Kwa maoni ya Dkt. Slaa, inawezekana Ben Saanane na wengine walitekwa na kupotezwa na Chadema

Kwa maoni ya Dkt. Slaa, inawezekana Ben Saanane na wengine walitekwa na kupotezwa na Chadema

Kuna vitu vingine ni bora kukaa kimya badala ya kuongea, kwa kuwa unapoongea watu wataweza kujua kina cha busara zako kama ni kirefu au kifupi sana. Katika maisha, ni bora kukaa kimya watu wadhani una busara, kuliko wewe kudhani una busara ukaongea hadharani na kufanya hata wale waliodhani una busara watambue kuwa huna busara.

Mfano ni hili la Lissu na suala zima la kupigwa risasi. Ni kweli hatuna ukweli wote, lakini pia kuna viashiria vingi kwamba vyombo vya usalama vya Serikali havikulipa uzito unaostahili katika kulipeleleza. Na pia kumekuwa na circumstantial evidence nyingi sana kwamba kwa namna moja au nyingine Serikali ilihusika. Sasa pale Dr. Slaa anaposema hawezi kuongelea hili, kisha anaeleza kisa cha mtu alietekwa na watu wa CHADEMA wenyewe, ni wazi ana nia ya kuufanya umma uamini kwamba kuna uwezekano Lissu alipigwa risasi na watu wa CHADEMA.

Lakini sasa, hili wazo la Dr. Slaa lingekuwa na circumstantial evidence nje ya huyo alietekwa na Chadema wenyewe, labda ndio angepaswa kuliunganisha na hicho kisa kingine. Na Dkt Slaa, anajuaje kwamba huyo aliesema aliongoza kumteka mtu wa CHADEMA yote hiyo haikuwa part ya plan ya kuwavuruga CHADEMA kwa kuwagonganisha wao kwa wao? Hivi Dr. Slaa hajui dirty politics zinavyochezwa, kampuni ya soda hii kuweka kondomu kwenye chupa ya kampuni ya soda ile ili watu waione ni kampuni ya soda chafu?

Kwa mfano, hivi Dr Slaa anajua kwamba muda mfupi baada ya Lissu kupigwa riasi Magufuli alimpigia simu Mwigulu Nchemba kama waziri wa Mambo ya Ndani atoe tamko kwamba serikali haikuhusika na jaribio la kumuua Lissu? (Mwigulu baada ya kupata ushauri wa wazee fulani wa CCM hakufanya hivyo, ikawa sababu mojawapo ya Magufuli kumchukia na hatimae kumtoa uwaziri). Muulize Mwigulu atakuambia, na utaelewa kwa nini pia Magufuli aliwachukia wazee fulani wa CCM.

Je, Dr. Slaa anajua kwamba Lissu alikuwa shadowed kwa muda mrefu kabla ya tukio? Je, anajua CCTV recordings ziliondolewa pale kwenye eneo la tukio? Je, Dr. Slaa anajua kwamba barabara zilifanywa tupu ili gari lililotumika kwenye jaribio liweze kupita bila pingamizi kuondoka sehemu ya tukio? Je, Dr. Slaa anajua gari mpya ya Nissan Patrol ilitumika na kuchomwa moto ili kuharibu ushahidi? Sasa nani ndani ya CHADEMA anaweza ku-mount operation ya namna hiyo dhidi ya Lissu?

Nani ndani ya CHADEMA anaweza ku-mount operation za aina ya utekaji na uuaji uliofanywa na kuufanikisha bila kuwa na support ya Serikali, na vyombo vya usalama vikae kimya bila kuwakamata kwa kutumia kila aina ya nguvu? Operation za namna hiyo ambazo nyingine zilifanyika mchana kweupe, zinaweza tu kufanyika ikiwa wanaozifanya wanajua Serikali na vyombo vya usalama viko nyuma yao. Yaani hili ni gumu sana kwa Dr. Slaa kulielewa?

N wazi sana Dr. Slaa amekuwa currupted na zawadi ya ubalozi aliyopewa na Magufuli, na sasa inamfanya kuwa shabiki namba moja wa Magufuli. In fact anaonyesha hata silka ya kumshutumu na kumpiga Rais Samia vijembe kichinichini kwa huu ushabiki wake kwa Magufuli. Dr. Slaa amekuwa psychologically bribed and corrupted na zawadi ya ubalozi kiasi kwamba sasa anajisahau kabisa, he is becoming so naive to the extent of forgetting to be clever. Poor Dr Slaa.
Kagusa kwenye kidonda chenu. Chadema ni waongo sana. Unakumbuka Mbowe alitangaza kuvamiwa na vijana eti ni wa Ccm. Lakini ilifahamika kuwa alilewa akaanguka kwenye ngazi, na hata kijana wake mwenyewe anathibitisha usiku ule alitika kunywa na kimada wake.

Siyo aibu ile? Chadema hamuaniniki mbele ya wenye akili zao.
 
Ilifanyika hivyo ili kumumaliza Kabisa kisiiasa Hayati JPM na alikuwa hajui kuwa lilikuwa ni kosa kwake kutokujua hilo. Ni kosa alilofanya JPM na walijua kuwa atafanya kosa la namna hiyo. Professionals hawawezi kwenda kwenye eneo la tukio wakiwa hawana Plan B. Stil, wakamimina risasi kama mvua na bado wasiweze kumaliza target yao. TL hakushambuliwa na Professionals, alishambuliwa na amateurs, yeye mwenyewe anajua hilo! Ili kumumaliza kabisa JPM, huduma kwa TL zikawa mbovu sana na hatimaye, ...... now you connect the dots!
Hakuna siri ya watu wawili, kuna siku mtu ataongea kilichotokea siku ile
 
bado huwa mnaangaika na huyu mzee basi na nyie mna matatizo
 
Mtoa mada, mgojwa wa ukimwi hagunduliwi kwa kuangaliwa, bali kupimwa. Asante.
 
Shida ni kwamba mnashindwa kutushawishi yafuatayo.
1. Nani alipangua zamu za ulinzi za polisi kwenye makazi ya viongozi?
2.Nani alisafisha njia ili kuwe na safe exit baada ya excution?
3. Nani alitoa cctv camera kwenye makazi ya viongozi?
4. Lissu alitaja mpaka gari iliyomtail toka dar mbona haijakamatwa?
5. Kama imepigwa kiberiti kupoteza ushahidi je nanani?
6. Lissu alimuomba kwa kuwataja siro na kipilimba in personal.
7. Kwanini serikali inakataa hoja ya wapelelezi huru kama scotland yard?
8. Kama inaogopa kufitinishwa na scotland yard mbona haitumii vyombo vyake polisi na tiss kumpeleleza?
9. Kauli ya Magufuli dakika chache kabla ya shambulio je haiwezi kutoa clue? ( This is government)
10. Kwanini watetezi wa ccm/gvt wanamtaka dereva wa lissu ila hawana haja ya kumjua mpangua zamu za ulinzi wa polisi na mchomomoa kamera ya cctv?

Maswali ni mengi mno sasa nimalizie kama msemaji mmoja hapo juu chadema wanawezaje kuendesha op kubwa kama hii na hawana jeshi wala polisi?
 
Dr.mihogo hana mpya analazimisha kuendelea kuonekana na chadema wananifurahisha maana ni kama wamempotezea hivi hakuna anayehangaika kumjibu.[emoji1787]
 
Mtoa mada, mgojwa wa ukimwi hagunduliwi kwa kuangaliwa, bali kupimwa. Asante.
Unakosea Mkuu. Mgonjwa wa ukimwi unaweza kumjua kwa macho, ila mwathirika wa VVU huwezi kumjua kwa macho.
 
This is very simple than you think: Tuombe USA au Uingereza watupe wapelelezi wafanye uchunguzi. Kuna mengi sana wanaweza kutusaidia. Kupigwa risasi Mh. Lissu, Azori Gwanda na Ben Saanane kutoweka nk....
CCM hawezi kukubali, mauaji waliyoyafanya ni mengi mno na high-profile murder incidences ni direct orders kutoka Ikulu.
 
Nimekupata mkuu. Samahani sana nilikuwa nimekusoma vibaya au nilichanganya madawa. Mimi na wewe tuko page moja kabisa. Nadhani kuna mada nilichanga nikadhani namjibu jamaa fulani.
Wewe ulisoma heading ukaenda ku comment, hukusoma maelezo yote, mbona jamaa ameeleza vizuri sana. Nilipoona comment yako nilikuonea huruma kwamba hukusoma na kuelewa.
 
Kama serikali haijahusika wameshindwa nini kufanya uchunguzi??, Kwamba chadema ina nguvu kuliko usalama wa Taifa au jeshi la polisi??. Huu upuuzi wakutetea vitu ambavyo hata mtoto wa darasa la saba anavifahamu ni ukichaa.
Chadema na CCM vyote ni vyama vya serikali, kwaiyo hakitokea mtu wa kuhatarisha ulaji wao pamoja na usalama wa serikali wanashirikiana kumshugurikia.
 
Haipo Serikali duniani inayoweza kufanya mambo ya kijinga kwa jinsi hii kama yanayodhaniwa kufanyika awamu ya 5 ya Hayati JPM. In fact JPM na Serikali yake hawakuhusika

Huko mbele ya safari mimi naamini kabisa kuwa ukweli wote utakuja kujulikana tu. Vita kati ya ukweli na uongo, uongo huwa unaanza unashinda kwanza, halafu ukweli ndiyo unakuja kumalizia kwa kushinda mwisho.
Ungeweza kutoa mchango wa kudaidia kidogo angalau kwa kutuambia zil CCTV camera zilizopo kuwa eneo la tukio zilienda wapi. Nani alizitoa, na kwa sababu gani?
 
BAVICHA kama kawaida wameishiwa hoja, wamejaa matusi.
Kutukana hakusaidii zaidi ya kuonyesha tabia zenu na jinsi mnavyotumika!
 
Ungeweza kutoa mchango wa kudaidia kidogo angalau kwa kutuambia zil CCTV camera zilizopo kuwa eneo la tukio zilienda wapi. Nani alizitoa, na kwa sababu gani?
Hoja hapa hata mimi sikatai kuwa CCTV zilizimwa. Ninachokataa ni kwamba wahusika hawakuwa Serikali;isipokuwa watu wengine tu ambao walikuwa na ujanja wa ku-pretend kama Serikali
Hivi wewe hujiulizi uamuzi wa mtu anayeshikilia mhimili mkubwa kabisa wa nchi kukataa kufanya kazi na CAG; ulikuwa ni uamuzi wa busara? Tatizo lililokuwepo ni kwamba mengi yaliyokuwa yakifanyika, JPM alikuwa hawezi kuona nyuma yake yalikuwa yanamaanisha nini; ndiyo tatizokubwa lililokuwepo na ndiyo lile linalopeleka confusion kwa watu walio wengi.

Mbali na hayo, Mbunge waJMT amejeruhiwa vibaya sana yuko mahtuti, na hapo hapo hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa ku-rescue maisha yake; na wakati alipokuwa anajeruhiwa CCTV camera zilikuwa zimezimwa!

Angalia vizuri matukio haya namna yalivyo. Usiwe unasikia kishindo kikubwa pale uliposimama halafu unaanza kuangaza macho hapo hapo ulipo kwenye miguu yako hapana. Ukisikia kishindo kikubwa hapo ulipo, kama upo Kariakoo, angalia Chalinze au Morogoro
 
Back
Top Bottom