Kwa mambo yote haya, Rais Samia hapendi mapambio

Kwa mambo yote haya, Rais Samia hapendi mapambio

mapessa

JF-Expert Member
Joined
Oct 9, 2014
Posts
664
Reaction score
1,168
Ndani ya Kipindi kifupi tumeona uwekezaji uliovunja rekodi tangu tupate Uhuru. Hatujawahi kuvutia uwekezaji kwa kiwango cha trilioni 9.6 thamani ya uwekezaji ndani ya miezi 9 yaani uwekezaji wa Rais samia miezi 9 unazidi uwekezaji wa miaka 4 iliyopita huyu Mama hana sifa ya kujikosha na kujitweza, haya mambo ndiyo yanawanyima usingizi na Raha wahasidi wake.

Tusichokijua kwa Rais Samia kitaaluma amesomea UCHUMI tena ni mchumi kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika Uingereza mambo yake yanaonekana.

Kuhusu kodi amevunja rekodi hivyo ana uwezo wa kukopa na kulipa madeni yote tuliyorithishwa.

Piga kazi!! Samia the Great!!
 
Mkuu unaweza ukataja miradi michache inayoakisi huo uwekezaji wa fedha hiyo?
 
Uko wapi huo uwekezaji
Umenikumbusha wakati wa sakata la Richmond Kuna dogo alitoka mbio mkoani KWENDA dar kutafuta hiyo kampuni apate Ajira ,hakuiina hata Bangor la ofisi ,alivyorudi akasema nimetafuta ofisi za Richmond sijaziona Kila akipita anakutana na mabango ya tunauza vocha hapa .
 
Lile jitu la mapambio na propaganda ndilo liliwaharibu wajinga ..

Samia kafanya mengi ya msingi kwa mda mfupi bila mapambio ya kipuuzi.
 
Lile jitu la mapambio na propaganda ndilo liliwaharibu wajinga ..

Samia kafanya mengi ya msingi kwa mda mfupi bila mapambio ya kipuuzi.
Mbona Sasa hivi hali inazidi kuwa mbaya kwenye mapambio Hadi hospital wanatembea na picha yake? Jana pia kwenye Daraja jipya wamekodiwa watu watembee na mabango ya picha yake

20220201_195633.jpg
20220201_142726.jpg
 
Ndani ya Kipindi kifupi tumeona uwekezaji uliovunja rekodi tangu tupate Uhuru. Hatujawahi kuvutia uwekezaji kwa kiwango cha trilioni 9.6 thamani ya uwekezaji ndani ya miezi 9 yaani uwekezaji wa Rais samia miezi 9 unazidi uwekezaji wa miaka 4 iliyopita huyu Mama hana sifa ya kujikosha na kujitweza, haya mambo ndiyo yanawanyima usingizi na Raha wahasidi wake.

Tusichokijua kwa Rais Samia kitaaluma amesomea UCHUMI tena ni mchumi kutoka vyuo vikuu vinavyoheshimika Uingereza mambo yake yanaonekana. Kuhusu kodi amevunja rekodi hivyo ana uwezo wa kukopa na kulipa madeni yote tuliyorithishwa.

Piga kazi.......!!! Samia the Great...!!!
Kamtimua sipika kwa sababu ya kukosolewa.

Unaweza kumtetea hapo?

Hiyo Miradi ya hizo pesa ni ipi?
 
Back
Top Bottom