Kwa maneno haya ya Polepole inamaanisha kifo cha Magufuli kina mchezo mchafu ndani yake?

aisee magufuli sio wa kwanza kufa humu duniani, hata sisi tulishafiwa na ndugu zetu tutoleeni upumbavu humu, yeye alikua na hatimiliki ya kuishi daima?
Sijuhi hata kama watakuelewa!! Mtu mwenyewe alikuwa naivèna clueless
 
Basi mkaifukue mfanye autopsy kwa kifo kama ni maradhi au vingine

Kila kukicha ni haya haya tu
Wangapi wamekufa jamani na tunasema tu kafa basi ?
 
Huyu chawa still bado aamini mungu wake amekufa
 
Kunguni yafaa abuni njia atafute mbadala ya kuishi baada ya godoro kupigwa dawa aache kulia kulia magu afufuki tena.
Kama hakujipanga imekula kwake haiji mara mbili bahati
 
True. Polepole anajua kishafikia mwisho wake kisiasa hasa ndani ya CCM unless zitokee miracle kama zile zilizomuingiza CCM.... Which is very unlikely.

Anachojaribu kujifanya kwa sasa ni kujaribu kuendelea kuwa relevant kwenye siasa za Tanzania... Ila naona kama vile anafanya makosa mengi kwa kipindi kifupi.
 
Sasa hapa mbona ni kama wewe ndo unaetueleza habari za hicho unachoita mchezo mchafu?? Maana polepole hajakizungumzia!
Mama tayari alishasema mjadala huu umekwisha hivyo tuheshimu maagizo ya mkuu wetu wa nchi maana hata kama tutachonga vipi Mwendazake hawezi kufufuka!
 
So ukijua itakusaidia nini au unataka uamshe kilio kwa makonda na sabaya waanze kulia upya
 
Napenda Kushauri Janeth Magufuli, Jesca Magufuli, na wale Watoto wengine Wajiunge JF anonymously watueleze wanayoyajua kuhusu baba Yao.

Mama Janeth Magufuli Alilia Sana Msibani.
 
Watanzania na uwezo wao wa kutunza hasira na visasi. JPM alikuwa na matatizo makubwa ya moyo ambayo hakuyachukulia kiumakini katika kuyatibu.

Ilipokuja corona hatari ya yeye kupoteza maisha ikawa ikiongozeka siku baada ya siku. Angetaka angeweza kutibiwa Ujerumani au sehemu yoyote duniani lakini alishaamua kuishi hivyo hivyo.
 
Kumuita mpumbavu umekwenda mbali sana. Mtunzie heshima hayati kwani huwa hasemwi vibaya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…