Kifo chake kilikuwa kifo chema kwa sababu alikufa akimtafuta Mungu ili amsamehe dhambi zake na pia alijua kwamba anakufa!
Tunachojua Ki Biblia ni kwamba mtu akifa akiwa na Roho Mtakatifu moyoni mwake, roho yake inakwenda peponi au paradiso na kama hana Roho Mtakatifu moyoni mwake, roho yake inakwenda kuzimu.
Mtu akifa, hatuna uwezo wa kufuatilia na kujua roho yake iko wapi!
Hakuna aliye na uwezo wa kufanya utafiti juu ya njia za Mungu na hukumu zake.