PAC wanahusikaje mkuu?
Wao wanasubiri tu taarifa ya mwisho..
Hawahusiki na usimamizi before taarifa.
Nijuze nijifunze kitu ndugu
PAC kazi yao ni kuisimamia serikali, kuishauri na kuizuia serikali kufanya project zitakazo sababisha hasara kwa taifa. Na PAC sio tu wanafanya kazi kwa kuletewa documentation juu ya meza na kuzifanyia kazi, pia wanayo mamlaka huru ya kuamua kufanya uchunguzi wao wenyewe kujiridhisha kwa kuunda tume.
2010 - 2015 PAC waliwahi kuunda tume huru kwenda kuchunguza migodi ya mwadui, buzwagi na kwengine. Walikua wakifanya kazi huru.
Kwa miaka 5 (2015 - 2020) PAC imeshindwa kuisimamia serikali katika project za ATCL na TTCL mpaka kufikua hatua imesababisha mabillioni ya hasara.
1) PAC kwanini hawakuizuia serikali isiingie kichwa kichwa kwenye ku invest hela nyingi sana katika hizo project??? Licha ya baadhi ya wabunge wa upinzani/mashirika ya ndege/wafanyabiashara/wanaharakati kuonya kwamba biashara hio ni kichaa.
2) Wakisema hatukujua kama project hizo zilikua zinaingiza kiasi hicho cha hasara. Je, walifanya jambo gani ku minimize hasara??? Waliunda tume kuchunguza hayo waliokua wakiambiwa na serikali ili kuyathibitisha???
3) Ni aibu PAC kupewa kazi ya kuisimamia serikali, halafu mabillioni ya hasara serikali inaliingiza taifa bila wao PAC kujua, wanakuja kujua CAG anapotoa mahesabu. Je CAG asingetoa hayo mahesabu au angedanganya ina maana PAC wasingejua??? Kuna haja gani ya kuwa na PAC bungeni kama hawajui hata mashirika ya serikali yanaingiza hasara nchi???
Na cha zaidi, hata waliojaribu kuwaambia ukweli, waliowaona ni wabaya. Mfano,
SPEAKER NDUGAI akumbushwe CAG Prof Assad alifanya ukaguzi wa mahesabu ya serikali, na aligundua huu ushenzi na madudu yote yaliofanyika... Ila aliposema kweli na kuweka wazi report yake, alikua mkali na kiherehere namba moja kumkashifu, kumwekea tamko la kutokufanya nae kazi, na kumdhalilisha kwa kumvua mkanda mpaka viatu siku anaingia bungeni. Wabunge wa CCM walimuunga mkono Speaker wao.
Sasa, CAG Kichere nae ameongea yale yale aliosema mwalimu wake CAG Prof Assad. Na yeye weka zuio la kufanya nae kazi bungeni!!!
Kifupi, wameshindwa kufanya kazi zao, walikubali kudanganywa na wakadanganyika. Walishindwa kutumia mamlaka yao huru ya kufanya uchunguzi kujiridhisha project za serikali zinaendeshwa kwa faida au hasara.