Kwa Mara ya kwanza Napongeza Ubunifu alioufanya Makonda Arusha

Mimi sio mshabiki wa Makonda, kutokana na namna ninavyomjua. Tabia zake binafsi na hulka zake ndo chanzo kikuu cha mimi kutokuwa shabiki wake na kila siku kumpinga kwenye masuala mengi sana.

Katika kumfuatilia kwangu tangu akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, then Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka alivyokuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi na sasa Mkuu wa Mkoa wa Arusha nadhani amefanya jambo moja tu ambalo naliona kama jambo la maana lenye impact chanya kwenye uchumi wa nchi.

Jambo hili ni huu ubinifu wa Land Rover Festival!

Pamoja na Rais Samia kuanza kusemwa vibaya na media za kimataifa ila tunakumbuka kuwa kwa muda wa miaka 3 sasa media hizi zilikuwa zikimsema vizuri sana hadi kuleta impact kubwa sana kwenye sekta ya utalii ambayo ndo chanzo chetu kikuu cha fedha za kigeni zinazotunisha mfuko wetu wa Benki Kuu bila kusahau uwekezaji wa kigeni (FDI)

Ni dhahili sasa kuwa, suala hili la Land Rover Festival ni ubunifu mkubwa sana katika kupiga chapuo ukuaji wa Utalii nchini Tanzania na kuufanya ukue zaidi katika siku za mbeleni na kuongeza mapato ya Taifa.

Nimependa publicity ya hili tukio na kusema kweli publicity hii ikienda hewani hadi kimataifa inaweza kuja kufanya mwaka kesho wakaja hadi waingereza na wajerumani kuja kushiriki hili Tamasha kwa kuleta magari yao.

Soma Pia: RC Makonda: Oktoba 2024 tuna maonesho ya Landcruiser, Range na Landrover 1000

Mwisho pamoja na kumpongeza Makonda kwa hii creativity na publicity yenye matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi.

Napendekeza pia Festival hii ihusishe matukio ya burudani kama vile mziki na maonyesho ya vyakula mbalimbali vya kitanzania.

Hili kusema kweli litakuza sana Utalii wetu na miaka ya mbeleni linaweza kuja kuwa Tamasha kubwa kama yale ya Carnival (Brazil) na mengineyo tunayoyafahamu Duniani.

Pili najua huu ni mwanzo ila ni vizuri Tamasha hili likawa linafanyika hata kwa Wiki nzima ili kuweka nafasi ya matukio mengi kufanyika.

Hongera Makonda. Huu ndo ubunifu tunaoutaka sio yale mambo yako ya kijinga ya kuchongea watu, ufitini, wivu wa madaraka, ufisadi, na kutafuta cheap popularity!

Keep it up!

Lord denning
🙋‍♂️✍️🎯👍👊👏👍🙏💐🎁
 
🤣🤣🤣🤣 najua hata Makonda baada ya kusoma uzi wangu lazima akatoe sadaka kesho kanisani!

Ni jambo la kawaida tu. Sinaga bifu za kishamba.

Uadui wangu na Sukuma Gang ni kutokana na mambo yao ya kijinga na kishamba hasa kipindi kile.

Otherwise kwenye mambo mazuri sote ni Watanzania.
🤝
 
Mkuu Lord denning ,nimeipenda objectivity yako, kiukweli kabisa watu objective wa kihivi ndio watalisaidia taifa letu by positive atitude itakayozaa positivism
thanks for this
P
 
Baadae kitakufa, wakati nakuwa nilikutana na kilimo kwanza ikafa, ikaja BRN ikafa, serikali ya viwanda ikafa(viwanda mia 3 kila mkoa ya Jafo), royal tour ikafa, leo maigizo ya land rover sijui hakuna lolote, ukiambiwa budget na kitakachopatikana ni mbingu na ardhi, TRA huwa wanasema wamekusanya 3T lakini huwezi kusikia wanasoma mapato na matumizi hata siku moja ni utapeli tapeli tu
Mkuu unachosema ni kweli, ila mleta mada kasema pamoja na mapungufu yote aliyo nayo Makonda kwa hili ni ubunifu wenye tija kwa Taifa.

Na ni kweli!!

Mkuu ukumbuke kuwa hata saa mbovu kuna muda husema majira sahihi.
 
Akiwa DC wa Kinondoni kwa ushirikiano na Ruge Mutahaba alianzisha Malkia wa Nguvu na yeye kuvishwa taji ya Balkia wa Nguvu na hapa ndipo akina sisi watu wa “Kauli Umba” tukamtolea kauli humu humu JF, iliyomuumbia u RC
wa DSM Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Naomba kuheshimu mawazo yako hata kwa kuliona hili moja tuu ni mwanzo mzuri wa kumuangazia Konda Boy with positive prospective outlook kutoka kwa mtu kama wewe, it does something good for him and his endeavors on the aspect the power of positive thinking that will make this festival a big thing in future, wasiwasi wangu ni kitu kinachoitwa continuity on the part of mamlaka yake ya uteuzi, ”ukipata tuu a "limelight” kosa!, utaonekana you are trying to steals the show!unang'olewa!. Inferiority complex ni tatizo on her part!, kuna mtu alitumbuliwa uwaziri kwa kosa la kupiga picha na rais fulani!. Baada ya mwenezi kung'ara, akaonekana ana overshine, akaondolewa!, baada ya Jerry Slaa kushine ardhi, akaondolewa!, baada ya Mtaka kushine Dodoma, akatupwa Njombe!, hivyo dogo akishine sana Arachuga, hichelewi kusikia amehamishwa kuwa RC Lindi au Singida, where is the continuity?

P
Huyu hata umuanzishie mkoa wa nanjilinji atawika tu. Wampeleka simiyu uone kama sio kila siku tunaisoma simiyu humu JF na kwingineko.

Mengine ni kuacha tu atimize nyota yake kuliko kupambana nayo.
 
Akiwa DC wa Kinondoni kwa ushirikiano na Ruge Mutahaba alianzisha Malkia wa Nguvu na yeye kuvishwa taji ya Balkia wa Nguvu na hapa ndipo akina sisi watu wa “Kauli Umba” tukamtolea kauli humu humu JF, iliyomuumbia u RC
wa DSM Nimemkubali Sana DC Makonda, anafaa kuwa Mkuu wa Mkoa Dar es Salaam

Naomba kuheshimu mawazo yako hata kwa kuliona hili moja tuu ni mwanzo mzuri wa kumuangazia Konda Boy with positive prospective outlook kutoka kwa mtu kama wewe, it does something good for him and his endeavors on the aspect the power of positive thinking that will make this festival a big thing in future, wasiwasi wangu ni kitu kinachoitwa continuity on the part of mamlaka yake ya uteuzi, ”ukipata tuu a "limelight” kosa!, utaonekana you are trying to steals the show!unang'olewa!. Inferiority complex ni tatizo on her part!, kuna mtu alitumbuliwa uwaziri kwa kosa la kupiga picha na rais fulani!. Baada ya mwenezi kung'ara, akaonekana ana overshine, akaondolewa!, baada ya Jerry Slaa kushine ardhi, akaondolewa!, baada ya Mtaka kushine Dodoma, akatupwa Njombe!, hivyo dogo akishine sana Arachuga, hichelewi kusikia amehamishwa kuwa RC Lindi au Singida, where is the continuity?

P
Mkuu uko sahihi na nakuunga mkono kwa asilimia zote, shida yetu kubwa kama taifa nimuendelezo chanya kwenye mambo ya kimkakati kitaifa.

Hili likipangiliwa vizuri na likawa synchronized kwa ustadi mkubwa na royal tour, kwa hakika ndani ya muda mfupi tutakuwa mbali sana kwenye nyanja ya Utalii kikanda na kimataifa!!
 
Oooh sawa. Ila hata kwa kulichukua na kulifanya liwe namna lilivyofanywa anastahili pongezi zetu.

Nategemea kuwaona Mawaziri wa Utalii na Habari wakishiriki kulipa publicity kubwa hili tukio ili liwe na manufaa tuliyoyasema humu.
🤝💯%
 
Mkuu uko sahihi na nakuunga mkono kwa asilimia zote, shida yetu kubwa kama taifa nimuendelezo chanya kwenye mambo ya kimkakati kitaifa.

Hili likipangilia vizuri na likawa synchronized kwa ustadi mkubwa na royal tour, kwa hakika ndani ya muda mfupi tutakuwa mbali sana kwenye nyanja ya Utalii kikanda na kimataifa!!
Naunga mkono hoja, ili hili litimie,kunahitaji the people who can share such vision ili kuifanyia iendelevu. Kwa aliyokuwa anayafanya akiwa mwenezi why aliondolewa?, au Jerry Slaa kuondolewa ardhi?, where is the continuity?

P
 
Mimi sio mshabiki wa Makonda, kutokana na namna ninavyomjua. Tabia zake binafsi na hulka zake ndo chanzo kikuu cha mimi kutokuwa shabiki wake na kila siku kumpinga kwenye masuala mengi sana.

Katika kumfuatilia kwangu tangu akiwa mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, then Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, mpaka alivyokuwa Katibu Mwenezi wa Chama cha Mapinduzi na sasa Mkuu wa Mkoa wa Arusha nadhani amefanya jambo moja tu ambalo naliona kama jambo la maana lenye impact chanya kwenye uchumi wa nchi.

Jambo hili ni huu ubinifu wa Land Rover Festival!

Pamoja na Rais Samia kuanza kusemwa vibaya na media za kimataifa ila tunakumbuka kuwa kwa muda wa miaka 3 sasa media hizi zilikuwa zikimsema vizuri sana hadi kuleta impact kubwa sana kwenye sekta ya utalii ambayo ndo chanzo chetu kikuu cha fedha za kigeni zinazotunisha mfuko wetu wa Benki Kuu bila kusahau uwekezaji wa kigeni (FDI)

Ni dhahili sasa kuwa, suala hili la Land Rover Festival ni ubunifu mkubwa sana katika kupiga chapuo ukuaji wa Utalii nchini Tanzania na kuufanya ukue zaidi katika siku za mbeleni na kuongeza mapato ya Taifa.

Nimependa publicity ya hili tukio na kusema kweli publicity hii ikienda hewani hadi kimataifa inaweza kuja kufanya mwaka kesho wakaja hadi waingereza na wajerumani kuja kushiriki hili Tamasha kwa kuleta magari yao.

Soma Pia: RC Makonda: Oktoba 2024 tuna maonesho ya Landcruiser, Range na Landrover 1000

Mwisho pamoja na kumpongeza Makonda kwa hii creativity na publicity yenye matokeo chanya kwenye uchumi wa nchi.

Napendekeza pia Festival hii ihusishe matukio ya burudani kama vile mziki na maonyesho ya vyakula mbalimbali vya kitanzania.

Hili kusema kweli litakuza sana Utalii wetu na miaka ya mbeleni linaweza kuja kuwa Tamasha kubwa kama yale ya Carnival (Brazil) na mengineyo tunayoyafahamu Duniani.

Pili najua huu ni mwanzo ila ni vizuri Tamasha hili likawa linafanyika hata kwa Wiki nzima ili kuweka nafasi ya matukio mengi kufanyika.

Hongera Makonda. Huu ndo ubunifu tunaoutaka sio yale mambo yako ya kijinga ya kuchongea watu, ufitini, wivu wa madaraka, ufisadi, na kutafuta cheap popularity!

Keep it up!

Lord denning
Mwishoni Umeisahau kumkumbusha na kuacha tabia zile za kudhalilisha hata Wazee wanaoweza kumzaa !😳

Big up Land Rover festival !
Hii ndio gari niliyojifunzia Udereva 1968 😳🙄😅
 
Soma ripoti za kuanzia 2000-2016 ndiyo ulinganishe na leo, kumbuka nyuma matumizi ya internet, social media kwa Tanzania yalikuwa chini sn

Hujielewi, how is that related to Samia? Utalii uko promoted only na wa fanya Biashara, na unaharibiwa na serikali!
Kama una akili kidogo tu, utaelewa!

Kama una akili kweli, soma kichwa cha Habari na Comment yangu uliyojibu, How is Samia related to report ya 2000 na 2016? Unesahau akili yako kwa mchepuko?
 
Za chini chini inasikika eti ndio makam was Rais ajaye baada ya filipo!!
Ngoja tuone!
 
Na hii ndo free thinking sasa. Pamoja na kuyasema mapungufu yake mengi ila still nimeweza kuona zuri lake na kulisema.

Huko Chamani kwao wamejaa wenye mawazo mgando ambao hawataki kusikia mtu akimkosoa Kiongozi yeyote hata kwa ukosoaji wa kistaarabu na wenye kuleta tija katika Nchi !

Hiyo ni pamoja na yeye Makonda alivyokuwa labda awe amebadilika kwa sasa !
Kwa sababu Binadamu anabadilika 😳
Siku hazigandi !
 
Back
Top Bottom