vya kioo? Ni Vitombe na Sahani za kioo! Basi siku moja natoka SHY kwenda Mhunze, kabla ya daraja nikakuta katikati ya barabara hivyo vyombo vimewekwa ugali ndani yake na kufunikiwa kama mtu ametengewa chakula, kikombe kimejaa maziwa! Cha ajabu kabla ya eneo hilo nilipishana na lori lakini halikuvigonga vile vyombo, sasa Mimi nikapunguza mwendo nikapita pembeni. Kama hatua ishirini hivi nikasimama nikarudi kucheki tukio, hamaaadi.sijakuta kitu chochote!!
Vitomb* ndio nini ?

Shy wachawi mno
1.kuna siku nikiwa advance, nipo likizo home nikakabwa usiku
2.kuna siku uvunguni mwa gari yetu tukakuta ngozi ya paka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu pole sana hiyo sehemu naijua mana nimekulia maeneo hayo,ukitoka mombo,kuna vijiji kadha kama mwelia,mwisho wa shama,kikwazu,chekelei,madumu,hizi sehemu ni mbaya sana, kipindi hicho usafiri ni baiskeli nikawaida kuwa beba hao viumbe wajastuka baiskeli imekuwa nzito ghafla pia kaharufu ka jasho la mtu utahisi,salama yenu nikule kumgonga huyo jama vinginevo ni hatari tupu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna habari iliwahi kurushwa redioni, kule kishapu shinyanga wakati huo, mkuu wa wilaya alisimamishwa na babu mmoja ili amsaidie kusogeza matofali, na mkuu akasema huyu babu anasemaje huyu, aka akili sawasawa ? Akamwamuru dereva wake waondoke. Babu akakaa. Wakaingia kwenye gari wakawasha wakajiona wanaenda kwa masaa zaidi ya manne hawakuwa wamefika na no mahali pa kwenda kwa nusu saa,. Walipo simamisha gari kutoka nje wakajikuta wapo pale pale hawajaondoka. Ilibidi wamwombe mzee wampe na hela ya kuweka kibarua mtu abebe. Ndipo babu akawaruhusu wakaondoka

Sent using Jamii Forums mobile app
Mwaka 2007 mugumu .mkoa wa mara
Kuna jamaa jirani yetu alikua mwalimu wa primaly
Sa kuna siku anaenda job akakutana na bibi kizee mchana wa saa saba
Bibi akaomba lifti jamaa akamtolea nje akasepa
Ghafla jamaa akaanza kuhisi baiskeli nzito akakazana tu .kufika maeneo ya shule, jamaa ile anashuka .bibi nae huyu "Ahsante mjukuu wangu"
Jamaa hakujibu aliogopa mno

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna siku ilikuwa 2007. Nikitoka Arusha kwenda Dar saa Saba Nane usiku nilikuwa napita maeneo ya kwedikwazu. Kuna mahala Barbara imenyooka Sana Basi nikawa natembea speed 100-120.
Kuna mrembo mmoja mdada akawa anasimamisha gari akiomba lift. Nikapiga taa kubwa kumwona vizuri mrembo haswaa, sikusimama nikanuoosha goti, huku najiuliza huyu anaenda Wapi saa hizi,. Bwana ile nampita kwa speed ile alinipiga busu Mara tatu hapo dirishani. Maana sikuwa nimefunga madirisha ili nipigwe upepo nisilale. Nilifika dar Sina raha kutwa nzima.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu hii chai sasa😂😂😂😂😂
 
Kuna ndugu yangu mmoja anaendesha magari makubwa, ilikua trip ya kutoka wilayani kuelekea mwanza (approx 200Km)
alianza safari saa 12 jioni mpaka kunakucha hajafika alikua anakutana na barabara nyingi ambazo akizifuata zinaishia mitoni
wachawi pumbavu zao
Haaaaaaa daah mkuu achaaa hayo huko Sudan/darful ndo shidaaaa

mndamba kutoka Ifakara
 
Hiyo kawaida kabisa kwa sisi tunao safiri safari kila mkoa mara nyingine unamkuta bibi tena yule unaemfaham lakini alishakufa au mbabu na bakora mkononi wakati mwingine unaona picha ya jeneza kabisa limefunguliwa na sanda ipo au mtoto mdogo anatambaa yaani tushazoea wala hofu ile haipo tena.
Onyo.ukiona vitu kama hivyo usijaribu kukwepa au kushika break inakula kwako.
Mi kukna siku naenda dodoma niko na ford new model kuna kizee kilitokea vichakani kikasimama ghalfa barabarani haki ya (mungu mungu nisamehe)nilikaza mikono kushika steling vizuri nilimpa nikafumba macho ili nisione ninavyoua huwezi amini nilimpita na sikusikia kishindo chochote na nilienda mbele kama 4 klmtrs nikapaki gari kuangalia sikuona tatizo kwenye gari na niliendekea nabsafari yangu bila presure.
Hee! Mungu epushia mbali,sijawahi kushuhudia vitu kama hivyo safarini

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sitasahau mwaka jana nilipopata ajari katika mazingira ya kutatanisha mbeya mjini, niligongwa na Ambulance yaani ilikuwa kwenye kona tumeongozana magari mawili mimi nilikuwa nyuma na gari dogo pia kulikuwa na gari dogo ambalo tulikuwa tumeongoza nalo baada ya kukuta kona ilikuwa ni kama nimepigwa usingizi hadi nilipokuja kushtuka baada ya kusikia kishindo kikubwa baada ya kugongwa na ambulance, bahati nzuri tulitoka wote salama.
 
Ndoto, usingizi na imani za kishirikina.

Hakuna kitu. Why usiku na si mchana??

Why barabarani tu na si njia ya train, Angani au Majini??.

Story za abunwasi na changamsha genge.

Nishasafiri Barabara nyingi, masaa yote kuspan 24 hours sijashuhudia hayo.

Ulongo tu na kutiana woga, kuwapa ulaji waganga wa kienyeji wafanye zindiko.
Bado tu Siku yako itafika utayaona hayo yasemwayo. Yakikutokea zingatia unavyoambiwa :--Usifunge brake, wala usikwepe, nyoosha usukani, to a mguu kwenye kijiko cha mafuta.. "Kalaga baho".

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom