HOST NOT FOUND
Mkuu, nakushukuru pia kwa namna unavyojaribu kuweka hoja zako kwa kina.
Lakini nadhani kuna sehemu kadhaa katika hoja yako ambazo zinaonekana kuwa na nguvu kwa juu, lakini zikichunguzwa kwa makini zinaacha maswali makubwa.
Kwanza umechukua wazo kwamba kama Mungu ameumba kila kitu basi hata mantiki ameiumba, kwa hiyo angeweza kuweka mantiki ambayo inaruhusu ulimwengu usio na mabaya.
Hapa kuna tatizo dogo la falsafa ambalo limejadiliwa sana kwa muda mrefu.
Kwanza kabisa, unakubali kuwa mantiki ni kitu, na kama Mungu hajaiumba mantiki, basi hajaumba kila kitu? In fact kama hajaumba mantiki anavyotaka yeye, huyo si Mungu, kwa sababu hajaweka misingi ya vitu, amekuja kuwa makenika wa kutengeneza vitu kwa mantiki iliyokwishawekwa tayari bila yeye kuiweka?
Mantiki si kitu kinachofanya kazi kama sheria za fizikia ambazo mtu anaweza kuzibadilisha.
Mantiki ni masharti ya uwezekano wa kitu kuwa na maana kabisa.
Na hilo ndilo linamfanya yule asiye na uamuzi wa mantiki iweje asiwe Mungu. Hiki ndicho kinamtenganisha Mungu na wengine wanaoweza kutengeneza vitu katika mantiki iliyopo tayari.
Kama tukisema kitu kinaweza kuwa na sifa mbili zinazopingana kwa wakati mmoja, hatujapanua mantiki, tumefuta maana ya maneno yenyewe. Ndiyo maana hata wanafalsafa wengi wanaosema Mungu ana uwezo wote bado wanakubali kwamba uwezo wote haujumuishi kufanya mambo yenye contradiction, kwa sababu contradiction si “kitu” kinachoweza kufanyika.
This is just your anthropic bias derived from this universe. Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote, kimantiki, anatakiwa asishindwe kuumba ulimwengu ambao unachokiona wewe leo kuwa ni logically consistent kiwe contradiction, na unachokiona wewe leo contradiction kiwe logically consistent. Niyo maana ya Mungu muweza yote hiyo. Ukisema hawezi hilo, basi si muweza yote huyo. Huelewi wapi?
Mfano wako wa Euclidean na non-Euclidean geometry unaonekana mzuri, lakini ukichunguza kwa makini hauonyeshi kuvunjika kwa mantiki. Non-Euclidean geometry haivunji mantiki; inabadilisha tu postulates za kijiometri kuhusu nafasi.
Kwanza, hata ulimwengu ambao hauruhusu mabaya hauvunji mantiki. Unasogeza tu postulates za mantiki, badala ya mazuri na mabaya kuwezekana, yanawezekana mazuri tu. Sasa hapo mantiki imevunjika vipi?
Pili, hata kama kuna mantiki inavunjika, hiyo ni mantiki ya ulimwengu huu. Mungu mwenye uwezo wote anatakiwa asishindwe kuumba ulimwengu mwingine wenye mantiki nyingine. Kwa nini unafanya mantiki ya ulimwengu huu ndiyo iwe mantiki pekee?
Unafanya kama vile kwa kuwa kwenye ulimwengu huu tuna three dimensions of space and one of time basi Mungu hawezi kuumba ulimwengu wenye three dimensions of time and one of space?
Ndani ya kila mfumo bado kuna consistency kali sana ya mantiki. Hakuna sehemu ambapo pembetatu inaweza kuwa na nyuzi 180 na pia isiwe 180 kwa wakati mmoja katika mfumo ule ule.
Sawa. Lakini hilo halimaanishi kwamba hakuna mfumo ambao pembetatu haina nyuzi 180. Upo.Ndio hiyo mifumo ya non-Euclidean geometry.
Sasa kwa nini unalazimisha Mungu hawezi kuumba ulimwengu wa non-Euclidean geometry, kwa sababu tu ulimwengu unaoujua wewe ni wa Euclidean geometry?
Kwa hiyo mfano huo unaonyesha kwamba tunaweza kuwa na mifumo tofauti ya kanuni, lakini hauthibitishi kwamba tunaweza kuwa na mfumo ambao unaruhusu contradiction ya moja kwa moja.
Kwanza kabisa siongelei mfumo unaoruhusu contradiction yoyote. Ulimwengu ambao hauruhusu mabaya hauruhusu contradiction yoyote. In fact huu ulimwengu unaoruhusu mabaya ndio unaruhusu contradiction, una contradict the existence of an all knowing, all capable, and all loving God.
Ulimwengu ambao hauruhusu mabaya una contradiction gani?
Sasa tukirudi kwenye hoja kuu, ulimwengu ambao mabaya hayawezekani kabisa.
Ili hilo liwe kweli, kuna uwezekano mbili tu, Ama viumbe hawana kabisa uwezo wa kuchagua tofauti na kile kinachotokea, au wana uwezo huo lakini hawawezi kamwe kuchagua mabaya.
Ulimwengu huo hauna mabaya, mabaya hayapo, hayawezi hata kufikirika, suala zima la kuchagua mabaya halipo kwa sababu mabaya hayafikiriki.
Kama hawana kabisa uwezo wa kuchagua, basi dunia hiyo ni kama programu iliyofungwa.
Dunia zote, au angalau hata hii, ni kama programu zilizofungwa. Ndiyo maana wewe leo ukitaka kurudi nyuma kwenye muda huwezi. Ukitaka uchague uwe mtu ambaye hajazaliwa huwezi. Kwa hiyo hii si point.
This is a moot superficial point. Kwa sababu unataka kuifanya dunia hiyo kama special imefungwa, wakati hata hii iko hivyo hivyo. Dunia hiyo haina u special.
Hakuna tatizo la mantiki hapo, lakini pia hakuna kitu kinachoitwa mema ya kimaadili, kwa sababu mema ya kimaadili yanahusisha uwezo wa kuchagua kati ya njia mbadala. Mfumo wa roboti wanaofanya mema kwa lazima hauna mema ya kimaadili, una utaratibu tu.
Si kweli. Kunaweza kuwa na dunia mabayo ina mema tu bila mabaya, kama vile ambavyo tunaweza kuwa na dunia ambayo muda unakwenda mbele tu, haurudi nyuma.
Umesema pia kwamba uhuru wa kuchagua ni “illusion”.
Hoja hiyo iko karibu na mtazamo wa determinism katika falsafa.
Lakini hata wanaounga mkono determinism mara nyingi wanakubali kitu kinachoitwa compatibilism, kwamba hata kama matukio mengi yana sababu za awali, bado kuna tofauti kati ya kitendo kinachotoka ndani ya nia ya mtu na kitendo kinacholazimishwa kutoka nje.
Hata kama nikikubali freewill kuwapo, kwa immanent critique, freewill nayo inatuonesha haiwezekani kuwao freewill kwa mtu na Mungu mjuzi wa yote akawepo. The two are mutuallu exclusive.
Mimi hoja yangu ni kwamba huyu Mungu ana contradictions nyingi zinazoonesha hayupo, hii ndiyo hoja kuu.
Hata nikikubali tuna uamuzi wa kufanya mambo kw afreewill, hilo nalo linaonesha Mungu mjuzi wa yote hayupo.
Yani kama mimi nina uhuru wa kuamua nakata kulia au kushoto, kabla sijakata, ili niwe na uhuru kweli, Mungu anatakiwa asijue nitaamua vipi. Akishajua tu nitaamua vipi, maana yake mimi sina uhuru kamili hapo.
Mfano rahisi wa maisha halisi, mtu anayekupa pesa kwa hiari na mtu anayekupa pesa kwa sababu amewekewa bunduki kichwani. Katika hali zote mbili kuna sababu zilizotangulia, lakini bado tunatambua tofauti ya kimaadili kati ya vitendo hivyo viwili.
The whole freewhill discussion is moot in the larger context, kwa sababu hata nikikubali tuna freewill, hilo linaonesha Mungu mwenye ujuzi wote hayupo.
Human freewill and God's perfect knowledge are mutually exclusive. You can have one or the other, but you can't have both.
Hapo ndipo dhana ya uchaguzi inaingia katika maana ya kimaadili, hata kama si “uhuru usio na mipaka”.
Hata nikikukubalia tuna freewill, hilo nalo linaonesha Mungu mjuzi wa yote hayupo.
Pia hoja yako inasema kwamba kama ulimwengu usio na mabaya ni logically possible basi Mungu angeweza kuuumba.
Sijasema hivyo, hujanielewa.
Nimesema Mungu muweza yote anatakiwa asishindwe kuumba ulimwengu ambao mabaya hayawezekani. Kuna tofauti. Framing yako inamfanya Mungu awe subject to logic. Mimi nakataa hili. Mungu muweza yote si subject to logic, yeye ndiye anaiuba logic.
Lakini hapa kuna hatua nyingine ya mantiki ambayo bado haijathibitishwa, kwamba ulimwengu huo unaweza kuwa na aina ile ile ya viumbe wenye maisha ya kiakili, mahusiano, kujifunza, na ukuaji wa maadili kama tunavyojua.
Je, ulimwengu usio na mabaya utakuwa na viumbe walewale? Why is this question important?
Ukiwa na mtoto mchanga, ambaye anaweza kuchagua sumu imuue au maziwa yampe lishe bora, utampatia sumu na maziwa achague mwenyewe, kwa sababu, usipompatia sumu na maziwa hatakuwa mtoto yuleyule? Au utahakikisha hapati sumu, anapata maziwa tu?
Katika sayansi na historia ya maisha tunaona kitu cha kuvutia sana, karibu kila mfumo unaoruhusu maendeleo, ubunifu, na uhuru fulani pia unaruhusu hatari na uwezekano wa makosa.
Mfano rahisi ni teknolojia. Internet imeruhusu maarifa kusambaa duniani, lakini pia imeruhusu udanganyifu na propaganda.
Mfumo unaoruhusu uhuru mkubwa wa mawasiliano hauwezi wakati huo huo kuondoa kabisa uwezekano wa matumizi mabaya bila kuondoa uhuru wenyewe.
So many logical fallacies here. Logical non sequitur. Problem of induction.
Una maana Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anashindwa kuumba ulimwengu wenye mfumo unaovutia kuhusu huu kwa kuwa na mazuri tu, bila mabaya? Ameshindwa kuumba ulimwengu unaoruhusu uhuru katika mazuri tu, bila mabaya?
Hivyo inawezekana kabisa kwamba ulimwengu unaoruhusu aina fulani ya uhuru wa viumbe wenye akili lazima pia uruhusu uwezekano wa mabaya. Hilo si kudai kwamba mabaya ni mazuri, bali kwamba uwezekano wake unaweza kuwa sehemu ya masharti ya kuwepo kwa viumbe huru.
Inawezekana au lazima?
Mungu mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote alilazimika kuruhusu mabaya ili kuruhusu uhuru?
Alishindwa kuumba ulimwengu wenye uhuru wa kufanya mema tu, bila mabaya?
Halafu kwa nini mnafikiri mabaya ni mambo ya kutenda tu? Hamuelewi kuwa kuna mabaya ya kiasili kama ma natural disasters? Was it necessary to have a world with dangerous natural disasters? Ilimlazimu Mungu kuumba hivi ulimwengu wenye ma natural disasters?
Sehemu ya mwisho ya hoja yako inasema kwamba kama ulimwengu huo ni logically impossible basi Mungu hana uwezo wote.
Lakini hapa kuna mkanganyiko mdogo, Katika falsafa ya uwezo wote, “uwezo wote” umeelezwa mara nyingi kama uwezo wa kufanya yote ambayo ni logically possible.
Huo si uwezo wote, huo ni uwezo wa kufanya yaliyo logically possible.
Hii dhana nzima ya Mungu muweza yote ni uongo tu. Na hata huyo anayesemwa kuweza kufanya yaliyo logically possible tunaona story ya kuwepo kwake inaji contradict, Mungu anapata hasira, sasa Mungu mjuzi wa yote, mwenye uwezo wote na upendo wote anapataje hasira?
Hilo si kupunguza nguvu ya Mungu bali ni kutambua kwamba contradiction si kitu halisi.
Contradiction si kitu halisi, Mungu ana contradiction na Mungu si kitu halisi, ni hadithi tu. Huelewi wapi?
Ni kama kusema Mungu hawezi kufanya “duara la pembe nne”. Hapo si kwamba uwezo wake una mipaka; ni kwamba kitu hicho hakina maana inayoweza kutekelezwa.
Mungu hawezi kufanya duara la pembe nne, kwa sababu hayupo.
Angekuwapo, angeweza kuumba ulimwengu wenye spacetime inayoruhusu duara la pembe nne.
Tumeona katika Euclidean Geometry tulifundishwa mistari parallel haikutani kamwe, tukaona katika non-Euclidean geometry mistaru parallel kama longitudes zote inakutana at the south and noth poles.
So, the problem here is your lack of imagination and your anthropic bias.
Kwa hiyo hoja yako inaleta swali zuri sana kuhusu uhusiano kati ya sifa za Mungu na uwepo wa mabaya.
Lakini ili hoja iwe kali kabisa bado inahitaji kuonyesha mambo mawili, kwamba ulimwengu wenye viumbe wanaofanya mema lakini ambao hawawezi kabisa kufanya mabaya ni logically coherent, na kwamba ulimwengu huo unaweza kuwa na aina ile ile ya maisha yenye maana kama tunavyojua.
Kwa nini ulimwengu huo usiwe logically coherent? Kuna kanuni gani ya mantiki utavunja? Na hata ukivunja kanuni ya mantiki, kwa nini unafikiri Mungu muumba vyote, mwenye uwezo wote, ujuzi wote na upendo wote anashindwa kuumba ulimwengu wenye mantiki tofauti?
Je, anayelazimika kufuata mantiki iliyopo bila kuweza kuiumba yeye au kuibadilisha ni Mungu muweza yote?
N akwa nini viumbe kuwa wale wale ni muhimu kuliko viumbe kuwa salama?
Kwa nini mtoto wako mchanga kuwa na uhuru wa kuchagua sumu au maziwa ni muhimu kuliko mtoto huyo kukosa uhuru huo na kuwa na maziwa tu awe salama?
Bila kuonyesha hilo, bado kuna uwezekano mkubwa kwamba kile unachokiita ulimwengu “usio na mabaya” kinaweza kuondoa masharti yale yale yanayofanya mema ya kimaadili yawe na maana.
Hapa hakuna hoja, ni anthropic bias tu. Maana ni nini? Mungu muweza yote, mjuzi wa yote na mwenye upendo wote akitaka kugeuza maana ya maana atashindwa?
Akishindwa, je, huyo ni uweza yote kweli?
Akiweza, swali lako lina umuhimu kweli?
Na wewe pia.