Uchaguzi 2020 Kwa mara ya kwanza gharama zote za Uchaguzi Mkuu kulipwa na Serikali

Kumbuka uchaguzi wa 2015 kulikuwa na uanfikishaji wa wapiga kura..zoezi linalohitaji pesa ndefu kuliko kupiga kura
 
Kwa hiyo hizo pesa zinakusanywa na walipa kodi!

Kwa hiyo wasiolipa kodi sio pesa zao?

Tanzania kuna vituko!
Kuna kiumbe halipi Kodi ?, Hivi unajua hata ukinunua bidhaa unalipa kodi au wewe kodi unayoijua na income tax pekee ?, hapo unapotumia hilo bundle kujibu hapa unadhani haujalipa kodi ?
 
Sasa kama washirika wamegoma kutoa fedha zao baada ya kugundua zinatumika vibaya serikali itafanyaje?
 
Hii itakuwa ni dhana ya kujitegemea ambayo faida yake ni kuwa na uhuru wa kuamua namna ya kuendesha uchaguzi bila kuingiliwa kimaamuzi na Wanaochangia gharama za Uchaguzi!
Acha propaganda hakuna cha kujitegemea wala nini, sema tu ukweli kwamba wafadhili wenu wa muda mrefu hasa UNDP wamewasusa.

Unafikiri pesa zote hizo kuingizwa kwenye uchaguzi bila kupata 'return' ni jambo jema?

Nani angekataa fedha za wafadhili kuendesha uchaguzi (kama zingekuwepo) ili hizi zetu zikatumike kwenye maeneo mengine muhimu zaidi?
 
Kwani toka awamu hii iingie madarakani kuna pesa yoyote ile walishatamka kuwa imetoka kwa mabeberu, SGR, BWAWA LA UMEME, yote walikuwa wanajitapa ni kwa pesa ya ndani hadi hapo watu waliposhituka kuona mbona deni la taifa linakuwa kila leo, ndio wakaja na pambio kuwa ni himilivu!!! Eti mbona USA, naye anakopa?!! Kukopa sio tatizo lakini kubali kuwa una kopa. Kwani hesabu ipo wazi tu ukichukua mapato ya mwezi ukitoa matumizi, picha halisi inaonekana!!!
 
Hapo hakuna cha kusifia na laiti ungejua madhara yake!
Madhara yake inabidi Watanzania waanze kuishi na wanachoweza kuzalisha. Huo ndio uwoga wenu nyie wapenda misaada. Acha tuishi kwa shida hadi akili zetu ziamke. Nimekuwa nikipinga sana sera za serikali za kiafrika za kuamini kwenye misaada.
 
Wanasaccos watanuna kusikia tumeanza kujitegemea!!
 
Ni kwa sababu Magufuli kaharibu mahusiano ya nchi yetu na mataifa washirika. Kuwaita binadamu wenzako mabeberu huku ukirudiarudia kila mara ni uwendawazimu wa aina yake! Magufuli ni mbaguzi na hafai kamwe kuwa kiongozi! Havumiliki!
Na ataendelea kuwa Rais wako kwa muda wa miaka mitano ijayo!
 
Beberu ni tusi na ni neno la kibaguzi. Hakuna lugha nyingine ya kulielezea. Watu weusi wakiitwa nyani unaona wanavyokuja juu? Vivyo hivyo kwa neno beberu
Hujui kitu nyamaza! Nenda kaendelee kutangaza vifo vya corona huko Kenya!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…