Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Kwa mara ya kwanza natofautiana na Mange Kimambi juu ya msimamo wa Iran

Nimekuambia hicho sio kitu ni sawa tu na kuumba namba kumi ambayo ni kubwa kuliko namba kumi

Al Mustahilah
Kwa hiyo Mungu muweza yote hawezi kuumba ulimwengu ambao una namba kumi iliyo kubwa kuliko namba kumi?
 
Nchi kuendeshwa kidini ni ujinga.

Hiyo dini yenyewe inasema kwenye dini hakuna kulazimishana.

Nchi ukiiiendesha kidini unawalazimisha watu wanaotaka na wasiotaka wafuate sheria za kidini.

Huoni kuwa huo ni ujinga?
Ushauri nzuri, Sasa Tuwaambie Nini Vatican? Nchi ya Kidini inayoongozwa na Papa na Ina balozi zake dunia nzima. nchi inayoongozwa Kwa KODI za waumini wa RC dunia nzima
 
Ushauri nzuri, Sasa Tuwaambie Nini Vatican? Nchi ya Kidini inayoongozwa na Papa na Ina balozi zake dunia nzima. nchi inayoongozwa Kwa KODI za waumini wa RC dunia nzima
Mimi nimetaja dini, zote.

Wewe kama una ugomvi wako maalum na Vatican pigana nao.
 
Hata sijaelewa bila shaka maana naona unachomeka swali juu ya swali mengine hata hayaeleweki
Sasa kama hujaelewa umejibu kitu ambacho hujaelewa?

Hili ndilo tatizo hapa, uwezo wako mdogo, unajibu maswali ambayo huyaelewi.

Unajijibia tu bila hata kuelewa unajibu nini.

Tutaelewana vipi ikiwa uwezo wako wa kuelewa ni mdogo na unajibu maswali usiyoyaelewa?
 
Kwa sababu unauliza maswali yasioyoelewa labda
Hata hivyo sijaelewa swali hilo tu la mantiki
Maswali yasiyoeleweka au wewe ndiye huelewi kwa sababu uwezo wako wa kuelewa mdogo?

You are boring me now.

I have better things to do and I don't want to be bothered by stupid people.

I am placing you in my ignore list so I don't see your stupid posts.
 
Dini ndo iliwaambia Waimbe Death to israel na USA? Dini ndo iliwaambia wafadhili magaidi wa HAMAS,HEZBOLAR na HOUTH?
Hamas sio magaidi, wana gombania nchi yawo.
Hezbollah sio magaidi wanaitetea Lebanon iliyo chukuliwa na Israel kwa msaada wa US
Houth sio magaidi wandai haki zawo na wanapigwa na kuuliwa na Saudi waki saidiwa ma US
Magaidi ni Israel ilouwa watu , watoto, wazee na kupora nchi ya watu na kuwasaidiwa na US.
Kila mpenda haki anajuwa hilo na atsema hivyo na wanachotaka udhalim huo uondoke.

Nyerere alikuwa akisema hayo wakati aki support Biafra.
 
ili tujue kitendo kipi ni ugaidi, na kipi siyo..

Kwanza inabidi kufafanua "Ugaidi ni nini?" kutoka katika source "nzito nzito".
Based on definition ya ugaidi, karibu kila nchi inayopiga nchi nyingine ni gaidi, hususani ikisababisha hofu, maafa, vifo kwa civilians.
ila mjadala ni mpana sana huu.

S5202603161837312.png
S20203161840022.png
S220203161839252.png
S3202603161838522.png
Chapter 5 International Terrorism

BBC Audio | Rethink | Rethink...the meaning of terrorism
 
Wewe nawe bendera fuata upepo tu...

Nani kakuambia kuwa huyo mnayemwita mtume Mohammad ni mungu?

Huyo ni binadamu tu aliyejipenyeza na kujiita mtume wa mungu wakati ni mtoto aliyezaliwa kwa mapenzi ya mume na mke...

Kawa - manipulate na kuwatengenezea sheria za kidini, nanyi kwa ujinga wenu wa kutumjua Mungu wa kweli, Yehova mkaingia king na sasa mnaendelea kuabudu wanadamu...

Toka huko, umedanganyika...!!
Wapi Mtume alipojiita yeye Mungu,Au Yesu alipojiita yeye Mungu?
 
HOST NOT FOUND

Kwanza kabisa, unakubali kuwa mantiki ni kitu, na kama Mungu hajaiumba mantiki, basi hajaumba kila kitu? In fact kama hajaumba mantiki anavyotaka yeye, huyo si Mungu, kwa sababu hajaweka misingi ya vitu, amekuja kuwa makenika wa kutengeneza vitu kwa mantiki iliyokwishawekwa tayari bila yeye kuiweka?

Kwanza kabisa, swali lako linaanza kwa kudhani kuwa mantiki ni kitu kinachoweza kuwekwa pembeni kama kifaa ambacho kinaweza kuumbwa au kubadilishwa, Lakini tatizo ni kwamba kabla hata hatujauliza kama mantiki imeumbwa au haijaumbwa, tayari tunaitumia.
Hii ina maana mantiki haiji kama matokeo ya hoja, inakuja kama sharti la uwezekano wa hoja yenyewe. Hata swali lako linategemea mantiki ili liweze kuwa swali lenye maana.

Kwa hiyo ukisema kama Mungu hajaumba mantiki basi hajaumba kila kitu, tayari unafanya hoja ndani ya mfumo wa mantiki unaodhani unaweza kuwekwa nje ya mazungumzo.
Hapo ndipo kuna mgongano wa kimtazamo, Unajaribu kusimama nje ya mantiki ili kuizungumza, lakini huwezi kufanya hivyo bila kuitumia. Ni sawa na kujaribu kuthibitisha kuwa lugha si muhimu huku ukitumia lugha hiyo hiyo.

Kwa mtazamo wa kina zaidi, mantiki si kitu kinachoshindana na Mungu wala si kitu kinachomfungia.
Mantiki ni mfumo unaofanya dhana kama “uwezo”, “kuumba”, “kweli”, au hata “Mungu” ziweze kueleweka. Ukivunja mfumo huo, maneno hayo yote yanapoteza maana. Kwa hiyo kusema Mungu angeweza kubadilisha mantiki kungeondoa hata maana ya kusema Mungu anaweza kufanya kitu.

Ndiyo maana wanafalsafa wengi wanaona tatizo si kwamba Mungu hawezi kufanya contradiction, bali kwamba contradiction si kitu kinachoweza kuwepo hata kifikra. Ni mkusanyiko wa maneno usio na rejea kwenye ukweli wowote.

Kwa hiyo kwa mtazamo wa kimtazamo kabisa, mantiki si kitu kilichowekwa nje ya Mungu wala si kitu kilichotengenezwa kama kifaa.
Ni sehemu ya muundo wa ukweli unaofanya hata mazungumzo juu ya Mungu yawezekane.
Ukiondoa mantiki, huondoi tu mipaka ya Mungu, unaondoa pia uwezo wa kuuliza swali kuhusu Mungu.

Na hapo ndipo hoja inarudi mahali pa msingi, si kwamba Mungu amefungwa na mantiki, bali ni kwamba mantiki ndiyo mazingira yanayofanya neno “Mungu” liweze kusema kitu chenye maana.

Mantiki inaweza kufananishwa na pumzi kwa sababu zote mbili ni vitu ambavyo mara nyingi hatuvitambui moja kwa moja, lakini bila hivyo hakuna kitu kingine kinaweza kuendelea.
Mtu anaweza kuzungumza, kufikiri, au kujenga hoja, lakini kila kitu hicho kinategemea pumzi yake kuendelea.

Vivyo hivyo, mtu anaweza kuuliza maswali, kukataa hoja, au kujenga nadharia, lakini kila kitu hicho kinategemea mantiki ili kiwe na maana.

Tofauti pekee ni kwamba pumzi ni kitu cha kibiolojia kinachowezesha uhai wa mwili, wakati mantiki ni mfumo unaowezesha uhai wa maana. Bila pumzi mwili unakufa; bila mantiki, maana ya maneno inakufa. Ndiyo sababu hata mtu anayepinga mantiki bado analazimika kuitumia ili apinge.

karibu Tujadili hapa kwanza Mkuu,
 
Kwanza kabisa, swali lako linaanza kwa kudhani kuwa mantiki ni kitu kinachoweza kuwekwa pembeni kama kifaa ambacho kinaweza kuumbwa au kubadilishwa, Lakini tatizo ni kwamba kabla hata hatujauliza kama mantiki imeumbwa au haijaumbwa, tayari tunaitumia.

Hili suala sielewi umuhimu wake unatoka wapi kwa muktadha wa maongezi ya Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote, upendo wote na muumba yote.

Swali hili lina umuhimu tu kama tunajiongelea sisi watu, ambao tunaitumia mantiki. Lakini, kama Mungu huyo yupo, aliyeumba kila kitu, huyo Mungu hayuko chini ya mantiki, yeye ndiye anatakiwa kuwa kaiumba mantiki.

Hii ina maana mantiki haiji kama matokeo ya hoja, inakuja kama sharti la uwezekano wa hoja yenyewe. Hata swali lako linategemea mantiki ili liweze kuwa swali lenye maana.

Sawa, lakini hapa hatuongelei swali langu tu, tunamuongelea Mungu muweza yote, mwenye upendo wote, mjuzi wa yote, aliyeumba yote, ambaye kaiumba hata hiyo mantiki. Kama hajaiumba mantiki si muweza yote wala muumba vyote. Huyo Mungu si subject kwa mantiki, yeye ndiye aliyeamua mantiki iwe hivyo ilivyo.

Kwa hiyo ukisema kama Mungu hajaumba mantiki basi hajaumba kila kitu, tayari unafanya hoja ndani ya mfumo wa mantiki unaodhani unaweza kuwekwa nje ya mazungumzo.

Hoja ni kwamba Mungu muumba yote kaumba mantiki pia. Na kama hajaumba mantiki hajaumba vyote. How do you dispute that?

Sijafanya hoja ndani ya mfumo wa mantiki ninaodhani unaweza kuwekwa nje ya mazungumzo, naonesha kuwa hoja ya kuwepo Mungu muumba yote haipo kimantiki na ina contradiction. This is immanent critique that you are failing to read well and comprehend.

I am showing you that the idea of an omnipotent, omniscient God who is subject to logic is a logical contradiction.

Hapo ndipo kuna mgongano wa kimtazamo, Unajaribu kusimama nje ya mantiki ili kuizungumza, lakini huwezi kufanya hivyo bila kuitumia. Ni sawa na kujaribu kuthibitisha kuwa lugha si muhimu huku ukitumia lugha hiyo hiyo.

Hakuna niliposimama nje ya mantiki ili kuizungumzia, nakuonesha kuwa maelezo ya kuwepo kwa Mungu muweza yote ambaye yuko subject to mantiki ni contradiction.

I am showing a logical contradiction, how is that standing outside of logic?

Tatizo huelewi immanent critique ni nini. Ninaposema "Let x be equal to y" in order to show you that x is not equal to y further ahead, you are stuck at criticicing me for equating x to y.

Kwa mtazamo wa kina zaidi, mantiki si kitu kinachoshindana na Mungu wala si kitu kinachomfungia.

Mantiki haishindani na Mungu kwa sababu Mungu hayupo, na mimi nakuonesha kuwa Mungu hayupo kwa kutumia mantiki, huelewi wapi?
Mantiki ni mfumo unaofanya dhana kama “uwezo”, “kuumba”, “kweli”, au hata “Mungu” ziweze kueleweka.

Mpaka sasa hujaweza kuthibitisha Mungu yupo kwa kutumia mantiki.

Ukivunja mfumo huo, maneno hayo yote yanapoteza maana. Kwa hiyo kusema Mungu angeweza kubadilisha mantiki kungeondoa hata maana ya kusema Mungu anaweza kufanya kitu.

Hujaelewa tofauti ya mantiki na mantiki hii. Una anthropic bias ya kufikiri kwamba mantiki ni lazima iwe mantiki hii.

Umeshasoma vitabu vya Lewis Carrol? Umesoma Alice in Wonderland na Through The Looking Glass?

Mantiki ni mfumo wenye consistency. Usikatae mantiki ambayo iko tofauti na ya dunia hii just because iko tofauti. Ukifanya hivyo unaweza kukataa mantiki ya non-Eclidean geometry ambayo ina mstari mnyoofu wenye nyuzi pungufu au zaidi ya 180, pembetatu yenye nyuzi pungufu au zaidi ya 180, na mistari parallel inayokutana.

Wewe unakataa kitu kuwa hakina mantiki kwa sababu tu kina mantiki tofauti.

Mungu muweza yote anatakiwa asishindwe kuumba ulimwengu ambao una mantiki na namba kumi ni zaidi ya namba kumi. That should be possible kwa mantiki mpya atakayoijenga, ingawa hiyo si sawa kwa mantiki ya dunia hii. Anatakiwa aweze kujenga number system kwa mantiki hiyo.

Ndiyo maana wanafalsafa wengi wanaona tatizo si kwamba Mungu hawezi kufanya contradiction, bali kwamba contradiction si kitu kinachoweza kuwepo hata kifikra. Ni mkusanyiko wa maneno usio na rejea kwenye ukweli wowote.

Hiyo ni limitation ya kifikiri, failure of imagination. Ukishasema Mungu muweza yote, maana yake huyo Mungu si subject kwa logic, yeye ndiye anatengeneza logic, maana yake anaweza kuumba ulimwengu ambao mambo yote unayoyaona ni contradiction yakawa tautology halafu mambo yote unayoyaona ni tautology yakawa contradiction.

Umejifunga sana katika anthropic bias. Yani wewe ni kama mtu ambaye umeshafundishwa kwamba, katika dunia hii, maisha yote yanatokana na element ya carbon.

Kwa hivyo ushakariri ili kitu kiweze kuishi, inabidi kiwe carbon based.

Wakati, katika kemia, hakuna sheria zinazozuia maisha kuwa silicon based.

Kwa hiyo kwa mtazamo wa kimtazamo kabisa, mantiki si kitu kilichowekwa nje ya Mungu wala si kitu kilichotengenezwa kama kifaa.
Ni sehemu ya muundo wa ukweli unaofanya hata mazungumzo juu ya Mungu yawezekane.
Ukiondoa mantiki, huondoi tu mipaka ya Mungu, unaondoa pia uwezo wa kuuliza swali kuhusu Mungu.

Hakuna ninapoondoa mantiki. Mbona hunielewi? Mimi nasimamia mantiki. Naonesha kuwa wazo la kuwepo Mungu halina mantiki, kwa kuwa Mungu huyo, muweza yote, alitakiwa kuwa na uwezo wa kuumba ulimwengu wenye mantiki inayoendana na sifa zake za uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote.

Ulimwengu tunaouona, kwa kuruhusu mabaya kuwapo, una onesha contradiction kati ya ulimwengu na sifa hizo za Mungu.

Siondoi mantiki, nazama kwa kina zaidi katika mantiki kuonesha kuwa Mungu muweza yote halazimishwi na mantiki kuumba hivi, angeweza kuumba ulimwengu usio na contradiction.

Mimi nasimamia mantiki kwa kina kikubwa sana, si tu logic, bali meta-logic. Yani mifumo yote inayoweza kuwa na consistency, sio huu tu, sio Euclidean geometry tu, hata non-Euclidean geometries zote.

You are stuck on this logic, this Euclidean geometry. Ndiyo maana hatuelewani.

Na hapo ndipo hoja inarudi mahali pa msingi, si kwamba Mungu amefungwa na mantiki, bali ni kwamba mantiki ndiyo mazingira yanayofanya neno “Mungu” liweze kusema kitu chenye maana.

Mungu alilazimiska kuumba hivi kwa mantiki hii au aliweza kuumba vyovyote kwa mantiki yoyote aliyoitaka?

Mantiki inaweza kufananishwa na pumzi kwa sababu zote mbili ni vitu ambavyo mara nyingi hatuvitambui moja kwa moja, lakini bila hivyo hakuna kitu kingine kinaweza kuendelea.
Mtu anaweza kuzungumza, kufikiri, au kujenga hoja, lakini kila kitu hicho kinategemea pumzi yake kuendelea.

Logical non sequiture fallacy, anthropic bias. The non living world can go on without pumzi but cannot go on without logic.

Vivyo hivyo, mtu anaweza kuuliza maswali, kukataa hoja, au kujenga nadharia, lakini kila kitu hicho kinategemea mantiki ili kiwe na maana.

Sawa, alkini mantiki ipi? Mantiki ambayo ingeweza kuwa si hii moja tu. Kama vile ambavyo ulimwengu ambao ungeweza kuwa si huu mmoja tu wenye three spatial dimension and one of time.

Tungewea kuwa na ulimwengu wenye dimensions tatu za time na moja ya space ambao kila unachokiona leo ni contradiction kikawa tautology na kila unachokiona leo tautology kikawa contradiction. Katika ulimwengu huo, namba zote ni sawa na kumi ila kumi tu si sawa na kumi. Mungu muweza yote angetaka kuumba ulimwengu huo uwe logically consistent, angefanya. Ulimwengu huo hau make sense katika ulimwengu huu na mantiki yetu, lakini angeamua u make sense katika ulimwengu huo, unge make.

Tofauti pekee ni kwamba pumzi ni kitu cha kibiolojia kinachowezesha uhai wa mwili, wakati mantiki ni mfumo unaowezesha uhai wa maana. Bila pumzi mwili unakufa; bila mantiki, maana ya maneno inakufa. Ndiyo sababu hata mtu anayepinga mantiki bado analazimika kuitumia ili apinge.

This alone makes your analogy a logical non sequiture fallacy and anthropic bias.

karibu Tujadili hapa kwanza Mkuu,

Karibu na wewe.
 
Back
Top Bottom