Rehema ya Mungu ilimuongoza Rais John Pombe Magufuli kujua kuwa muda wake wa kuondoka umefika,alisema waambie madaktari waniruhusu niende nyumbani,Gen Mabeyo akajibu Mh suala la afya sina mamlaka nayo, tusubiri madaktari wanasemaje, naomba utulie upo kwenye mikono salama,akasema niitie Paroko wangu wa Oysterbay na Kardinali Pengo,tulimkosa alikuwa kwenye misa lakini baada ya misa Kardinali Pengo alikuja pamoja na Paroko wa Parokia ya Oysterbay wakamsalia na kumpa sakramenti ya upako wa Wagonjwa,wakamuogoza sala ya toba na sala ya mwisho,akapumzika,jioni akakata roho,kwa wakatoliki hiki ni kifo chema na unakwenda mbinguni.
-Mwenye kujaji ni Mungu peke yake Luka 18:9-14
9 Yesu alitoa mfano huu kwa ajili ya wale waliojiona kuwa wao ni wenye haki na kuwadharau wengine. 10 Watu wawili walikwenda hekaluni kusali, mmoja wao alikuwa Farisayo na mwingine alikuwa mtoza ushuru. 11 yule Farisayo alisimama akasali kimoyomoyo. ‘Ninakushukuru Mungu kwa sababu mimi si kama watu wengine: wany ang’anyi, wadhalimu, wazinzi, au kama huyu mtoza ushuru. 12 Mimi nafunga mara mbili kwa juma na kutoa sehemu ya kumi ya mapato yangu.’ 13 Lakini yule mtoza ushuru alisimama mbali. Hakuthubutu hata kuinua uso wake kutazama mbinguni; bali alijipiga kifuani kwa majuto akasema, ‘Mungu, nihurumie, mimi mwenye dhambi.’
14 Nawaambieni, huyu mtoza ushuru alirudi nyumbani akiwa amehesabiwa haki mbele za Mungu na wala si yule Farisayo. Kwa maana ye yote ajikwezaye atashushwa na ye yote ajinyenyekezaye, atainuliwa.” mara nyingi ndugu wa mgonjwa ndio humfuata baba Paroko na kumuomba ampatie mgonjwa sakramenti ya Mafuta matakatifu,lakini Shujaa Magufuli yeye mwenyewe alimuagiza CDF awaite Baba Paroko na Kardinali Pengo kwa ajili ya Huduma,basi Yesu Kristo alisema " Dhambi zenu zijapokuwa Nyekundu zitafanywa nyeupe kama theruji" na tena " Watoza Ushuru watatangulia kuuona Ufalme wa Mbinguni kabla yenu",ni vyema Gen Mabeyo ametoa Ufafanuzi maana umezima uvumi mwingi kama ule wa jamaa wa ubelgiji mara hivi mara vile ukiwemo ule wa COVID 19,
-Kwa Wapagani kama Yericko Nyerere.
Wapo wanaoendelea kumtukana Marehemu,kumhukumu wao wamejigeuza Miungu wanahukumu,wapo wanaokufuru kama vile wao hawaji kufa,wapo wanaosema karma imefanya kazi sababu uongozi wake usalama waliteka,mara walimpiga risasi Lissu,kwa kuwa hakuna anayejua wala msema ukweli wao wanaamini karma imefanya kazi,karma ni malipo ya dhambi,basi kama ni kweli karma imefanya kazi na Hayati amelipa deni la dhambi basi baada ya kulipa malipo ya karma,deni linakuwa limelipwa in full,hivyo hakuna haja ya kuendelea kutukana na kukufuru kwa maana mtu wetu ameingia peponi mbinguni kwa Baba yake,rejea makala ya Pascal Mayala kule jamii forum yenye kichwa Voices From Within:Je, wajua yuko Peponi, Mbinguni,kwa Baba yake? Why kumshutumu, kumsakama na kumsimanga? Aachwe apumzike kwa amani,Nakuombea nawe ndugu msomaji,Mungu akujalie kujua siku yako ya kufa ili uweze kuandaa nyumba yako na kutubu,kwa maana hakuna binadamu mkamilifu hata mmoja.
Nikiishia hapa, Mimi ni
Msemakweli Chakubanga,
Dar es Salaam.
0755078854
-Bachelor of business administration in International business.
-Master of Leadership and Management.
Recent Publications;-
-Assessment on the Effects of Micro-financing on Poverty Reduction.