Lord denning
JF-Expert Member
- Jun 3, 2015
- 15,819
- 33,255
Mimi sio mshabiki wa Makonda, kutokana na namna ninavyomjua. Tabia zake binafsi na hulka zake ndo chanzo kikuu cha mimi kutokuwa shabiki wake na kila siku kumpinga kwenye masuala mengi sana.
Katika kumfuatilia kwangu tangu akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, then Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka alivyokuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi na sasa Mkuu wa Mkoa wa Arusha nadhani amefanya jambo moja tu ambalo naliona kama jambo la maana lenye impact chanya kwenye uchumi wa nchi.
Jambo hili ni huu ubinifu wa Land Rover Festival!
Pamoja na Rais Samia kuanza kusemwa vibaya na media za kimataifa ila tunakumbuka kuwa kwa muda wa miaka 3 sasa media hizi zilikuwa zikimsema vizuri sana hadi kuleta impact kubwa sana kwenye sekta ya utalii ambayo ndo chanzo chetu kikuu cha fedha za kigeni zinazotunisha mfuko wetu wa Benki Kuu bila kusahau uwekezaji wa kigeni (FDI)
Ni dhahili sasa kuwa, suala hili la Land Rover Festival ni ubunifu mkubwa sana katika kupiga chapuo ukuaji wa Utalii nchini Tanzania na kuufanya ukue zaidi katika siku za mbeleni na kuongeza mapato ya Taifa.
Nimependa publicity ya hili tukio na kusema kweli publicity hii ikienda hewani hadi kimataifa inaweza kuja kufanya mwaka kesho wakaja hadi waingereza na wajerumani kuja kushiriki hili Tamasha kwa kuleta magari yao.
Soma Pia: RC Makonda: Oktoba 2024 tuna maonesho ya Landcruiser, Range na Landrover 1000
Mwisho pamoja na kumpongeza Makonda kwa hii creativity na publicity yenye matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi.
Napendekeza pia Festival hii ihusishe matukio ya burudani kama vile mziki na maonyesho ya vyakula mbalimbali vya kitanzania.
Hili kusema kweli litakuza sana Utalii wetu na miaka ya mbeleni linaweza kuja kuwa Tamasha kubwa kama yale ya Carnival (Brazil) na mengineyo tunayoyafahamu Duniani.
Pili najua huu ni mwanzo ila ni vizuri Tamasha hili likawa linafanyika hata kwa Wiki nzima ili kuweka nafasi ya matukio mengi kufanyika.
Hongera Makonda. Huu ndo ubunifu tunaoutaka sio yale mambo yako ya kijinga ya kuchongea watu, ufitini, wivu wa madaraka, ufisadi, na kutafuta cheap popularity!
Keep it up!