Uchaguzi 2020 Kwa mara ya kwanza gharama zote za Uchaguzi Mkuu kulipwa na Serikali

Uchaguzi 2020 Kwa mara ya kwanza gharama zote za Uchaguzi Mkuu kulipwa na Serikali

Wewe mchague Lisu ili aendelee kuwaramba!

Sisi watanzania tutamchagua tena Magu ili tuendelee kujitegemea kama hivi, hatutaki kummuabudu mtu ili aje aingilie mambo yetu ya ndani ya nchi sisi.
Mkuu,
Kwenye hiyo "sisi watanzania " yako na Mm Nipo???

Naomba uniondoe.. Siwezi kumchagua jiwe.. Never

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mawazo tegemezi haya. Kwani huwa hawaleti pesa hata wanapoandikiwa "barua" kuacha kufanya hivo?

Mnapomleta Dambisa Moyo kuhusu kupinga misaada, msisahau pia kuleta tathmini za madhara yanayosababishwa na taifa kuwepo na deni kubwa la nje. Kiulinzi msaada siyo hatari kama deni kubwa la nje: Sisi tumekataa misaada lakini tumeenda kukopa fedha nyingi kwao wenyewe. Unajua kwanini kipindi cha mzee Mkapa Uchumi wa nchi ulipaa sana?

Moja ya sababu kubwa ni kusamehewa madeni ya nje (Debt Relief) ambapo sehemu kubwa ya mapato ya nchi zilipelekwa kwenye maendeleo. Sababu kubwa ya pili ni kuongezekwa kwa kiwango cha uzalishaji kilicholetwa na sera ya ubinafsishaji iliyoleta wawekezaji wa nje. Sababu ya tatu ni misaada mikubwa ya kiuchumi kutoka nje hasa mataifa ya G8.

Sasa tofauti ni ipi kama unakataa misaada halafu hapohapo unaenda kukopa kwao fedha za maendeleo?
Hivi ni asilimia ngapi ya pato la taifa ambayo hutumika kila mwaka katika kulipa madeni ya nje?
Hivi unajua hata masharti gani mengine wanaipa nchi tunapoenda kukopa hizo fedha kwao?
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za Uchaguzi Mkuu tokea tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992.

Ieleweke kuwa Mwaka 2015, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ilitumia jumla ya Shilingi 534,499,415,599/= katika zoezi zima la Uchaguzi Mkuu. Pesa kati ya hizo zilitolewa na Washirika wa Maendeleo ambao ni Umoja wa nchi za Ulaya, Uingereza na Marekani kupitia mradi wa DEP unaosimamiwa na UNDP ambapo pia walitoa vifaa kwa ajili ya uchaguzi na pia ukarabati wa Kituo cha Kuchakata taarifa za Wapiga Kura (Data Processing Center).

Kuanzia sasa mpaka Uchaguzi Mkuu, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ya Tanzania (NEC) inatarajia kutumia shilingi bilioni 331.7 kukamilisha zoezi la Uchaguzi Mkuu ambapo fedha hizo zitatolewa kupitia Mfuko Mkuu wa Hazina kwa kuzingatia kifungu cha 122 cha Sheria ya Taifa ya Uchaguzi.

Hii itakuwa ni dhana ya kujitegemea ambayo faida yake ni kuwa na uhuru wa kuamua namna ya kuendesha uchaguzi bila kuingiliwa kimaamuzi na Wanaochangia gharama za Uchaguzi!
Asante lakini nasikitika kusema kuwa huu ndo mwaka wenu wa mwisho
 
Mnapomleta Dambisa Moyo kuhusu kupinga misaada, msisahau pia kuleta tathmini za madhara yanayosababishwa na taifa kuwepo na deni kubwa la nje. Kiulinzi msaada siyo hatari kama deni kubwa la nje: Sisi tumekataa misaada lakini tumeenda kukopa fedha nyingi kwao wenyewe. Unajua kwanini kipindi cha mzee Mkapa Uchumi wa nchi ulipaa sana?

Unaikumbuka picha hii ni ya nani na ilipopigwa alikuwa anajibu nini? Kuna thread nzima humu JF inayoongea majibu yake unaweza kuitafuta; inawezekan sis tuna tuna span fupi sana na kumbukumbu na hivyo wepesi sana wa kulaumu.

1597868697206.png
 
Unaidifia serikali kwa kufanya hivyo au ni kwa vile hawana jinsi baada ya kuharibu mahusiano na wafadhiri.
 
Wewe mchague Lisu ili aendelee kuwaramba!

Sisi watanzania tutamchagua tena Magu ili tuendelee kujitegemea kama hivi, hatutaki kummuabudu mtu ili aje aingilie mambo yetu ya ndani ya nchi sisi.
Nyoko eti tujitegemee umawashwa nn ww io simu unayotumia nan katengeneza
 
Hii imekaa vibaya kwa Tundulisu sababu Ile serikal anayo iita ya kimabavu na inayo wabagua wapinzan ndio ambayo itampa hela ili afanye uchaguzi

Sent from my JKM-LX1 using JamiiForums mobile app
 
Hamjatoa kule kwenye mifuko ya hifadhi za jamii?

Mnaiba haki za wazee wetu huku mkijitapa mnajitegemea, kujitegemea gani kwa kupora haki za wengine?
Sasa unataka tufanye uchaguzi kwa raha zetu wenyewe alafu mzigo wa gharama tuwape watu wengine hiyo ni akili au uchafu emu tumieni akili nyie wapuuzi
 
Unaikumbuka picha hii ni ya nani na ilipopigwa alikuwa anajibu nini? Kuna thread nzima humu JF inayoongea majibu yake unaweza kuitafuta; inawezekan sis tuna tuna span fupi sana na kumbukumbu na hivyo wepesi sana wa kulaumu.
Msomi mzima unaacha kujibu hoja unaanza kuzungumza viroja, hili ni jambo la aibu mno kutoka kwako. Nimekuuliza swali rahisi sana naona umeishia kuzunguka mbuyu kwasababu mpaka sasa naamini huwezi kunijibu: Kuna utofauti gani pale ambapo umekataa msaada wa beberu lakini hapohapo unaenda kukopa pesa nyingi kwake huyohuyo beberu ???
 
Tatzio la wewe kutokujua jibu hilo ni la kwako; ndiyo maana mtihani ule ule huwa kuna wengine hushinda kwa maksi nyingi na wengine kushindwa kabisa. Ni afadhali ungejikita kwenye mada kuliko kuleta swala la usomi kwani mimi sikukujibu wewe kama msomi, na wala sikukuambia kuwa mimi ni msomi. Nilingia kwenye mada nikitegemea tutabadilishana mawazo na kuskilizana pande zote lakni wewe unaruka ukuta.
 
UNAFIKI WA NDEGE CHICHI-DODO: Hapendi kinyesi, lakini anakula wadudu wanaokaa kwenye kinyesi.
Mnakataa misaada ya mabeberu na kuwatukana lakini mnashangilia miradi inayotokana na mikopo ya mabeberu.
 
UNAFIKI WA NDEGE CHICHI-DODO: Hapendi kinyesi, lakini anakula wadudu wanaokaa kwenye kinyesi.
Mnakataa misaada ya mabeberu na kuwatukana lakini mnashangilia miradi inayotokana na mikopo ya mabeberu.
Hiki kikao hukiwezi
 
Ni kwasababu Magufuli kaharibu mahusiano ya nchi yetu na mataifa washirika. Kuwaita binadamu wenzako mabeberu huku ukirudiarudia kila mara ni uwendawazimu wa aina yake! Magufuli ni mbaguzi na hafai kamwe kuwa kiongozi! Havumiliki!
Hoja ya msingi hapa ni kuwa kwa mara ya kwanza serikali ya Tanzania itagharamia uchaguzi wote kwa pesa zake.

Kusema Magufuli anafaa au hafai ni mtazamo wako na una haki ya fikra hizo.
 
Wewe mchague Lisu ili aendelee kuwaramba!

Sisi Watanzania tutamchagua tena Magu ili tuendelee kujitegemea kama hivi, hatutaki kummuabudu mtu ili aje aingilie mambo yetu ya ndani ya nchi sisi.
Huyo jamaa anafurahisha sana!
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa serikali ya Tanzania kulipa gharama zote za Uchaguzi Mkuu tokea tuingie kwenye mfumo wa vyama vingi mwaka 1992...

Uchaguzi wa Mwaka 2000 pia tulitumia fedha zetu za ndani.. Natafuta magazeti ya kipindi hiko nilete kama ushahidi.
 
Back
Top Bottom